Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuipa nyongo Dunia na Kujiepusha na yaliyo haramu.

Hadithi 8

Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ وَجَنَّةُ الْكَافِرِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba maisha ya Dunia kwa muumini ni kama Gereza analoishi kwa amri za kisheria, kama kufanya maamrisho na kuacha makatazo, basi akifa anapumzika na haya na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, katika neema za kudumu, nayo kwa Kafiri ni kama Pepo; kwa sababu anafanya ndani yake kila inachotamani nafsi yake na kuamrishwa na matamanio yake, basi akifa anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama miongoni mwa adhabu za kudumu.

Mafunzo
  1. Amesema Nawawi: Kila muumini ni mfungwa, amezuiliwa katika dunia kuyaendea matamanio yaliyoharamishwa pamoja na machukizo, amelazimishwa kufanya matendo ya utiifu na magumu, basi akifa anapumzika na haya, na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu kwake miongoni mwa neema za kudumu, na raha halisi isiyokuwa na mapungufu, na ama Kafiri basi yeye huyamiliki hayo aliyoyapata katika starehe za dunia, pamoja nakuwa ni machache, na yamejawa tabu ziilizojaa vikwazo mbali mbali, hivyo, anapokufa anaingia katika adhabu ya kudumu, na mateso ya milele.
  2. Amesema Assanadi: Kauli yake: "Gereza la Muumini" Bila shaka hata kama ndani yake kuna neema, basi Pepo ni bora kwake kuliko hizo, "Na Pepo ya Kafiri" Basi hata kama kuna machukizo ila Moto ndio shari zaidi kwake kuliko hayo.
  3. Udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Dunia ni nyumba ya majaribu na mitihani kwa wenye imani.
  5. Kafiri ameiwahisha Pepo yake Duniani; akaadhibiwa kwa kunyimwa Pepo Akhera na neema zake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2272) (2956). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 535). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 419). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 367). موسوعة فقه القلوب، لمحمد التويجري (4/ 3471). كتاب العلم، لابن عثيمين (ص37).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لو كان لي مِثْلُ أحدٍ ذهبًا، لسرني أن لا تمر عليَّ ثلاث ليالٍ وعندي منه شيءٌ إلا شيء أرْصُدُهُ لِدَيْنٍ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-Amesema: "Lau kama ningekuwa na dhahabu kubwa mfano wa mlima Uhudi, basi ningependa zisipite siku tatu nikiwa namiliki chochote katika mali hiyo zaidi ya kile ninachokihifadhi kwaajili ya kulipa madeni".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim na tamko ni la BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Lau kama ningekuwa ninamiliki katika mali kiasi cha dhahabu halisi kama mlima Uhudi, basi ningekitoa chote katika njia ya Mwenyezi Mungu, na nisingebakisha katika mali hiyo ila kiasi ninachokihitaji kwa kukidhi mahitaji, na kulipa madeni ninayodaiwa.

Marejeo

كنوز رياض الصالحين، أ.د. حمد بن ناصر بن عبد الرحمن العمار، دار كنوز اشبيليا، الطبعة الأولى : 1430 هـ. منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، المؤلف: حمزة محمد قاسم، راجعه: الشيخ عبد القادر الأرناؤوط، عني بتصحيحه ونشره: بشير محمد عيون، الناشر: مكتبة دار البيان، دمشق - الجمهورية العربية السورية، مكتبة المؤيد، الطائف - المملكة العربية السعودية عام النشر: 1410 هـ - 1990 م. نزهة المتقين، د. مصطفى سعيد الخن، د. مصطفى البغا، محي الدين مستو، علي الشرجبي، محمد أمين لطفي، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة الأولى : 1397 هـ 1977 م، الطبعة الرابعة عشر 1407 هـ 1987م. شرح رياض الصالحين، المؤلف: محمد بن صالح بن محمد العثيمين، الناشر: دار الوطن للنشر، الرياض، الطبعة: 1426 هـ. رياض الصالحين، د. ماهر بن ياسين الفحل، الناشر: دار ابن كثير للطباعة والنشر والتوزيع، دمشق - بيروت، الطبعة: الأولى، 1428 هـ - 2007 م. صحيح مسلم، المؤلف: مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت. صحيح البخاري، المؤلف: محمد بن إسماعيل أبو عبدالله البخاري الجعفي، المحقق: محمد زهير بن ناصر الناصر، الناشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda

