عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ».
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemsemea uongo kwa makusudi kwa kumnasibishia kauli au kitendo kwa uongo, basi atambue kuwa Akhera atakua na makazi motoni; ndio malipo yake kwa kumsingizia kwake uongo.
Mafunzo
- Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa makusudi kabisa ni sababu ya kuingia motoni.
- Kumsemea uongo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- si sawa na kuwasemea uongo watu wengine, kwa kuwa hilo linaambatana na madhara makubwa katika dini na dunia.
- Hii ni tahadhari ya kusambaza hadithi kabla ya kuthibitisha usahihi wake kuwa ni kweli zimenasibishwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- au la!.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 33) (110)، صحيح مسلم (1/ 10) (3)، إكمال المعلم (1/111)، شرح النووي على مسلم (1/65)، المفهم (1/32)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (2/ 151)، شرح مقدمة سنن ابن ماجه (5/ 8).