Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu

عَنْ أَبِي نَجِيحٍ العِرْبَاضِ بْنِ سَارِيَةَ رضي الله عنه قَالَ: وَعَظَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنْهَا القُلُوبُ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا العُيُونُ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ! كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ؛ فَأَوْصِنَا، قَالَ: «أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللَّهِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ، وَإِنْ تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ بَعْدِي فَسَيَرَى اخْتِلَافًا كَثِيرًا، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيينَ، عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الأُمُورِ؛ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ».
Imesimuliwa kutoka kwa Abuu Najihi Al-'Irbat bin Sariya, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ya kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alituaidhi mawaidha makali sana. Nyoyo zikajaa hofu kwa sababu yake, na macho yakamiminika machozi kwa sababu yake, basi tukasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kama kwamba ni mawaidha ya anayeaga. Basi tuusie." Akasema: "Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu, zikamateni na kuzing'ata kwa magego. Na jihadharini na mambo ya kuzushwa. Kwani kila jambo jipya (katika dini) ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu."
Imepokelewa na Abu Daud na TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kushikamana na sunna na kuifuata.
  2. Kuyatilia umuhimu mawaidha na kulainisha nyoyo.
  3. Amri ya kuwafuata mahalifa wanne waongofu baada yake, nao ni Abuubakari na Omari, na Othman, na Ally radhi za Allah ziwe juu ya wote.
  4. Katazo la kuzua katika Dini, nakuwa uzushi wote ni upotofu.
  5. Usikivu na utii kwa atakayesimamia mambo ya waumini katika yale yasiyokuwa maasi.
  6. Umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati na hali zote.
  7. Hitilafu lazima itokee katika umma huu, na wakati wa kutokea kwake ni lazima kurejea katika Sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mahalifa waongofu.
Marejeo

الأربعون النووية (ص: 89) (ح28). سنن أبي داود (7/ 16) (4607). سنن الترمذي (4/ 408) (2676). سنن ابن ماجه (1/ 28) (42). مسند أحمد (28/ 367) (17142). تحفة الأحوذي (7/ 366). عون المعبود وحاشية ابن القيم (12/ 235). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 278).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Umuhimu wa sunnah na Nafasi yake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com