Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili akasema: Hakika watu wa makaburi haya mawili wanaadhibiwa; na wala hawaadhibiwa katika jambo kubwa, hata kama ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Ama mmoja wao alikuwa hajali katika kuhifadhi mwili wake na nguo zake kutokana na mkojo anapokidhi haja yake, Na mwingine alikuwa akitembea kati ya watu kwa uchonganishi, akinukuu maneno ya mtu mwingine kwa lengo la kuwadhuru na kuleta sintofahamu baina yao na ugomvi kati ya watu.
Mafunzo
Uchonganishi na kuacha kujistiri na mkojo ni katika madhambi makubwa na ni katika sababu za adhabu za kaburini.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alifunua baadhi ya mambo yaliyofichikana kama adhabu za kaburini ili kuonyesha alama ya utume wake rehema na amani ziwe juu yake.
Kitendo hiki cha kuchukua tawi na kulipasua vipande viwili na kuviweka juu ya makaburi ni maalumu kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfunulia kuona hali za watu wa makaburi yale mawili, hakiwezi kuwa kipimo cha watu wengine, kwa sababu hakuna ajuaye hali za watu walioko kaburini.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 53) (218).
صحيح مسلم (1/ 240) (292).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص43).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص22).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 29).
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Likiwekwa Jeneza, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, na likiwa si la mtu mwema basi husema: Ubaya ulioje, mnalipeleka wapi? Huisikia sauti yake kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angelisikia basi angezimia".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba Jeneza likiwekwa kitandani, na wanaume wakalibeba katika shingo zao, likiwa ni la mtu mwema basi husema: Niwahisheni, kwa yale linayoyaona mbele yake katika neema, na likiwa si la mtu mwema, hupiga yowe kwa sauti mbaya ya kukera, na kusema: Nasikitika kwa maangamivu yake, mnalipeleka wapi?! kwa yale linayoyaona mbele yake miongoni mwa adhabu, inasikika sauti yake kwa kila kitu isipokuwa mwanadamu, na lau angeliisikia basi angezimia kutokana na ukubwa wa kile alichosikia.
Mafunzo
Maiti mwema huanza kuona habari njema kabla ya kuzikwa kwake, na kafiri hufadhaika, na kuona mambo kinyume na hivyo.
Baadhi ya suti husikiwa na viumbe vingine tofauti na mwanadamu, na wala mwanadamu hawezi kuzisikia.
Sunna ni kulibeba Jeneza juu ya mabeba ya wanaume na si wanawake; kwa katazo la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwakataza wanawake kusindikiza Jeneza.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 85) (1314).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 513).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 400).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 122).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 546).
kutoka kwa Albaraa bin Aazib Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Muislamu atakapoulizwa kaburini anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu", Hiyo ndiyo kauli yake Mtukufu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Ibrahim: 27].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Muumini ataulizwa kaburini, watamuuliza Malaika wawili waliopangiwa kufanya hivyo, nao ni Munkari na Nakiri, kama walivyotajwa katika Hadithi kadhaa, atashuhudia kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hii ndio kauli thabiti aliyoisema Mwenyezi Mungu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera" [Surat Ibrahim: 27].
Mafunzo
Nikuwa maswali ya kaburini ni kweli yapo.
Fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake waumini katika dunia na akahera anawapa nguvu kwa kauli thabiti.
Ubora wa shahada ya tauhidi na kufa juu yake.
Mwenyezi Mungu kumpa thabati (nguvu) Muumini katika dunia ni kwa kumpa msimamo katika imani, na kutembea katika njia iliyonyooka, na wakati wa kufa kwa kufa katika tauhidi, na kaburini wakati akiulizwa na Malaika wawili.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 80) (4699).
صحيح مسلم (4/ 2201) (2871).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 498).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 386).
Kutoka kwa Abdillah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika mmoja wenu anapokufa huonyeshwa makao yake asubuhi na jioni, akiwa katika watu wa peponi basi huonyeshwa katika watu wa peponi, na akiwa katika watu wa motoni basi huonyeshwa katika watu wa motoni, basi husemwa: Haya ndiyo makao yako mpaka atakapokufufua Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mja anapokufa huonyeshwa mbele yake makao yake na sehemu yake maalumu peponi au motoni, mwanzo wa mchana na mwisho wake; mahali pake peponi, na sehemu yake motoni akiwa ni miongoni mwa watu wa motoni, na huambiwa: Haya ndiyo makao yako utakayofufuliwa kwayo siku ya Kiyama; na katika hilo kuna kuneemeka kwa muumini, na kuadhibiwa kwa kafiri.
Mafunzo
Adhabu za kaburi na neema zake ni kweli.
Amesema bin Hajari: Hakika kuonyeshwa huku kwa muumini na kafiri kuko wazi, na ama muumini aliyechanganya mema na maovu inategemea anaweza kuonyeshwa makao yake katika pepo atakayofikia.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 99-100) (1379).
صحيح مسلم (4/ 2199) (2866).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري، لبدرالدين العيني (8/ 209).
التنوير شرح الجامع الصغير، لمحمد الصنعاني (2/ 209).
الإفصاح عن معاني الصحاح، ليحيى بن هبيرة (4/ 131).