عَنْ أَبِي العَبَّاسِ سَهْلِ بْنِ سَعِدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ، فَقَالَ: «ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النَّاسُ».
Kutoka kwa Abul Abbasi Sahli bin Sa'di As-saai'diy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nijulishe amali ambayo nikiifanya atanipenda Mwenyezi Mungu na watu watanipenda, akasema: "Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda".
Imepokelewa na Ibn Majah na wengineo kwa sanadi nzuriDarajaAmesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan
Maelezo

Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali ambayo akiifanya Mwenyezi Mungu atampenda na watu watampenda, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Atakupenda Mwenyezi Mungu utakapoacha yasiyo na msingi katika Dunia, na yale yasiyokunufaisha katika Akhera, na ukaacha yale yanayoweza kuwa na madhara katika dini yako, na watu watakupenda utakapoyapa nyongo yaliyoko mikononi mwao miongoni mwa vitu vya kidunia; kwa sababu wanayapenda kulingana na tabia zao za asili, na atakayebanana nao katika hayo watamchukia, na atakayewaachia watampenda.

Mafunzo
  1. Ubora wa kuipa nyongo dunia, nayo: Ni mtu kuacha yasiyofaa katika Akhera.
  2. Kuipa nyongo dunia daraja yake ni kubwa kuliko unyenyekevu; kwa sababu unyenyekevu ni kuacha mambo ambayo huenda yakakudhuru, na kuipa nyongo dunia ni kuacha yasiyofaa katika Akhera.
  3. Amesema Assanadi: Hakika Dunia inapendeka kwa watu, yeyote atakayepambana nao humo atachukiza kwao kwa kadiri ya hilo, na atakayewaacha na hicho wanachokipenda atapendeka ndani ya nyoyo zao kwa kiwango cha hilo.
Marejeo

الأربعون النووية (ص118) (ح31). سنن ابن ماجه (5/ 225) (4102). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص73). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين (ص111). الفوائد المستنبطة من الأربعين النووية، للشيخ عبد الرحمن البراك (ص87). الأحاديث الأربعون النووية وعليها الشرح الموجز المفيد، لعبد الله بن صالح المحسن (1/61).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayeamka miongoni mwenu akiwa na afya njema katika mwili wake, akiwa na amani katika mji wake, na anamiliki chakula cha siku yake hiyo, basi atakuwa ni kama kakusanyiwa dunia (yote)

عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ مِحْصَنٍ الْأَنْصَارِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ مُعَافى فِي جَسَدِهِ، آمِنًا فِي سِرْبِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا».
Kutoka kwa Ubaidillaah bin Mihswan Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeamka miongoni mwenu akiwa na afya njema katika mwili wake, akiwa na amani katika mji wake, na anamiliki chakula cha siku yake hiyo, basi atakuwa ni kama kakusanyiwa dunia (yote)".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayeamka miongoni mwenu enyi waislamu akiwa mzima wa afya katika mwili wake akiwa amesalimika na matatizo na magonjwa, akiwa na amani ndani ya nafsi yake na watu wake na familia yake na barabara zake, na akiwa hana hofu, na akiwa na chakula cha halali cha kumtosha kwa siku yake; basi ni kana kwamba kakabidhiwa dunia yote nzima.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa haja ya mtu kuwa na afya na amani na nguvu.
  2. Ni wajibu kwa mja amhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu na amshukuru kwa neema hizi.
  3. Himizo la kuridhika na kuipa nyongo dunia.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 167) (2346). سنن ابن ماجه (5/ 253) (4141). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 570). التنوير شرح الجامع الصغير، لمحمد الصنعاني (10/ 110).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema

عَنْ ‌الزُّبَيْرِ بْنِ الْعَوَّامِ قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ: {ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ} [التكاثر: 8]، قَالَ الزُّبَيْرُ: يَا رَسُولَ اللهِ، وَأَيُّ النَّعِيمِ نُسْأَلُ عَنْهُ، وَإِنَّمَا هُمَا الْأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالْمَاءُ؟ قَالَ: «أَمَا إِنَّهُ سَيَكُونُ».
Kutoka kwa Zubairi bin Awwam amesema: Ilipoteremka: "Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema" [Takathur: 8], akasema Zubairi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazooulizwa juu yake, au ni hivi vyeusi viwili tende na maji (Vyakula na vinywaji kwa ujumla)? Akasema: "Hakika bila shaka zitakuwa hizo".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ilipoteremka aya: "Kisha hakika bila shaka mtaulizwa siku hiyo kuhusu neema" Yaani: Mtakuja kuulizwa kuhusu kutekeleza shukurani kwa yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu juu yenu miongoni mwa neema, akasema Zubairi bin Awwam radhi za Allah ziwe juu yake: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazoulizwa juu yake?! Ni neema mbili ambazo hazihitaji kuziomba ambazo ni tende na maji!. Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ama hakika nyinyi mtaulizwa kuhusu neema pamoja hali hii iliyo nayo, ni hizi neema mbili kubwa katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mafunzo
  1. Msisitizo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema.
  2. Neema ni miongoni mwa vile ambavyo mja ataulizwa kwavyo siku ya Kiyama.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 375) (3356)، سنن ابن ماجه (5/ 262) (4158)، شرح سنن ابن ماجه للسيوطي (ص: 307)، تحفة الأحوذي (9/203)، مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (25/ 251).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuwahi kula Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake milo miwili kwa siku isipokuwa mlo mmoja utakuwa ni tende

