Amesema Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili nikihifadhi kwa kukiandika, mabwana wa kikuraishi wakanikataza, na wakasema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu anazungumza katika furaha na hasira, na huenda akakosea, nikaacha kuandika. Nikamueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- waliyosema, akaashiria kwa kidole chake kinywani kwake akasema: Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake haitoki ndani yake ila haki kwa hali zote, na katika furaha na hasira. Na alisema Mtukufu kumuhusu Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hatamki kwa matamanio * Si vinginevyo, ila huo ni wahyi anaofunuliwa" [An najm: 3-4].
- Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekingwa katika yale anayoyafikisha kutoka kwa Mola wake Aliyetakasika na kutukuka, katika furaha na hasira.
- Pupa ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kuihifadhi sunna na kuifikisha.
- Kufaa kuapa hata kama hakuna masilahi katika hilo, kama kulitilia mkazo jambo.
- Kuiandika elimu ni katika sababu kubwa zinazoihifadhi elimu.
سنن أبي داود (5/ 489) (3646)، شرح سنن أبي داود للعباد (412/ 21).