Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote

عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَحْسَنَ النَّاسِ خُلُقًا.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na tabia zilizokamilika kuliko watu wote, na mtu wa mbele katika tabia njema na mambo mazuri, kama maneno mazuri, na kufanya heri, na uso mkunjufu, na kujizuia na maudhi na kuyavumilia kutoka kwa wengine.

Mafunzo
  1. Ukamilifu wa tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  2. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yeye ndiye kiigizo kamili katika tabia nzuri.
  3. Himizo la kuiga kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika tabia nzuri.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 45) (6203). صحيح مسلم (4/ 1805) (2310). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 670). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 524). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (9/ 57). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 556).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sifa za kitabia.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com