Ameeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu baadhi ya hali zake maalum pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwake: Nikuwa alikuwa akioga kutokana na janaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja wakichota wote kwa pamoja. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumwendea akiwa katika hedhi anamuamrisha afunike mwili wake kuanzia kitovuni mpaka magotini, kisha akimshikashika bila ya tendo la ndoa. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu msikitini anatoa kichwa chake kwa Aisha anamuosha naye akiwa nyumbani kwake na akiwa katika siku zake.
- Inafaa mtu kuoga na mke wake katika chombo kimoja.
- Inafaa kumpapasa mwenye hedhi, mahali pasipokuwa tupu, nakuwa mwili wake ni twahara na wala si najisi.
- Inapendeza kwa mwanamke kuvaa kikoi (au mtandio) wakati wa kupapaswa.
- Kuchukua sababu zinazozuia kuingia katika haramu.
- Katazo kwa mwenye hedhi kukaa msikitini.
- Uhalali kwake wa kuvipapasa vitu vibichi au vikavu, ikiwemo kuziosha nywele na kuzitana
- Muamala mzuri wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa familia yake.
صحيح البخاري (1/ 67) (299 - 301). صحيح مسلم (1/ 244) (297)، (1/ 255) (319). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 66). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص79). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 76).