Hakim bin Hizam alimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake mahitaji ya kidunia akampatia, kisha akamuomba mara nyingine akampatia, kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ewe Hakim, hakika mali hii huvutia na hupendwa sana, atakayeipata bila kuomba na akaichukua pasina kujikweza na pupa, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa pupa na tamaa ya nafsi basi hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa kama yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu wenye kutoa ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini unaoomba, anasema Hakim: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, namuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitopunguza mali ya yeyote kwa kumuomba chochote baada yako mpaka niondoke duniani. Basi akawa khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu Abubakari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akimuita Hakim ili ampatie sadaka, anakataa kupokea chochote, kisha kiongozi wa Waumini Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alimuita ili ampatie mali, akakataa kuchukua, basi Omari akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi nimemletea haki yake aliyomgawia Mwenyezi Mungu kutoka katika mali ya Ngawira waliyoipata Waislamu kutoka kwa Makafiri pasina vita wala mapigano, akakataa kuichukua, Hakim hakupunguza mali ya yeyote kwa kumuomba baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.
- Kuchukua mali na kuikusanya kwa njia za kisheria hakupingani na kuiepuka dunia; kwa sababu kuipa mgongo dunia ni ukwasi wa nafsi na moyo kutofungamana na mali.
- Kumebainishwa ukubwa wa ukarimu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba alikuwa akitoa utoaji wa mtu asiyeogopa umasikini kamwe!
- Kutoa nasaha na kupupia katika kuwanufaisha ndugu, wakati wa kutoa msaada; kwa sababu wakati huo nafsi huwa imejiandaa kupokea maneno mazuri.
- Kujizuia kuwaomba watu, na kuchukia kufanya hivyo, hasa hasa panapokuwa hakuna haja.
- Hapa kuna ubaya wa kupupia mali na kuombaomba sana.
- Muombaji atakapolazimisha kuomba, hakuna tatizo kumnyima na kumfelisha, na kumpa nasaha, na kumuamrisha kujizuia kuomba, na kuacha pupa ya kutaka kuchukua.
- Hastahiki yeyote kuchukua chochote kutoka katika Hazina ya mali za Waislamu isipokuwa baada ya kupepwa na kiongozi, na ama kabla kuwagawanywa kwa ngawira, hastahiki pia kufanya hivyo.
- Inafaa kuomba kukiwa na haja.
- Amesema bin Hajari: Ndani ya kisa hiki nikuwa, inatakiwa kwa kiongozi kutombainishia muombaji madhara yaliyoko katika uombaji isipokuwa baada ya kukidhi haja yake ili mawaidha yake yafike mahala pake, ili asifikirie kuwa huenda hiyo ndio sababu ya kumnyima shida yake.
- Ubora wa Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na kushikamana kwake na ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake.
- Amesema Is-haka bin Rahawaihi: Alifariki Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ulipofikia wakati wa kufa, na hakika alikuwa amekwisha kuwa tajiri mwenye mali nyingi kuliko Makuraishi wote.
صحيح البخاري (4/ 5) (2750). صحيح مسلم (2/ 717) (1035). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (8/ 13). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 584). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (1/ 459). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 386). منار القاري، لحمزة قاسم (3/ 45). المنهاج شرح صحيح مسلم، للنووي (7/ 126). إكمال المعلم بفوائد مسلم، للقاضي عياض (3/ 566).