Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri

عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى الفَجْرَ جَلَسَ فِي مُصَلَّاهُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ حَسَنًا، وَقَالَ: كَانَ لَا يَقُومُ مِنْ مُصَلَّاهُ الَّذِي يُصَلِّي فِيهِ الصُّبْحَ أَوِ الغَدَاةَ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ، فَإِذَا طَلَعَتِ الشَّمْسُ قَامَ، وَكَانُوا يَتَحَدَّثُونَ فَيَأْخُذُونَ فِي أَمْرِ الجَاهِلِيَّةِ، فَيَضْحَكُونَ وَيَتَبَسَّمُ.
Kutoka kwa Jabiri bin Samura radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri, na akasema: Alikuwa hanyanyuki kutoka katika mswala wake alioswalia hapo Alfajiri au asubuhi, mpaka linapochomoza Jua, basi linapochomoza Jua anasimama, na walikuwa wakizungumza wanajikuta wameingia katika mazungumzo ya zama za ujinga, wanacheka na yeye anatabasamu.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Na miongoni mwa sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza kwa kunyanyuka, na alikuwa hasimami kutoka katika mswala wake aliouswalia Alfajiri, mpaka Jua lichomoze. Jua linapochomoza anasimama, na walikuwa wakizungumza wanachukua katika baadhi ya mambo yao ya kabla ya Uislamu na huku yeye kanyamaza, wanacheka, na huenda yeye akatabasamu pamoja nao.

Mafunzo
  1. Sunna ya kufanya dhikiri asubuhi mpaka Jua lichomoze, na kubaki katika kikao chake anapokuwa hana udhuru.
  2. Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa tabia njema na upole, kiasi kwamba alikuwa akikaa na Maswahaba zake, na akisikiliza mazungumzo yao na simulizi zao, na anatabasamu kwa sababu yake.
  3. Inafaa kufanya mazungumzo na kukumbushia enzi za ujinga msikitini.
  4. Inafaa kucheka na kutabasamu; kwa sababu kilichokatazwa ni kukithirisha kucheka.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 464) (670). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (14/ 407). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 296).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Mambo ya Mtume.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com