Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Muongozo wake Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika Ndoa na kuamiliana na wake zake.

Hadithi 3

Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: حَفِظْتُ مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشْرَ رَكَعَاتٍ: رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ المَغْرِبِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ العِشَاءِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَكَانَتْ سَاعَةً لاَ يُدْخَلُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيهَا، حَدَّثَتْنِي حَفْصَةُ أَنَّهُ كَانَ إِذَا أَذَّنَ المُؤَذِّنُ وَطَلَعَ الفَجْرُ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ، وَفِي لَفْظٍ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُصَلِّي بَعْدَ الْجُمُعَةِ رَكْعَتَيْنِ.
Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema : Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zoteDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Abdullahi bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake: Yakuwa miongoni mwa swala za sunna alizozihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni rakaa kumi na huitwa kuwa ni sunna zilizopangiliwa, Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, Na kabla ya Alfajiri rakaa mbili, Zikatimia rakaa kumi. Na ama swala ya Ijumaa aliswali baada yake rakaa mbili.

Mafunzo
  1. Imendezeshwa kuswali rakaa hizi zilizopangiliwa, na kudumu nazo.
  2. Sheria ya kuswali sunna nyumbani.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 58-59) (1180، 1181). صحيح مسلم (2/ 601) (882). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص112).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

“Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.”

عَنْ زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْها أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَيْهَا فَزِعًا يَقُولُ: «لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ اليَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مِثْلُ هَذِهِ» وَحَلَّقَ بِإِصْبَعِهِ الإِبْهَامِ وَالَّتِي تَلِيهَا، قَالَتْ زَيْنَبُ بِنْتُ جَحْشٍ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ: أَنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ قَالَ: «نَعَمْ إِذَا كَثُرَ الخَبَثُ».
Kutoka kwa Zainab bint Jahshi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia ndani kwake akiwa na mfadhaiko huku akisema: “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Zainab bint Jahshi Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akiwa na mfadhaiko na khofu kubwa, akasema: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, akiashiria kutaraji jambo baya litatokea, na hakuna kusalimika katika hilo ila kwa kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: Ole wao Waarabu kutokana na shari inayokaribia kutokea, leo imefunguliwa katika ngome ya Ya'ajuj na Ma'ajuj kiasi hiki, ambacho ni ukuta alioujenga Dhul-Qarnain, na akazungusha duara kwa kidole gumba chake na kile kinachofuata (kuonyesha kiasi kilicho funguliwa). Akasema Zainab Mwenyezi Mungu amuwie radhi: Vipi Mwenyezi Mungu atuangamize na hali wapo waumini wema miongoni mwetu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: “Maovu yatakapokithiri, kama vile uovu, ufisadi, maasi, uzinzi, pombe na vitu vingine, maangamizo yatawakumba wote.

Mafunzo
  1. Hofu haiushughulishi moyo wa muumini kiasi cha kuacha kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa hofu, kwa sababu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu mioyo hupata utulivu.
  2. Himizo la kukemea maasi na kuzuia kutokea kwake.
  3. Maangamizo ya watu wote hutokea kwa sababu ya kukithiri kwa maasi na kuenea kwake, na kutoyakemea hata kama watu wema ni wengi.
  4. Majanga huwakumba watu wote, wema na waovu, lakini wao watafufuliwa kulingana na nia zao.
  5. "Amewataja Waarabu katika kauli yake: "Ole wao Waarabu kwa shari iliyokaribia"; kwa sababu wao ndio walioingia katika Uislamu kwa wingi wakati akisema hivyo.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 138) (3346). صحيح مسلم (4/ 2208) (2880). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 280). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 54). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 437). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 212).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤمنينَ رضي الله عنها قَالَتْ: كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَالنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ إِنَاءٍ وَاحِدٍ كِلاَنَا جُنُبٌ، وَكَانَ يَأْمُرُنِي، فَأَتَّزِرُ، فَيُبَاشِرُنِي وَأَنَا حَائِضٌ، وَكَانَ يُخْرِجُ رَأْسَهُ إِلَيَّ وَهُوَ مُعْتَكِفٌ فَأَغْسِلُهُ وَأَنَا حَائِضٌ.
Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi, na alikuwa akitoa kichwa chake kwangu, naye akiwa katika itikafu (msikitini), ninamuosha nami nikiwa katika hedhi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu baadhi ya hali zake maalum pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwake: Nikuwa alikuwa akioga kutokana na janaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja wakichota wote kwa pamoja. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumwendea akiwa katika hedhi anamuamrisha afunike mwili wake kuanzia kitovuni mpaka magotini, kisha akimshikashika bila ya tendo la ndoa. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu msikitini anatoa kichwa chake kwa Aisha anamuosha naye akiwa nyumbani kwake na akiwa katika siku zake.

Mafunzo
  1. Inafaa mtu kuoga na mke wake katika chombo kimoja.
  2. Inafaa kumpapasa mwenye hedhi, mahali pasipokuwa tupu, nakuwa mwili wake ni twahara na wala si najisi.
  3. Inapendeza kwa mwanamke kuvaa kikoi (au mtandio) wakati wa kupapaswa.
  4. Kuchukua sababu zinazozuia kuingia katika haramu.
  5. Katazo kwa mwenye hedhi kukaa msikitini.
  6. Uhalali kwake wa kuvipapasa vitu vibichi au vikavu, ikiwemo kuziosha nywele na kuzitana
  7. Muamala mzuri wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa familia yake.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 67) (299 - 301). صحيح مسلم (1/ 244) (297)، (1/ 255) (319). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 66). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص79). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 76).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com