Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili akasema: Hakika watu wa makaburi haya mawili wanaadhibiwa; na wala hawaadhibiwa katika jambo kubwa, hata kama ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Ama mmoja wao alikuwa hajali katika kuhifadhi mwili wake na nguo zake kutokana na mkojo anapokidhi haja yake, Na mwingine alikuwa akitembea kati ya watu kwa uchonganishi, akinukuu maneno ya mtu mwingine kwa lengo la kuwadhuru na kuleta sintofahamu baina yao na ugomvi kati ya watu.
- Uchonganishi na kuacha kujistiri na mkojo ni katika madhambi makubwa na ni katika sababu za adhabu za kaburini.
- Mwenyezi Mungu Mtukufu alifunua baadhi ya mambo yaliyofichikana kama adhabu za kaburini ili kuonyesha alama ya utume wake rehema na amani ziwe juu yake.
- Kitendo hiki cha kuchukua tawi na kulipasua vipande viwili na kuviweka juu ya makaburi ni maalumu kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfunulia kuona hali za watu wa makaburi yale mawili, hakiwezi kuwa kipimo cha watu wengine, kwa sababu hakuna ajuaye hali za watu walioko kaburini.
صحيح البخاري (1/ 53) (218). صحيح مسلم (1/ 240) (292). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص43). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص22). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 29).