Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Tabia mbovu.

Hadithi 26

Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا جَمَعَ اللهُ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرْفَعُ لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ، فَقِيلَ: هَذِهِ غَدْرَةُ فُلَانِ بْنِ فُلَانٍ».
Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama atakapowakusanya wa mwanzo na wa mwisho kwa ajili ya hesabu, atasimika kwa kila haini ambaye hakutimiza ahadi aliyokubaliana nayo kwa Mwenyezi Mungu au pamoja na watu, alama ambayo atamfedhehesha kwayo mbele za watu kwa sababu ya hiana yake, na kutanadiwa juu yake siku hiyo: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani; kwa ajili ya kutangaza ubaya wa kitendo chake mbele ya waliokusanyika katika uwanja halaiki (mahashari).

Mafunzo
  1. Uharamu wa hiana na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa; kwa sababu ndani yake kuna ahadi hii kali ya adhabu.
  2. Hiana iliyosemwa katika hadithi inakusanya kila aliyekuamini juu ya damu, au heshima, au siri, au mali, kisha ukamfanyia hiana, na ukaenda kinyume na dhana yake katika kukuamini kwake.
  3. Amesema Qurtubi: Hili ni tamko kutoka kwake linawahusu waarabu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya; kwani wao walikuwa wakinyanyua bendera nyeupe kwa ajili ya kutimiza ahadi, na kwa usaliti bendera nyeusi, ili wamlaumu haini na wamkemee, hadithi ikapelekea kutokea mfano wa hilo kwa haini; ili awe mashuhuri kwa sifa yake hiyo siku ya Kiyama, na watamsema kwa ubaya waliosimama katika uwanja huo.
  4. Amesema bin Hajari: Na katika hadithi hii nikuwa watu siku ya Kiyama wataitwa kwa ubini wa baba zao; kwa kauli yake aliposema: "Huu ni usaliti wa fulani bin fulani".
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 104) (3188) صحيح مسلم (3/ 1359) (1735). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص745). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 188).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

عن أبي بكرة رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «‌أَلَا ‌أُنَبِّئُكُمْ بِأَكْبَرِ الْكَبَائِرِ؟» ثَلَاثًا، قَالُوا: بَلَى يَا رَسُولَ اللهِ، قَالَ: «الْإِشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ» وَجَلَسَ وَكَانَ مُتَّكِئًا، فَقَالَ: «أَلَا وَقَوْلُ الزُّورِ»، قَالَ: فَمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى قُلْنَا: لَيْتَهُ سَكَتَ.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anawaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba zake kuhusu madhambi makubwa, akataja haya matatu: 1- Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu: Nako ni kuielekeza aina yoyote katika aina za ibada kwa asiye Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika uungu wake na uumbaji na ulezi wake na majina yake na sifa zake. 2- Kuwaasi wazazi wawili: Nayo ni kila aina ya maudhi kwa wazazi wawili, sawa sawa iwe kwa kauli au kitendo, na kuacha kuwafanyia wema. 3- Kauli ya uongo ikiwemo ushahidi wa uongo: Nayo ni kila kauli ya kuzusha ya uongo, yenye lengo la kumdhalilisha yule anayekusudiwa kwa kuchukua mali yake au kumfanyia uadui katika heshima yake au mfano wa hayo. Alikariri Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari hii ya kusema uongo ikiwa ni tahadhari juu ya ubaya wake na athari zake mbaya kwa jamii, mpaka wakasema Masahaba: Laiti angelinyamaza; Kwa sababu ya kumhurumia, na kwa kuchukia kile kinachompa kero Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Mafunzo
  1. Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu; kwa sababu amelifanya kuwa dhambi kubwa la kwanza na kubwa kuliko yote, na inayotia mkazo katika hili ni kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi pale anaposhirikishwa, na anasamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye".
  2. Ukubwa wa haki ya wazazi wawili, pale alipoambatanisha haki zao na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 172) (2654)، (8/ 4) (5976)، (8/ 62) (6273-6274). صحيح مسلم (1/ 91) (87). عمدة الأحكام من كلام خير الأنام صلى الله عليه وسلم (ص257) (380). شرح النووي على مسلم (2/ 81). الإلمام بشرح عمدة الأحكام لإسماعيل الأنصاري (2/ 149). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام للبسام (ص703). أعلام السنة المنشورة لاعتقاد الطائفة الناجية المنصورة، لحافظ بن أحمد الحكمي (ص111).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: مَرَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَبْرَيْنِ، فَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَيُعَذَّبَانِ، وَمَا يُعَذَّبَانِ فِي كَبِيرٍ، أَمَّا أَحَدُهُمَا فَكَانَ لاَ يَسْتَتِرُ مِنَ البَوْلِ، وَأَمَّا الآخَرُ فَكَانَ يَمْشِي بِالنَّمِيمَةِ» ثُمَّ أَخَذَ جَرِيدَةً رَطْبَةً، فَشَقَّهَا نِصْفَيْنِ، فَغَرَزَ فِي كُلِّ قَبْرٍ وَاحِدَةً، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، لِمَ فَعَلْتَ هَذَا؟ قَالَ: «لَعَلَّهُ يُخَفِّفُ عَنْهُمَا مَا لَمْ يَيْبَسَا».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili akasema: Hakika watu wa makaburi haya mawili wanaadhibiwa; na wala hawaadhibiwa katika jambo kubwa, hata kama ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Ama mmoja wao alikuwa hajali katika kuhifadhi mwili wake na nguo zake kutokana na mkojo anapokidhi haja yake, Na mwingine alikuwa akitembea kati ya watu kwa uchonganishi, akinukuu maneno ya mtu mwingine kwa lengo la kuwadhuru na kuleta sintofahamu baina yao na ugomvi kati ya watu.

