Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ وَجَنَّةُ الْكَافِرِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba maisha ya Dunia kwa muumini ni kama Gereza analoishi kwa amri za kisheria, kama kufanya maamrisho na kuacha makatazo, basi akifa anapumzika na haya na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, katika neema za kudumu, nayo kwa Kafiri ni kama Pepo; kwa sababu anafanya ndani yake kila inachotamani nafsi yake na kuamrishwa na matamanio yake, basi akifa anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama miongoni mwa adhabu za kudumu.

Mafunzo
  1. Amesema Nawawi: Kila muumini ni mfungwa, amezuiliwa katika dunia kuyaendea matamanio yaliyoharamishwa pamoja na machukizo, amelazimishwa kufanya matendo ya utiifu na magumu, basi akifa anapumzika na haya, na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu kwake miongoni mwa neema za kudumu, na raha halisi isiyokuwa na mapungufu, na ama Kafiri basi yeye huyamiliki hayo aliyoyapata katika starehe za dunia, pamoja nakuwa ni machache, na yamejawa tabu ziilizojaa vikwazo mbali mbali, hivyo, anapokufa anaingia katika adhabu ya kudumu, na mateso ya milele.
  2. Amesema Assanadi: Kauli yake: "Gereza la Muumini" Bila shaka hata kama ndani yake kuna neema, basi Pepo ni bora kwake kuliko hizo, "Na Pepo ya Kafiri" Basi hata kama kuna machukizo ila Moto ndio shari zaidi kwake kuliko hayo.
  3. Udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Dunia ni nyumba ya majaribu na mitihani kwa wenye imani.
  5. Kafiri ameiwahisha Pepo yake Duniani; akaadhibiwa kwa kunyimwa Pepo Akhera na neema zake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2272) (2956). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 535). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 419). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 367). موسوعة فقه القلوب، لمحمد التويجري (4/ 3471). كتاب العلم، لابن عثيمين (ص37).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kuipa nyongo Dunia na Kujiepusha na yaliyo haramu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com