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا أَكَلَ آلُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَكْلَتَيْنِ فِي يَوْمٍ إِلَّا إِحْدَاهُمَا تَمْرٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kula Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake milo miwili kwa siku isipokuwa mlo mmoja utakuwa ni tende.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kwamba watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kula milo miwili kwa siku moja isipokuwa mlo mmoja kati ya hiyo utakuwa ni tende.

Mafunzo
  1. Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na watu wa nyumba yake, huenda kuna wakati hawakupata mlo zaidi ya mmoja.
  2. Tende ilikuwa rahisi kwao kuliko chochote.
  3. Ubora wa kuipa nyongo dunia na kutosheka na kichache katika maisha, na kuwa hilo ni katika tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana wa Mitume.
  4. Kula milo miwili kwa siku ni katika mambo halali na yanayofaa, nayo ni katika desturi za Waarabu inafahamika, walikuwa wakila kwa siku milo miwili, chakula cha mchana, na chakula cha usiku.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 97) (6455). صحيح مسلم (4/ 2282) (2971). فتح الباري لابن حجر (11/ 292).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُنْذُ قَدِمَ المَدِينَةَ مِنْ طَعَامِ البُرِّ ثَلاَثَ لَيَالٍ تِبَاعًا، حَتَّى قُبِضَ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kushiba tangu walipoingia Madina kwa chakula cha ngano kwa muda wa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki rehema na amani ziwe juu yake.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya maisha ya chini, kwani maisha halisi ni maisha ya Akhera.
  2. Amesema bin Hajari: Na kinachoonekana nikuwa sababu ya kutoshiba kwao mara nyingi ilikuwa ni kwa sababu ya uchache wa upatikanaji wa chochote kwao, yaani walikuwa wakipata chakula lakini walikuwa wakithamini wenye shida zaidi yao kuliko nafsi zao.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 75) (5416). صحيح مسلم (4/ 2282) (2970). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (7/ 129). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (45/ 129).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka

عَنْ عَمْرِو بْنِ الحَارِثِ خَتَنِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخِي أُمِّ المؤمِنين جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ الحَارِثِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُم، قَالَ: مَا تَرَكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا وَلاَ دِينَارًا وَلاَ عَبْدًا وَلاَ أَمَةً وَلاَ شَيْئًا، إِلَّا بَغْلَتَهُ البَيْضَاءَ، وَسِلاَحَهُ، وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً.
Kutoka kwa Amri bin Harithi shemeji yake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kaka yake na mama wa waumini Juwairia binti Harithi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, amesema: Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha Dirham ya fedha wala Dinari ya dhahabu, wala mtumwa mmilikiwa wala kijakazi mmilikiwa, wala mbuzi wala ngamia wala chochote katika mali, isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akimpanda, na silaha yake aliyokuwa akiibeba, na kipande cha Ardhi alichokitoa wakfu kwa ajili ya wasafiri.

Mafunzo
  1. Manabii hawarithiwi.
  2. Kumebainishwa alivyoviacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baada ya kifo chake.
  3. Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha kitu chochote cha msingi, kutokana na ukarimu wake na utoaji wake na wema wake.
  4. Amesema Al-Karmani: Dhamiri katika kauli yake "na akavifanya" hii inarudi katika vitu vitatu: Yaani; nyumbu na silaha na Ardhi na si katika Ardhi peke yake.
  5. Shemeji: Ni kaka wa dada, na neno "Akhtani" hutumika kwa ndugu wa mwanamke.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 2) (2739). النهاية في غريب الحديث والأثر (254). فتح الباري لابن حجر (5/ 360). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (14/ 31).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com