Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Usamehevu wake Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:

Hadithi 1

Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa

عَن أَبي عَبْدِ اللهِ الْجَدَلِيِّ قَالَ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها عَنْ خُلُقِ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَتْ: لَمْ يَكُنْ فَاحِشًا وَلَا مُتَفَحِّشًا وَلَا صَخَّابًا فِي الْأَسْوَاقِ، وَلَا يَجْزِي بِالسَّيِّئَةِ السَّيِّئَةَ وَلَكِنْ يَعْفُو وَيَصْفَحُ.
Kutoka kwa Abuu Abdillah Al-Jadali amesema: Nilimuuliza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na maneno machafu wala mwenye kujilazimisha machafu, wala hakuwa na makelele masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya, lakini alikuwa akisamehe na kufuta kosa.
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Aliulizwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Haikuwa katika tabia zake uchafu na ubaya wa kauli na vitendo, na wala hakuwa akijilazimisha machafu wala kuyakusudia, wala hakuwa mpiga kelele kwa kunyanyua sauti yake masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya; lakini alikuwa akilipa ubaya kwa wema, na akisamehe ndani ya moyo, na akifuta kosa na kulipuuza katika dhahiri.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa tabia alizokuwa nazo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, tabia za juu na kuwa kwake mbali na tabia mbaya.
  2. Himizo la kufanya tabia njema na kujiweka mbali na tabia mbaya.
  3. Kumekemewa kujilazimisha machafu katika kauli na maneno machafu.
  4. Kumekemewa kunyanyua sauti juu ya watu na kuwapigia makelele.
  5. Himizo la kuukabili ubaya kwa wema, na kusamehe na kufuta kosa.
Marejeo

سنن الترمذي (3/ 543) (2016). مسند أحمد (42/ 256) (25417). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن حجر(6/ 575). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، القسطلاني (9/ 30). معجم اللغة العربية المعاصرة (2/ 1629). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (9/ 3717).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com