Mafunzo
  1. Uchonganishi na kuacha kujistiri na mkojo ni katika madhambi makubwa na ni katika sababu za adhabu za kaburini.
  2. Mwenyezi Mungu Mtukufu alifunua baadhi ya mambo yaliyofichikana kama adhabu za kaburini ili kuonyesha alama ya utume wake rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Kitendo hiki cha kuchukua tawi na kulipasua vipande viwili na kuviweka juu ya makaburi ni maalumu kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfunulia kuona hali za watu wa makaburi yale mawili, hakiwezi kuwa kipimo cha watu wengine, kwa sababu hakuna ajuaye hali za watu walioko kaburini.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 53) (218). صحيح مسلم (1/ 240) (292). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص43). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص22). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 29).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: «الشِّرْكُ بِاللهِ، وَالسِّحْرُ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللهُ إِلَّا بِالْحَقِّ، وَأَكْلُ الرِّبَا، وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ، وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافِلَاتِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake kujitenga mbali na maovu saba na maasi yenye kuangamiza, na alipoulizwa ni yapi hayo? akayabainisha kuwa ni: La kwanza: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine, kwa kujifanyia mshirika na mfano wake utakasifu ni wake kwa namna yoyote ile itakayokuwa, na kuielekeza aina yoyote ya ibada miongoni mwa ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kaanza na ushirikina; kwa sababu ndio dhambi kubwa kuliko yote. La pili: Uchawi -Nao namna ya ufungaji mafundo na makombe na madawa na ufukishaji mioshi-, yanayoleta athari katika mwili wa mwenye kurogwa kwa kuua au kutia maradhi, au kuwatenganisha kati ya wana ndoa wawili, nayo ni kazi ya kishetani, na wengi wao hawaufikii uchawi isipokuwa kwa ushirikina na kujikurubisha kwa maruhani wachafu kwa kitu wanachokipenda. La tatu: Ni kuua nafsi aliyokataza Allah isiuliwe isipokuwa kwa kigezo cha kisheria, na hutekelezwa na hakimu. La nne: Kutumia riba kwa kula au kwa njia nyingine katika njia za kunufaika. La tano: Kufanya uadui katika mali ya mtoto mdogo aliyefiwa na baba yake naye akiwa chini ya umri wa kubalehe. La sita: Kukimbia katika vita kati ya waislamu na makafiri. La saba: Kuwatuhumu wanawake huru wenye kujizuia na machafu kwa uzinifu, na vile vile kuwatuhumu wanaume.

