Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Umuhimu wa sunnah na Nafasi yake.

Hadithi 8

Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً، وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Fikisheni kutoka kwangu japokuwa aya moja, na simulieni kuhusu wana wa Israeli wala hakuna ubaya, na yeyote atakayenisemea uongo mimi kwa makusudi basi na ajiandae, makazi yake ni motoni".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuifikisha elimu kutoka kwake katika Qur'ani na mafundisho yake (Sunna), hata kama kitu kitakuwa kidogo kama aya moja toka ndani ya Qur'ani au hadithi, kwa sharti mfikishaji awe mjuzi katika kile anachokifikisha na kuwalingania watu kwacho. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna ubaya kusimulia kuhusu wana wa Israeli kwa yale yaliyotokea kwao katika matukio, yale yasiyokinzana na sheria yetu. Kisha akatahadharisha kumzulia uongo, nakuwa yeyote mwenye kumzulia uongo kwa makusudi basi ajiandalie mwenyewe makazi yake motoni.

Mafunzo
  1. Himizo la kufikisha sheria ya Allah, nakuwa mtu anajukumu la kuyafikisha aliyoyahifadhi na kuyaelewa hata kama ni kidogo.
  2. Ulazima wa kutafuta elimu ya kisheria, ili mtu awe na uwezo wa kumuabudu Allah na kuifikisha sheria yake kwa sura sahihi.
  3. Uwajibu wa kuhakiki usahihi wa kila hadithi kabla ya kuifikisha au kuisambaza kwa kutahadhari kutoingia katika ahadi hii ya adhabu kali.
  4. Himizo la ukweli katika maneno, na kuchukua tahadhari katika mazungumzo, ili mtu asiingie katika uongo, na hasa hasa katika sheria ya Allah -Aliyetakasika na kutukuka-.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 170) (3461). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 464). نزهة المتقين، لمصطفى الخن وغيره (2/ 951). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 429).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo

عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدَبٍ وَالْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ رضي الله عنهما قَالَا: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ حَدَّثَ عَنِّي بِحَدِيثٍ يُرَى أَنَّهُ كَذِبٌ، فَهُوَ أَحَدُ الْكَاذِبِينَ».
Kutoka kwa Samura bin Jundab na Mughira bin Shu'ba radhi za Allah ziwe juu yao, wamesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo"
Imepokelewa na Imamu Muslim katika Utangulizi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayenukuu Hadithi kutoka kwake hali yakuwa anajua au anadhani au dhana yake kubwa kuwa ni kumzulia uongo rehema na amani ziwe juu yake; basi mpokezi atashirikiniana na mwanzilishi wa uongo huu katika dhambi.

Mafunzo
  1. Kuzichunguza hadithi zinazopokelewa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kupata uhakika wa usahihi wake kabla ya kuzipokea na kuzisimulia.
  2. Sifa ya uongo ataitwa kila aliyezusha uongo na kwa yule atakayeuhamisha na kuusambaza kwa watu wengine.
  3. Ni haramu kusimulia Hadithi ya uzushi kwa mtu anayejua kuwa ni ya kutunga, au anayedhania kuwa ni ya kutunga, isipokuwa kama ni kwa ajili ya kutahadharisha.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 8).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu

عن المقدام بن معدِيْكَرِب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «أَلَا هَلْ عَسَى رَجُلٌ يَبْلُغُهُ الْحَدِيثُ عَنِّي وَهُوَ مُتَّكِئٌ عَلَى أَرِيكَتِهِ فَيَقُولُ: بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ كِتَابُ اللهِ، فَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَلَالًا اسْتَحْلَلْنَاهُ، وَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَرَامًا حَرَّمْنَاهُ، وَإِنَّ مَا حَرَّمَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَمَا حَرَّمَ اللهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Mikdad Bin Maadi Karbi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu hivyo tukikuta halali ndani yake tutaihalalisha na tukikuta ndani yake kuna haramu tutaiharamisha, na kwa hakika chochote alichokiharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na amani ziwe juu yake ni kama alichokiharamisha Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo

Amefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake kuwa umefika wakati kutakuwa na kundi la watu, mmoja wao atakuwa amekaa na kuegemea katika tandiko lake, inamfikia hadithi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kusema: Kitakachotuamua kati yetu na nyie kwenye mambo yetu ni Qur'ani tukufu pekee ndiyo inatutosha, tukikuta ndani yake halali tunaifanyia kazi, na tukikuta ndani yake haramu tunajiepusha nayo. kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila kitu alichokiharamisha au kukikataza katika sunna zake basi mambo hayo hukumu yake ni kama alivyoharamisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake; kwa kuwa yeye ni mfikishaji kwa niaba ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Kuitukuza Sunna kama inavyotukuzwa Qur'ani tukufu na kuhukumu kwayo.
  2. Kumtii Mtume ndiyo kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi Mtume ndiyo kumuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Kuthibitika kuwa Sunna ni hoja, na jawabu kwa mwenye kuikataa Sunna au kuipinga.
  4. Na mwenye kuipinga Sunna na kudai kuwa Qur'ani pekee yamtosha, basi mtu huyo atakuwa kavipinga vyote viwili, na ni muongo kwa kudai kwake kuifuata Qur'ani.
  5. Miongoni mwa alama za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake-, ni kutoa taarifa ya kitu kuwa kitatokea mbeleni na hutokea kama alivyotoa taarifa.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 13) (4604)، سنن الترمذي (4/ 399) (2664)، سنن ابن ماجه (1/ 9) (12)، نخب الأفكار في تنقيح مباني الأخبار في شرح معاني الآثار (13/ 154).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ».
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemsemea uongo kwa makusudi kwa kumnasibishia kauli au kitendo kwa uongo, basi atambue kuwa Akhera atakua na makazi motoni; ndio malipo yake kwa kumsingizia kwake uongo.

Mafunzo
  1. Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa makusudi kabisa ni sababu ya kuingia motoni.
  2. Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- si sawa na kuwasemea uongo watu wengine, kwa kuwa hilo linaambatana na madhara makubwa katika dini na dunia.
  3. Hii ni tahadhari ya kusambaza hadithi kabla ya kuthibitisha usahihi wake kuwa ni kweli zimenasibishwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- au la!.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 33) (110)، صحيح مسلم (1/ 10) (3)، إكمال المعلم (1/111)، شرح النووي على مسلم (1/65)، المفهم (1/32)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (2/ 151)، شرح مقدمة سنن ابن ماجه (5/ 8).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi

عن العِرْباضِ بن ساريةَ رضي الله عنه قال: قام فينا رسول الله صلى الله عليه وسلم ذات يوم، فوَعَظَنا مَوعظةً بليغةً وَجِلتْ منها القلوبُ، وذَرَفتْ منها العيونُ، فقيل: يا رسول الله، وعظتَنَا موعظةَ مُودِّعٍ فاعهد إلينا بعهد. فقال: «عليكم بتقوى الله، والسمع والطاعة، وإن عبدًا حبشيًّا، وسترون من بعدي اختلافًا شديدًا، فعليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين، عَضُّوا عليها بالنواجِذ، وإياكم والأمور المحدثات، فإن كل بدعة ضلالة».
Na kutoka kwa Irbadhi bin Sariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kushikamana na sunna na kuifuata.
  2. Kuyatilia umuhimu mawaidha na kulainisha nyoyo.
  3. Amri ya kuwafuata mahalifa wanne waongofu baada yake, nao ni Abuubakari na Omari, na Othman, na Ally radhi za Allah ziwe juu ya wote.
  4. Katazo la kuzua katika Dini, nakuwa uzushi wote ni upotofu.
  5. Usikivu na utii kwa atakayesimamia mambo ya waumini katika yale yasiyokuwa maasi.
  6. Umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati na hali zote.
  7. Hitilafu lazima itokee katika umma huu, na wakati wa kutokea kwake ni lazima kurejea katika Sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mahalifa waongofu.
Marejeo

الأربعون النووية (ص: 89) (ح28)، سنن أبي داود (7/ 16) (4607)، سنن الترمذي (4/ 408) (2676)، سنن ابن ماجه (1/ 28) (42)، مسند أحمد (28/ 367) (17142)، تحفة الأحوذي (7/ 366)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (12/ 235)، شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 278).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kutakuwa mwisho wa umma wangu na watu, wakikuhadithieni mambo ambayo humkuwahi kuyasikia nyinyi wala baba zenu, ole wenu na ole wao

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «سَيَكُونُ فِي آخِرِ أُمَّتِي أُنَاسٌ يُحَدِّثُونَكُمْ مَا لَمْ تَسْمَعُوا أَنْتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ، فَإِيَّاكُمْ وَإِيَّاهُمْ».
Kutoka kwa Abuu Huraira kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kutakuwa mwisho wa umma wangu na watu, wakikuhadithieni mambo ambayo humkuwahi kuyasikia nyinyi wala baba zenu, ole wenu na ole wao".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa watatokea watu katika zama za mwisho katika umma wake wakizua uongo, na wakisema mambo ambayo hakuyasema yeyote kabla yao, wataeleza simulizi za uongo na za kutunga, akatuamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- tujiweke mbali nao na wala tusikae nao, na wala tusisikilize mazungumzo yao; ili hadithi hizo za kutunga tusiziweke ndani ya nafsi, tukashindwa kujiepusha nazo.

