Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Alama za Kiama .

Hadithi 5

Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto,

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلاَ أُحَدِّثُكُمْ حَدِيثًا عَنِ الدَّجَّالِ، مَا حَدَّثَ بِهِ نَبِيٌّ قَوْمَهُ؟ إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّهُ يَجِيءُ مَعَهُ بِمِثَالِ الجَنَّةِ وَالنَّارِ، فَالَّتِي يَقُولُ إِنَّهَا الجَنَّةُ هِيَ النَّارُ، وَإِنِّي أُنْذِرُكُمْ كَمَا أَنْذَرَ بِهِ نُوحٌ قَوْمَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto, na hakika mimi ninakutahadharisheni kama alivyo watahadharisha Nabii Nuhu watu wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anawaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake kuhusu Dajali, sifa zake, na dalili zake, kwa mambo ambayo hakuna Nabii yeyote aliyetangulia kuyasimulia kabla yake, miongoni mwa hayo ni: Chongo wa jicho. Na Mwenyezi Mungu kampa kitu mfano wa Pepo na Moto, kulingana na mtazamo wa macho. Bali Pepo yake ni Moto na Moto wake ni Pepo, mwenye kumtii atamuingiza katika Pepo hii kama watu wanavyoiona, lakini uhalisia wake ni Moto wenye kuunguza, na atakayemuasi atamuingiza Motoni kama watu wanavyouona, lakini kwa uhalisia ni Pepo nzuri. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akatuonya dhidi ya fitina yake kama vile Nuhu alivyowaonya watu wake kuhusu hilo.

Mafunzo
  1. Ukubwa wa fitina ya Dajali.
  2. Kuokoka kutokana na fitina ya Dajali kupo katika imani ya kweli, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutafuta hifadhi kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake katika tashahudi ya mwisho, na kuhifadhi aya kumi za mwanzo wa Suratul-Kahf.
  3. Pupa kubwa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa umma wake, alipowawekea wazi Waislamu sifa za Dajali ambazo hakuna mtume kabla yake aliyewahi kuzieleza.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 134) (3338). صحيح مسلم (4/ 2250) (2936).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

“Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.”

عَنْ زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْها أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَيْهَا فَزِعًا يَقُولُ: «لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ اليَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مِثْلُ هَذِهِ» وَحَلَّقَ بِإِصْبَعِهِ الإِبْهَامِ وَالَّتِي تَلِيهَا، قَالَتْ زَيْنَبُ بِنْتُ جَحْشٍ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ: أَنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ قَالَ: «نَعَمْ إِذَا كَثُرَ الخَبَثُ».
Kutoka kwa Zainab bint Jahshi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia ndani kwake akiwa na mfadhaiko huku akisema: “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Zainab bint Jahshi Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akiwa na mfadhaiko na khofu kubwa, akasema: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, akiashiria kutaraji jambo baya litatokea, na hakuna kusalimika katika hilo ila kwa kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: Ole wao Waarabu kutokana na shari inayokaribia kutokea, leo imefunguliwa katika ngome ya Ya'ajuj na Ma'ajuj kiasi hiki, ambacho ni ukuta alioujenga Dhul-Qarnain, na akazungusha duara kwa kidole gumba chake na kile kinachofuata (kuonyesha kiasi kilicho funguliwa). Akasema Zainab Mwenyezi Mungu amuwie radhi: Vipi Mwenyezi Mungu atuangamize na hali wapo waumini wema miongoni mwetu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: “Maovu yatakapokithiri, kama vile uovu, ufisadi, maasi, uzinzi, pombe na vitu vingine, maangamizo yatawakumba wote.

