Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Huruma yake Mtume Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:

Hadithi 3

Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto,

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَلاَ أُحَدِّثُكُمْ حَدِيثًا عَنِ الدَّجَّالِ، مَا حَدَّثَ بِهِ نَبِيٌّ قَوْمَهُ؟ إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّهُ يَجِيءُ مَعَهُ بِمِثَالِ الجَنَّةِ وَالنَّارِ، فَالَّتِي يَقُولُ إِنَّهَا الجَنَّةُ هِيَ النَّارُ، وَإِنِّي أُنْذِرُكُمْ كَمَا أَنْذَرَ بِهِ نُوحٌ قَوْمَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto, na hakika mimi ninakutahadharisheni kama alivyo watahadharisha Nabii Nuhu watu wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anawaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake kuhusu Dajali, sifa zake, na dalili zake, kwa mambo ambayo hakuna Nabii yeyote aliyetangulia kuyasimulia kabla yake, miongoni mwa hayo ni: Chongo wa jicho. Na Mwenyezi Mungu kampa kitu mfano wa Pepo na Moto, kulingana na mtazamo wa macho. Bali Pepo yake ni Moto na Moto wake ni Pepo, mwenye kumtii atamuingiza katika Pepo hii kama watu wanavyoiona, lakini uhalisia wake ni Moto wenye kuunguza, na atakayemuasi atamuingiza Motoni kama watu wanavyouona, lakini kwa uhalisia ni Pepo nzuri. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akatuonya dhidi ya fitina yake kama vile Nuhu alivyowaonya watu wake kuhusu hilo.

Mafunzo
  1. Ukubwa wa fitina ya Dajali.
  2. Kuokoka kutokana na fitina ya Dajali kupo katika imani ya kweli, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutafuta hifadhi kwa Mwenyezi Mungu dhidi yake katika tashahudi ya mwisho, na kuhifadhi aya kumi za mwanzo wa Suratul-Kahf.
  3. Pupa kubwa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa umma wake, alipowawekea wazi Waislamu sifa za Dajali ambazo hakuna mtume kabla yake aliyewahi kuzieleza.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 134) (3338). صحيح مسلم (4/ 2250) (2936).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha)

عَنْ مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ أَخْوَفَ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمُ الشِّرْكُ الْأَصْغَرُ» قَالُوا: وَمَا الشِّرْكُ الْأَصْغَرُ يَا رَسُولَ اللهِ؟ قَالَ: «الرِّيَاءُ، يَقُولُ اللهُ عز وجل لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِذَا جُزِيَ النَّاسُ بِأَعْمَالِهِمْ: اذْهَبُوا إِلَى الَّذِينَ كُنْتُمْ تُرَاؤُونَ فِي الدُّنْيَا، فَانْظُرُوا هَلْ تَجِدُونَ عِنْدَهُمْ جَزَاءً؟».
Imepokelewa kutoka kwa Mahmud bin Labid -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha), atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama kuwaambia, pindi watu wote watakapolipwa kwa matendo yao: 'Nendeni kwa wale mliokuwa mkijionyesha kwao duniani, mtazame je mtapata kwao malipo?".
Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa jambo kubwa zaidi analoliogopea juu ya umma wake: Ni shirki ndogo nayo; ni mtu kufanya kwa ajili ya watu. Kisha akaeleza kuhusu adhabu ya wenye kujionyesha siku ya Kiyama kwa kuambiwa: Nendeni kwa wale mliokuwa mkifanya kwa ajili yao, mkatazame je wanamiliki malipo na thawabu za kukupeni kwa amali hiyo?!.

Mafunzo
  1. Ulazima wa kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutahadhari na riyaa.
  2. Huruma yake kubwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya umma wake na pupa yake ya kutaka kuwaongoza na kuwapa kwake nasaha.
  3. Ikiwa hii ndio hofu yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akizungumza na Masahaba ambao ndio watukufu kwa watu wema, basi hofu kwa wale wataokuja baada yao ni kubwa zaidi.
Marejeo

مسند أحمد (39/ 39) (23630). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص57). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص45).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya ishaa, akatoka Omar, akasema: Swala Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamelala wanawake na watoto, akatoka na kichwa chake kikitona maji akisema: Lau kama nisingehofia kuwapa tabu umma wangu basi ningewaamrisha swala hii waiswali wakati huu

عن عَبْد اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قال: «أّعْتَمَ النَبِيُّ -صلَّى الله عليه وسلَّم- بِالعِشَاء، فَخَرَج عُمَر فقال: الصَّلاةَ يا رسول الله، رَقَد النِسَاءُ والصِّبيَان. فَخَرَجَ ورَأسُهُ يَقطُر يقول: لَولاَ أن أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي -أو على النَّاس- لَأَمَرتُهُم بهذه الصَّلاة هذه السَّاعَة».
Kutoka kwa Abdillahi bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya Ishaa, akatoka Omar, akasema: Swala Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamelala wanawake na watoto, akatoka na kichwa chake kikitona maji akisema: Lau kama nisingehofia kuwapa tabu umma wangu basi ningewaamrisha swala hii waiswali wakati huu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alichelewa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika swala ya ishaa, mpaka usiku ukawa mkubwa,na wakalala wanawake na watoto, miongoni mwa wale wasiokuwa na uwezo wa kuvumilia kusubiri kwa muda mrefu, akaenda kwake Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akasema: Swala, hakika wamelala wanawake na watoto. Akaja-Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka nyumbani kwake akielekea msikitini na kichwa chake kikitona maji kwasababu ya kuoga na akazungumza kwa kulibainisha hilo kuwa kilichobora katika swala ya ishaa ni kuichelewesha, lau kama si tabu wanazozipata wale wenye kuisubiri swala: Lau kama nisingehofia tabu kwa umma wangu basi ningewaamrisha swala hii katika wakati huu wakuchelewa.

Marejeo

الإلمام بشرح عمدة الأحكام لإسماعيل الأنصاري، ط1، دار الفكر، دمشق، 1381هـ تيسير العلام شرح عمدة الأحكام للبسام، حققه وعلق عليه وخرج أحاديثه وصنع فهارسه: محمد صبحي بن حسن حلاق، ط10، مكتبة الصحابة، الإمارات - مكتبة التابعين، القاهرة، 1426 هـ تنبيه الأفهام شرح عمدة لأحكام لابن عثيمين، ط1، مكتبة الصحابة، الإمارات، 1426هـ عمدة الأحكام من كلام خير الأنام صلى الله عليه وسلم لعبد الغني المقدسي، دراسة وتحقيق: محمود الأرناؤوط، مراجعة وتقديم: عبد القادر الأرناؤوط، ط2، دار الثقافة العربية، دمشق ، بيروت، مؤسسة قرطبة، 1408 هـ صحيح البخاري، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر، ط1، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ. صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، 1423 هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com