Mafunzo
  1. Nikuwa madhambi makubwa idadi yake siyo saba pekee, na kutajwa kwake pekee kuwa ni saba ni kwa sababu ya ukubwa wake na hatari yake.
  2. Ruhusa ya kuua nafsi ikiwa ni kwa haki kama kisasi na kuritadi na zinaa baada ya ndoa, na hii hutekelezwa na hakimu aliyewekwa kisheria.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 10) (2766). صحيح مسلم (1/ 92) (89). شرح صحيح البخارى لابن بطال (8/ 489). الملخص في شرح كتاب التوحيد، للشيخ صالح الفوزان (ص201).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata

عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ صُرَدٍ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ جَالِسًا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَجُلاَنِ يَسْتَبَّانِ، فَأَحَدُهُمَا احْمَرَّ وَجْهُهُ، وَانْتَفَخَتْ أَوْدَاجُهُ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي لَأَعْلَمُ كَلِمَةً لَوْ قَالَهَا ذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ، لَوْ قَالَ: أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ، ذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ» فَقَالُوا لَهُ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «تَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ»، فَقَالَ: وَهَلْ بِي جُنُونٌ؟
Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Walitukanana na kushutumiana watu wawili mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ukawa mwekundu uso wa mmoja wao na ikavimba mishipa inayozunguka shingo yake. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninajua neno ambalo lau angelisema huyu aliyekasirika basi hasira zingemuondokea, lau angesema: Audhubillaahi mina sh-shaitwanir rajiim - Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa. Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani. Akasema: Hivi mimi ni mwendawazimu?! Alidhania kuwa hajilindi na Shetani isipokuwa mwenye wazimu.

Mafunzo
  1. Pupa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kutoa muongozo na kuelekeza, panapopatikana sababu zake.
  2. Hasira hutokana na Shetani.
  3. Amri ya kujilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa wakati wa hasira, amesema Mtukufu: "Na ikiwa uchochezi wa Shetani utakuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu.." Mpaka mwisho wa Aya.
  4. Tahadhari ya kutoa matusi na yenye kufanana na matusi kama kutoa laana, na chukizo la hayo; kwa sababu mambo haya hupelekea katika uharibifu baina ya watu.
  5. Kunukuu nasaha kumpelekea ambaye hajazisikia ili anufaike nazo.
  6. Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake dhidi ya hasira; kwa sababu husukuma katika shari na ugomvi, na alikuwa rehema na amani ziwe juu yake hakasiriki isipokuwa yanapotendwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hii ndio hasira nzuri.
  7. Amesema Imam Nawawi katika kauli yake "Kwani unaniona mimi ninawazimu": Kauli hii inaonyesha kuwa msemaji alikuwa ni miongoni mwa wanafiki, au ni katika mabedui wakorofi.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 124) (3282). صحيح مسلم (4/ 2015) (2610). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 110). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص50). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 270). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 78).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت: قُلْتُ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: حَسْبُكَ مِنْ صَفِيَّةَ كَذَا وَكَذَا، -قَالَ أَحدُ الرُّوَاةِ: تَعْنِي قَصِيرَةً- فَقَالَ: «لَقَدْ قُلْتِ كَلِمَةً لَوْ مُزِجَتْ بِمَاءِ الْبَحْرِ لَمَزَجَتْهُ» قَالَتْ: وَحَكَيْتُ لَهُ إِنْسَانًا، فَقَالَ: «مَا أُحِبُّ أَنِّي حَكَيْتُ إِنْسَانًا وَأَنَّ لِي كَذَا وَكَذَا».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Inakutosha kwa Safia kadhaa wa kadhaa, (Anasema mmoja wa wapokezi wa hadithi hii: Alikuwa akikusudia ufupi) Akasema: "Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo" Akasema Aisha: Na nikamsimulia kuhusu mtu fulani, akasema: "Sipendi kuona kuwa kuna mtu nimemsimulia na kwamba mimi nina kadhaa wa kadhaa".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Inakutosha kwa Safia (Alikuwa akikusudia mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake) Kuwa miongoni mwa aibu zake za kimaumbile ya kimwili ni mfupi, Mtume akasema: Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi lingeyazidia na kuyabadili na kuyaharibu, Aisha akasema: Na nilichokifanya ni sawa na kitendo cha mtu kumsema mtu ili kumshusha hadhi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Sipendezwi kuzungumza aibu zake, au kusimulia kuhusu yeye au kufanya mfano wa vitendo vyake, au kusema mfano wa kauli zake, kwa sura ya kumdharau hata kama nitapewa kiasi kingi katika mali za dunia kwa hilo.