عن المقدام بن معدِيْكَرِب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «أَلَا هَلْ عَسَى رَجُلٌ يَبْلُغُهُ الْحَدِيثُ عَنِّي وَهُوَ مُتَّكِئٌ عَلَى أَرِيكَتِهِ فَيَقُولُ: بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ كِتَابُ اللهِ، فَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَلَالًا اسْتَحْلَلْنَاهُ، وَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَرَامًا حَرَّمْنَاهُ، وَإِنَّ مَا حَرَّمَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَمَا حَرَّمَ اللهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Mikdad Bin Maadi Karbi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu hivyo tukikuta halali ndani yake tutaihalalisha na tukikuta ndani yake kuna haramu tutaiharamisha, na kwa hakika chochote alichokiharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na amani ziwe juu yake ni kama alichokiharamisha Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo
Amefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake kuwa umefika wakati kutakuwa na kundi la watu, mmoja wao atakuwa amekaa na kuegemea katika tandiko lake, inamfikia hadithi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kusema: Kitakachotuamua kati yetu na nyie kwenye mambo yetu ni Qur'ani tukufu pekee ndiyo inatutosha, tukikuta ndani yake halali tunaifanyia kazi, na tukikuta ndani yake haramu tunajiepusha nayo. kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila kitu alichokiharamisha au kukikataza katika sunna zake basi mambo hayo hukumu yake ni kama alivyoharamisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake; kwa kuwa yeye ni mfikishaji kwa niaba ya Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Kuitukuza Sunna kama inavyotukuzwa Qur'ani tukufu na kuhukumu kwayo.
Kumtii Mtume ndiyo kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi Mtume ndiyo kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kuthibitika kuwa Sunna ni hoja, na jawabu kwa mwenye kuikataa Sunna au kuipinga.
Na mwenye kuipinga Sunna na kudai kuwa Qur'ani pekee yamtosha, basi mtu huyo atakuwa kavipinga vyote viwili, na ni muongo kwa kudai kwake kuifuata Qur'ani.
Miongoni mwa alama za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake-, ni kutoa taarifa ya kitu kuwa kitatokea mbeleni na hutokea kama alivyotoa taarifa.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 13) (4604)، سنن الترمذي (4/ 399) (2664)، سنن ابن ماجه (1/ 9) (12)، نخب الأفكار في تنقيح مباني الأخبار في شرح معاني الآثار (13/ 154).
Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Nitawahadithieni Hadithi nimeisikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hadithi hiyo hatowahadithia yeyote asiyekuwa mimi: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake anasema: "Kwa hakika miongoni mwa alama za Kiyama ni kuondolewa elimu, na kuzidi ujinga, na kukithiri uzinifu, unywaji pombe, na wanaume watakuwa wachache na wanawake watakuwa wengi mpaka itafikia wanawake hamsini kusimamiwa na mwanaume mmoja."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika alama za kukaribia Kiyama ni kuondolewa elimu ya sheria na kuondolewa kwake itakuwa ni kwa kufa wanachuoni. Na matokeo yake utazidi na utaenea ujinga, na uzinifu utaenea na uchafu, na unywaji pombe utazidi na idadi ya wanaume itapungua na ya wanawake itazidi; Mpaka itafikia hatua mwanaume mmoja atabeba mambo yao na kusimamia maslahi yao.
Mafunzo
Kumewekwa wazi baadhi ya alama za Kiyama.
Kujua muda wa Kiyama ni katika mambo ya ghaibu (yasiyoonekana wala kujulikana) ni katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha.
Himizo juu ya kujifunza elimu ya kisheria kabla ya kukosekana kwake.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 37) (5231)، صحيح مسلم (4/ 2056) (2671)، فتح الباري لابن حجر (9/ 330)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (20/ 213).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka apite mtu juu ya kaburi la mtu aseme: Natamani ningekua nafasi yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Kiyama hakitosimama mpaka mtu apite katika kaburi atamani laiti angelikuwa maiti mfano wake, na sababu ni kuihofia nafsi yake kwa kutoweka dini yake kwa kuzidiwa na batili na waovu, na kudhihiri kwa fitina na maasi na maovu.
Mafunzo
Kuna ishara ya kudhihiri maasi na fitina zama za mwisho.
Himizo la kuchukua tahadhari na kujiandaa na mauti kwa imani na matendo mema, na kujiweka mbali na mazingira ya fitina na balaa.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 58) (7115)، صحيح مسلم (4/ 2231) (157)، إكمال المعلم (8/451)، شرح ابن بطال (10/58)، الإفصاح عن معاني الصحاح (6/295)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (44/ 388).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Hakitasimama Kiyama mpaka mpigane na Mayahudi, mpaka jiwe ambalo nyuma yake kuna Myahudi liseme: Ewe Muislamu huyu hapa Myahudi nyuma yangu njoo umuuwe."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Kiyama hakitasimama mpaka Waislamu watakapopigana na Mayahudi, Mpaka atakapo kimbia Myahudi nyuma ya mawe ili ajifiche waislamu wasimuone; Mwenyezi Mungu atalitamkisha jiwe na litamuita Muislamu: Na kumwambia kuwa Myahudi yupo nyuma yake mpaka aje na amuuwe.
Mafunzo
Kutoa habari -Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-ya baadhi ya mambo yaliyofichikana na yatakayotokea baadaye, kwa namna ambayo Mwenyezi Mungu alivyomuonesha, na mambo hayo yatatokea kwa lazima.
Waislamu kupigana na Mayahudi katika zama za mwisho, na tukio hilo ni katika alama za Kiyama.
Kubakia kwa Dini ya Uislamu mpaka siku ya Kiyama, na itazishinda dini zote.
Nusura ya Mwenyezi Mungu kwa waislamu dhidi ya maadui zao, na katika hilo la kuwashinda ameyafanya mawe yaongee katika siku za mwisho.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 42) (2926)، صحيح مسلم (4/ 2238) (2921)، عمدة القاري (14/199) الكوكب الوهاج شرح صحيح مسلم (26/198).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com