Mafunzo
  1. Hofu haiushughulishi moyo wa muumini kiasi cha kuacha kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa hofu, kwa sababu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu mioyo hupata utulivu.
  2. Himizo la kukemea maasi na kuzuia kutokea kwake.
  3. Maangamizo ya watu wote hutokea kwa sababu ya kukithiri kwa maasi na kuenea kwake, na kutoyakemea hata kama watu wema ni wengi.
  4. Majanga huwakumba watu wote, wema na waovu, lakini wao watafufuliwa kulingana na nia zao.
  5. "Amewataja Waarabu katika kauli yake: "Ole wao Waarabu kwa shari iliyokaribia"; kwa sababu wao ndio walioingia katika Uislamu kwa wingi wakati akisema hivyo.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 138) (3346). صحيح مسلم (4/ 2208) (2880). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 280). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 54). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 437). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 212).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika katika watu waovu zaidi ni wale watakaokutwa na Kiyama wakiwa hai, na mwenye kuyafanya makaburi kuwa mahala pa kusalia

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بن مسعودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ مِنْ شِرَارِ النَّاسِ مَنْ تُدْرِكُهُ السَّاعَةُ وَهُمْ أَحْيَاءٌ، وَمَنْ يَتَّخِذُ الْقُبُورَ مَسَاجِدَ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika katika watu waovu zaidi ni wale watakaokutwa na Kiyama wakiwa hai, na mwenye kuyafanya makaburi kuwa mahala pa kusalia".
Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu watu waovu, nakuwa hao ndio Kiyama kitasimama juu yao, na wale wanaoyafanya makaburi kuwa misikiti, wakisali hapo na wakiyaelekea wakati wa ibada.

Mafunzo
  1. Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi; kwa sababu kitendo hicho ni njia ya kuingia katika shirki.
  2. Uharamu wa kusali katika makaburi hata bila kujengea; kwa sababu msikiti ni jina la kila mahali panaposujudiwa hapo hata kama hakuna jengo.
  3. Atakayeyafanya makaburi ya watu wema kuwa mahala pa kusalia huyo ni katika viumbe waovu, hata kama atadai kuwa lengo lake ni kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

مسند أحمد (6/ 394) (3844). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص191). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص176). أحكام الجنائز، للألباني (1/ 217).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf

عن أبي الدرداء رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ حَفِظَ عَشْرَ آيَاتٍ مِنْ أَوَّلِ سُورَةِ الكَهْفِ، عُصِمَ مِنَ الدَّجَّالِ». وفي رواية: «مِنْ آخِرِ سُورَةِ الكَهْف».
Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayehifadhi aya kumi kwa moyo wake za mwanzo wa suratul Kahaf atakingwa na kuepushwa na kuhifadhiwa na fitina za Masihi Dajali atakayetoka zama za mwisho na atadai uungu, na fitina zake ni fitina kubwa itakayotokea katika Ardhi tangu kuumbwa kwa Adam mpaka kusimama kwa Kiyama; kwa yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo ya ajabu ambayo atawafitinisha kwayo watakaomfuata, na hii ni kwa sababu mwanzo wa suratul Kahaf kuna maajabu na miujiza mikubwa kuliko fitina na za Dajali kwa watu, atakayezizingatia hatofitinika na Dajali. Na katika riwaya nyingine: Ni aya kumi za mwisho wa sura kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Hivi wanadhani wale waliokufuru kuwa wanaweza kujifanyia..."

Mafunzo
  1. Kumebainishwa fadhila ya suratul Kahaf, na kuwa mwanzo wake na mwisho wake zinakinga na fitina za Dajali.
  2. Kumeelezwa swala la Dajali, na kumebainishwa yanayokinga na fitina hiyo.
  3. Himizo la kuihifadhi suratul Kahaf nzima, ikiwa atashindwa basi ahifadhi aya kumi za mwanzo na za mwisho.
  4. Amesema Al-Qurtubi katika sababu ya hilo: Imesemekana: Kwa sababu ya yale yaliyoko ndani ya kisa cha watu wa pangoni katika maajabu na miujiza, atakayeizingatia hatoshangazwa na jambo la Dajali na halitamtisha hilo na wala hatofitinika, na imesemekana: Kwa sababu ya kauli yake Mtukufu: "Ili kitoe onyo kali kutoka kwake" Kwa kuuhusisha ugumu na ukali na kwake, na ndio unafaa kwa yale atakayokuwa nayo Dajali katika kudai uungu na kutawala kwake na ukubwa wa fitina yake, inakuwa maana ya hadithi nikuwa: atakayesoma aya hizi na akazizingatia na akasimama katika maana zake zitamtahadharisha na atasalimika naye.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 555) (809). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 243). شرح النووي على مسلم (6/ 92). فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (6/ 119). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (13/ 115). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لملا القاري (4/ 1465). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن (2/ 760).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii

عن تَميم الداري رضي الله عنه، قال: سمعتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «‌لَيَبْلُغَنَّ ‌هَذَا الأَمْرُ مَا بَلَغَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ، وَلَا يَتْرُكُ اللهُ بَيْتَ مَدَرٍ وَلَا وَبَرٍ إِلَّا أَدْخَلَهُ اللهُ هَذَا الدِّينَ، بِعِزِّ عَزِيزٍ أَوْ بِذُلِّ ذَلِيلٍ، عِزًّا يُعِزُّ اللهُ بِهِ الإِسْلَامَ، وَذُلًّا يُذِلُّ اللهُ بِهِ الكُفْرَ» وَكَانَ تَمِيمٌ الدَّارِيُّ يَقُولُ: قَدْ عَرَفْتُ ذَلِكَ فِي أَهْلِ بَيْتِي، لَقَدْ أَصَابَ مَنْ أَسْلَمَ مِنْهُمُ الْخَيْرُ وَالشَّرَفُ وَالْعِزُّ، وَلَقَدْ أَصَابَ مَنْ كَانَ مِنْهُمْ كَافِرًا الذُّلُّ وَالصَّغَارُ وَالْجِزْيَةُ.
Imepokelewa kutoka kwa Tamim Ad-Dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Litafikia jambo hili ulipofika usiku na mchana, na wala hatoacha Mwenyezi Mungu nyumba ya mjini wala ya kijijini isipokuwa ataiingiza Mwenyezi Mungu dini hii, kwa utukufu wa yeyote au kwa udhalili wa yeyote, ni utukufu anaoutukuza Mwenyezi Mungu uislamu, na ni udhalili anaoudhalilisha Mwenyezi Mungu ukafiri" na alikuwa Tamimu Dari akisema, nililijua hilo kwa watu wa familia yangu, kwa hakika alipata aliyesilimu miongoni mwao kheri na heshima na utukufu, na aliyekuwa kafiri alipata udhalili na unyonge na ulipaji kodi.
Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani zimshukie, amesema kuwa dini hii itaenea sehemu zote za ardhi, hivyo dini hii itafika sehemu yoyote ile ufikapo usiku na mchana, na hatoiwaacha Mwenyezi Mungu Mtukufu nyumba yoyote mijini na vijijini wala mabondeni na majangwani isipokuwa ataiingiza dini hii, atakayeikubali dini hii na akaiamini basi atakuwa mtukufu kwa sababu ya utukufu wa Uislamu, na atakayeikataa na akaipinga basi atakuwa dhalili mwenye kufedheheshwa. Kisha swahaba Tamim Al-Dari, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akaeleza kuwa alilijua hilo aliloambiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake kwa watu nyumba yake hasa, kwani kila aliyesilimu miongoni mwao alipata kheri na heshima, na utukufu, na aliyekufuru miongoni mwao alipata udhalili na unyonge, hii ikiwa ni pamoja na pesa anazowalipa Waislamu kama Jizia (Kodi).

Mafunzo
  1. Habari njema kwa waislamu kuwa dini yao itasambaa katika pande zote za Ardhi.
  2. Utukufu ni kwa Uislamu na waislamu na udhalili ni kwa makafiri na ukafiri.
  3. Kuna dalili miongoni mwa dalili za utume na alama miongoni mwa alama zake, kiasi kwamba jambo hilo limetokea kama alivyoeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Marejeo

مسند أحمد (28/ 154) (16957). النهاية في غريب الحديث والأثر، لابن الأثير (4/ 309). المصباح المنير في غريب الشرح الكبير، لأحمد الفيومي (1/ 163). الموسوعة الفقهية الكويتية، (15/ 163).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com