Mafunzo
  1. Tahadhari na kitisho dhidi ya kusengenya.
  2. Kuigiza mionekano na kuwasimuliza watu kwa njia ya kudharau na kushusha hadhi ni katika usengenyaji ulioharamishwa.
  3. Kueleza wasifu wa aibu za kimwili ni sehemu katika usengenyaji.
  4. Amesema Kadhi: Kuchanganya na kubadili na kuunganisha kitu na kingine, na maana yake ni kuwa utesi huu lau ungelikuwa ni katika vitu vinavyochanganyikana na Bahari basi ungeibadili kutoka katika hali yake, pamoja na wingi, ni vipi ukiwa katika amali ndogo kisha ukachanganyika nazo!.
  5. Hapa kumeelezwa sehemu miongoni mwa mambo yanayotokea kati ya wana ndoa wawili miongoni mwa wivu.
  6. Kutokubaliana kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na uovu.
  7. Kuifanya dunia kuwa ndogo pamoja na vyote vilivyomo pale inapolinganishwa na radhi za Allah Mtukufu na kutokasirika kwake.
  8. Uislamu ni dini ya tabia njema, na umeamrisha kuhifadhi heshima zisije kuvunjwa kwa kauli au kitendo; kwa sababu hilo ni miongoni mwa mambo yanayopandikiza chuki na uadui kati ya waislamu.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 237) (4875). سنن الترمذي (4/ 275) (2502). مسند أحمد (41/ 433) (24964). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 25). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للقاري (7/ 3046). التيسير بشرح الجامع الصغير، للمناوي (2/ 339). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 411).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَوْ كَانَ لِابْنِ آدَمَ وَادِيَانِ مِنْ مَالٍ لَابْتَغَى وَادِيًا ثَالِثًا، وَلَا يَمْلَأُ جَوْفَ ابْنِ آدَمَ إِلَّا التُّرَابُ، وَيَتُوبُ اللهُ عَلَى مَنْ تَابَ».
Kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu, na hakuna kinachoweza kujaza tumbo la mwanadamu isipokuwa udongo, na Mwenyezi Mungu humsaheme mwenye kuomba msamaha".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba lau kama mwanadamu angelipata bonde moja lililojaa dhahabu, basi angependa kwa sababu ya tamaa yake ambayo ndiyo maumbile yake awe na mabonde mengine mawili, na kwamba mwanadamu haachi kuipupia dunia mpaka anakufa na lijae tumbo lake kwa udongo wa kaburi lake.

