Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kutakuwa mwisho wa umma wangu na watu, wakikuhadithieni mambo ambayo humkuwahi kuyasikia nyinyi wala baba zenu, ole wenu na ole wao

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «سَيَكُونُ فِي آخِرِ أُمَّتِي أُنَاسٌ يُحَدِّثُونَكُمْ مَا لَمْ تَسْمَعُوا أَنْتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ، فَإِيَّاكُمْ وَإِيَّاهُمْ».
Kutoka kwa Abuu Huraira kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kutakuwa mwisho wa umma wangu na watu, wakikuhadithieni mambo ambayo humkuwahi kuyasikia nyinyi wala baba zenu, ole wenu na ole wao".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa watatokea watu katika zama za mwisho katika umma wake wakizua uongo, na wakisema mambo ambayo hakuyasema yeyote kabla yao, wataeleza simulizi za uongo na za kutunga, akatuamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- tujiweke mbali nao na wala tusikae nao, na wala tusisikilize mazungumzo yao; ili hadithi hizo za kutunga tusiziweke ndani ya nafsi, tukashindwa kujiepusha nazo.

Mafunzo
  1. Kuna alama miongoni mwa alama za utume, kiasi kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alieleza yatakayotokea katika umma wake, na yamekuwa kama alivyoeleza.
  2. Kujitenga mbali na watu wanaomzulia uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na dini ya Uislamu, na kutosikiliza uongo wao.
  3. Tahadhari na kukubali simulizi au kuzisambaza ila baada ya kuzihakiki kupata usahihi wake na kuthibiti kwake.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 12) (6)، قرة عين المحتاج في شرح مقدمة صحيح مسلم بن الحجاج (2/ 8).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Umuhimu wa sunnah na Nafasi yake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com