Mafunzo
  1. Kuna alama miongoni mwa alama za utume, kiasi kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alieleza yatakayotokea katika umma wake, na yamekuwa kama alivyoeleza.
  2. Kujitenga mbali na watu wanaomzulia uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na dini ya Uislamu, na kutosikiliza uongo wao.
  3. Tahadhari na kukubali simulizi au kuzisambaza ila baada ya kuzihakiki kupata usahihi wake na kuthibiti kwake.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 12) (6)، قرة عين المحتاج في شرح مقدمة صحيح مسلم بن الحجاج (2/ 8).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki

عن عبدِ الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: كنتُ أكتبُ كلَّ شيءٍ أسمعُه من رسولِ الله صلَّى الله عليه وسلم أُريدُ حفْظَه، فنهتْني قريشٌ، وقالوا: أتكْتبُ كلَّ شيءٍ تَسمَعُه من رسول الله صلَّى الله عليه وسلم، ورسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم بَشَرٌ يتكلَّمُ في الغضَبِ والرِّضا؟ فأمسَكتُ عن الكتاب، فذكرتُ ذلك لرسول الله صلَّى الله عليه وسلم، فأومأ بإصبَعِه إلى فيه، فقال: «اكتُبْ، فوالذي نفسي بيدِه، ما يَخرُجُ منه إلا حقٌّ».
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kukihifadhi, Makuraishi wakanikataza, na wakasema: Hivi unaandika kila kitu unachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu huzungumza wakati wa hasira na furaha? Nikaacha kuandika, nikamueleza hilo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaashiria kwa kidole chake katika kinywa chake, akasema: "Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaSahihi
Maelezo

Amesema Abdallah bin Amri radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili nikihifadhi kwa kukiandika, mabwana wa kikuraishi wakanikataza, na wakasema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu anazungumza katika furaha na hasira, na huenda akakosea, nikaacha kuandika. Nikamueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- waliyosema, akaashiria kwa kidole chake kinywani kwake akasema: Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake haitoki ndani yake ila haki kwa hali zote, na katika furaha na hasira. Na alisema Mtukufu kumuhusu Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hatamki kwa matamanio * Si vinginevyo, ila huo ni wahyi anaofunuliwa" [An najm: 3-4].

Mafunzo
  1. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekingwa katika yale anayoyafikisha kutoka kwa Mola wake Aliyetakasika na kutukuka, katika furaha na hasira.
  2. Pupa ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kuihifadhi sunna na kuifikisha.
  3. Kufaa kuapa hata kama hakuna masilahi katika hilo, kama kulitilia mkazo jambo.
  4. Kuiandika elimu ni katika sababu kubwa zinazoihifadhi elimu.
Marejeo

سنن أبي داود (5/ 489) (3646)، شرح سنن أبي داود للعباد (412/ 21).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu

عَنْ أَبِي نَجِيحٍ العِرْبَاضِ بْنِ سَارِيَةَ رضي الله عنه قَالَ: وَعَظَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنْهَا القُلُوبُ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا العُيُونُ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ! كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ؛ فَأَوْصِنَا، قَالَ: «أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللَّهِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ، وَإِنْ تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ بَعْدِي فَسَيَرَى اخْتِلَافًا كَثِيرًا، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيينَ، عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الأُمُورِ؛ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ».
Imesimuliwa kutoka kwa Abuu Najihi Al-'Irbat bin Sariya, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ya kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alituaidhi mawaidha makali sana. Nyoyo zikajaa hofu kwa sababu yake, na macho yakamiminika machozi kwa sababu yake, basi tukasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kama kwamba ni mawaidha ya anayeaga. Basi tuusie." Akasema: "Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu, zikamateni na kuzing'ata kwa magego. Na jihadharini na mambo ya kuzushwa. Kwani kila jambo jipya (katika dini) ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu."
Imepokelewa na Abu Daud na TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kushikamana na sunna na kuifuata.
  2. Kuyatilia umuhimu mawaidha na kulainisha nyoyo.
  3. Amri ya kuwafuata mahalifa wanne waongofu baada yake, nao ni Abuubakari na Omari, na Othman, na Ally radhi za Allah ziwe juu ya wote.
  4. Katazo la kuzua katika Dini, nakuwa uzushi wote ni upotofu.
  5. Usikivu na utii kwa atakayesimamia mambo ya waumini katika yale yasiyokuwa maasi.
  6. Umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati na hali zote.
  7. Hitilafu lazima itokee katika umma huu, na wakati wa kutokea kwake ni lazima kurejea katika Sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mahalifa waongofu.
Marejeo

الأربعون النووية (ص: 89) (ح28). سنن أبي داود (7/ 16) (4607). سنن الترمذي (4/ 408) (2676). سنن ابن ماجه (1/ 28) (42). مسند أحمد (28/ 367) (17142). تحفة الأحوذي (7/ 366). عون المعبود وحاشية ابن القيم (12/ 235). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 278).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com