Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba Jeneza likiwekwa kitandani, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, kwa yale linayoyaona mbele yake katika neema, na likiwa si la mtu mwema, hupiga yowe kwa sauti mbaya ya kukera, na kusema: Nasikitika kwa maangamivu yake, mnalipeleka wapi?! kwa yale linayoyaona mbele yake miongoni mwa adhabu, inasikika sauti yake kwa kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angeliisikia basi angezimia kutokana na ukubwa wa kile alichosikia.
- Maiti mwema huanza kuona habari njema kabla ya kuzikwa kwake, na kafiri hufadhaika, na kuona mambo kinyume na hivyo.
- Baadhi ya suti husikiwa na viumbe vingine tofauti na mwanadamu, na wala mwanadamu hawezi kuzisikia.
- Sunna ni kulibeba Jeneza juu ya mabeba ya wanaume na si wanawake; kwa katazo la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwakataza wanawake kusindikiza Jeneza.
صحيح البخاري (2/ 85) (1314). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 513). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 400). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 122). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 546).