Mafunzo
  1. Pupa kubwa ya mwanadamu ya kukusanya mali na vinginevyo katika starehe za Dunia.
  2. Amesema Nawawi: Hapa kumekemewa pupa ya kuipupia Dunia na kupenda wingi wa mali na kuwa na tamaa.
  3. Mwenyezi Mungu anaikubali toba ya mwenye kutubia kutokana na sifa mbaya.
  4. Amesema Nawawi: Hadithi imekuja katika mfumo wa kueleza hali ya wanadamu wengi katika kuipupia Dunia, na inaungwa mkono na kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Na Mwenyezi Mungu humsamehe mwenye kuomba msamaha".
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 93) (6439). صحيح مسلم (2/ 725) (1048). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 54). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 76). المعجم الوسيط، (1/ 148).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «إِيَّاكُمْ وَالظَّنَّ؛ فَإِنَّ الظَّنَّ أَكْذَبُ الْحَدِيثِ، وَلَا تَحَسَّسُوا، وَلَا تَجَسَّسُوا، وَلَا تَحَاسَدُوا، وَلَا تَدَابَرُوا، وَلَا تَبَاغَضُوا، وَكُونُوا عِبَادَ اللهِ إِخْوَانًا».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno, na wala msitiliane shaka (kwa kuhisiana vibaya), na wala msichunguzane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, na wala msichukiane, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na anatahadharisha baadhi ya yale yanayoweza kupelekea kufarakana na uadui baina ya waislamu, na miongoni mwayo: (Dhana) Nazo ni tuhuma zinazojitokeza ndani ya moyo pasina ushahidi, na akabainisha kuwa hayo ni mazungumzo ya uongo mno. Na kuhusu (kuhisiana vibaya): Nako ni kutafuta aibu za watu kwa kutazama au kusikiliza. (Na kupelelezana): Nako ni kutafuta yaliyofichikana miongoni mwa mambo, na hii hutumika zaidi katika shari. Na kuhusu: (Husuda) nako ni kuchukia kupatikana kwa neema kwa watu wengine. Na kuhusu (Kutengana) kwa kuwapuuza baadhi ya watu wenzao, hamsalimii wala hamtembelei ndugu yake muislamu, Na kuhusu: (Kuchukiana) na kuchukia na kubeza, kama kuwaudhi watu wengine, na kutotabasamu, na kukutana nao kwa sura mbaya. Kisha akazungumza neno moja linalokusanya kila kitu, ambalo litatengeneza hali za waislamu baadhi yao kwa baadhi: (Na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja). Udugu ni kiunganishi kinachounganisha mahusiano kati ya watu, na kinazidisha mapenzi na kuzoeana baina yao.

Mafunzo
  1. Dhana mbaya haidhuru kwa mtu ambaye zimedhihiri kwake alama zake, na ni wajibu juu ya muumini awe mwerevu mjanja, hadanganyiki na watu waovu na mafasiki.
  2. Makusudio yake ni kutahadharisha na tuhuma ambazo zinabakia ndani ya nafsi, na kuziendeleza, ama yanayojitokeza ndani ya nafsi na hayabakii haya mtu hachukuliwi katenda dhambi.
  3. Kuchukua tahadhari dhidi ya sababu za kubezana na kukata mahusiano baina ya jamii ya kiislamu, ikiwemo ujasusi na husuda na mfano wake.
  4. Usia kwa muislamu wa kuamiliana na ndugu yake muamala wa ndugu kwa ndugu katika nasaha na mapenzi.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 19) (6064). صحيح مسلم (4/ 1985) (2563). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 219). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 414). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 363).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 26
Hadithi 26
  1. Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani
  2. Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?
  3. Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu
  4. Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza
  5. Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata
  6. Hakika umesema neno ambalo lau lingechanganywa na maji ya Bahari basi (lingeyabadili rangi) kwa kuchanganyika nayo
  7. Lau mwanadamu angelikuwa na mabonde mawili ya mali basi angelitafuta la tatu
  8. Tahadharini na dhana; kwani dhana ni mazungumzo ya uongo mno
  9. Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri
  10. Haingii peponi mfitinishaji
  11. Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi
  12. Hakika watoa laana hawatokuwa mashahidi wala watetezi siku ya Kiyama
  13. Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu
  14. Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi
  15. Atakayejifunza elimu katika yale yanayo ambayo hutafutwa radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu, hajifunzi isipokuwa kwa ajili ya kupata masilahi ya kidunia, basi hatoipata harufu ya Pepo siku ya Kiyama
  16. Je mnajua ni nani aliyefilisika?
  17. Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo
  18. Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao
  19. Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani
  20. Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie
  21. Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekataza kunyoa kiduku
  22. Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha
  23. Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni
  24. Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu
  25. Achaneni (na ubaguzi) kwani una nuka
  26. Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com