Aliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Zainab bint Jahshi Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akiwa na mfadhaiko na khofu kubwa, akasema: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, akiashiria kutaraji jambo baya litatokea, na hakuna kusalimika katika hilo ila kwa kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: Ole wao Waarabu kutokana na shari inayokaribia kutokea, leo imefunguliwa katika ngome ya Ya'ajuj na Ma'ajuj kiasi hiki, ambacho ni ukuta alioujenga Dhul-Qarnain, na akazungusha duara kwa kidole gumba chake na kile kinachofuata (kuonyesha kiasi kilicho funguliwa). Akasema Zainab Mwenyezi Mungu amuwie radhi: Vipi Mwenyezi Mungu atuangamize na hali wapo waumini wema miongoni mwetu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: “Maovu yatakapokithiri, kama vile uovu, ufisadi, maasi, uzinzi, pombe na vitu vingine, maangamizo yatawakumba wote.
- Hofu haiushughulishi moyo wa muumini kiasi cha kuacha kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa hofu, kwa sababu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu mioyo hupata utulivu.
- Himizo la kukemea maasi na kuzuia kutokea kwake.
- Maangamizo ya watu wote hutokea kwa sababu ya kukithiri kwa maasi na kuenea kwake, na kutoyakemea hata kama watu wema ni wengi.
- Majanga huwakumba watu wote, wema na waovu, lakini wao watafufuliwa kulingana na nia zao.
- "Amewataja Waarabu katika kauli yake: "Ole wao Waarabu kwa shari iliyokaribia"; kwa sababu wao ndio walioingia katika Uislamu kwa wingi wakati akisema hivyo.
صحيح البخاري (4/ 138) (3346). صحيح مسلم (4/ 2208) (2880). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 280). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 54). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 437). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 212).