Hakuwahi kupewa hiyari Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya mambo mawili hata siku moja isipokuwa atachukua jepesi lake, madamu si dhambi, ikiwa itakuwa ni dhambi, basi hujiwekanalo mbali kuliko watu wote
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake baadhi ya tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwa zile alizozieleza: Nikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwahi kupewa hiyari baina ya mambo mawili isipokuwa alichukua jepesi zaidi kati ya hayo, madamu hilo jepesi halipelekei katika madhambi, basi alikuwa akijiweka mbali zaidi kuliko watu wote, na hapo anachagua gumu zaidi. Hakuwahi kulipiza kisasi rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya nafsi yake binafsi, bali alikuwa akisamehe na kufuta katika haki yake isipokuwa yakivunjwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu hapo analipiza kisasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na alikuwa ni mtu mwenye hasira kuliko watu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
- Sunna ya kuchukua jepesi katika mambo madamu hakuna maasi ndani yake.
- Wepesi wa Uislamu.
- Sheria ya kukasirika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika upole na subira na kutekeleza haki katika kusimamisha sheria na mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Amesema bin Hajari: Na hapa kuna kuacha kuchukua jambo gumu, na kutosheka na jepesi, na kuacha kung'ang'ania katika yale yasiyokuwa ya dharura.
- Himizo la kusamehe isipokuwa katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
صحيح البخاري (4/ 189) (3560). صحيح مسلم (4/ 1813) (2327). فتح الباري لابن حجر (575/6). شرح صحيح مسلم (83/15). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (601/9). شرح رياض الصالحين لابن عثيمين (587/3).