Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake
Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Hivi leo hii nyinyi si mnapata chakula na kinywaji mkitakacho? Kwa hakika mimi nilimuona Nabii wenu rehema na amani ziwe juu yake inafika mahala hapati hata tende mbovu ya kutosha kujaza tumbo lake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, maisha waliyonayo watu miongoni mwa neema, na kwamba wao muda wote wana uhakika wa chakula na kinywaji kwa kiwango watakacho, kisha akaeleza kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba alikuwa hapati katika tende mbovu kiasi cha kujaza tumbo lake kutokana na njaa.
Mafunzo
Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuipa nyongo Dunia.
Himizo la kuipa nyongo Dunia, na kuipunguza kwa kadiri iwezekanavyo, na kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Kuwakumbusha watu neema walizonazo, na kuwahimiza wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2284) (2977).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 537).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 421).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 300).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 370).
كشف المشكل، لابن الجوزي (2/ 216).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com