Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kucheka kwake Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:

Hadithi 1

Sikumuona Mtume -rehema amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُسْتَجْمِعًا قَطُّ ضَاحِكًا، حَتَّى أَرَى مِنْهُ لَهَوَاتِهِ، إِنَّمَا كَانَ يَتَبَسَّمُ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Sikumuona Mtume -rehema amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema amani ziwe juu yake alikuwa hapitilizi kucheka mpaka kionekane kilimi chake, nacho ni kinyama kinachoning'inia juu ya koo, bali alikuwa akitabasam.

Mafunzo
  1. Kulikuwa kucheka kwa Mtume rehema amani ziwe juu yake ni kutabasam anaporidhia au kufurahishwa na jambo.
  2. Amesema bin Hajari: Sikuwahi kumuona akipitiliza katika kucheka kiasi cha kucheka kicheko kamili kwa kujiachia mzima mzima kwa kicheko.
  3. Kukithirisha kucheka na kunyanyua sauti kwa kujikohoza hii si miongoni mwa sifa za watu wema.
  4. Kukithirisha kucheka kunaondoa haiba ya mtu na heshima yake mbele ya ndugu zake.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 24) (6092). صحيح مسلم (2/ 616) (899).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com