Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani

عَنْ هِشَامِ بْنِ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ رَضيَ اللهُ عنهما أَنَّهُ مَرَّ عَلَى أُنَاسٍ مِنَ الْأَنْبَاطِ بِالشَّامِ، قَدْ أُقِيمُوا فِي الشَّمْسِ، فَقَالَ: مَا شَأْنُهُمْ؟ قَالُوا: حُبِسُوا فِي الْجِزْيَةِ، فَقَالَ هِشَامٌ: أَشْهَدُ لَسَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ اللهَ يُعَذِّبُ الَّذِينَ يُعَذِّبُونَ النَّاسَ فِي الدُّنْيَا».
Kutoka kwa Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba yeye alipita kwa watu miongoni mwa Anbat huko Sham, wakiwa wamesimamishwa juani, akasema: Wamekuwaje? Wakasema: Wamefungwa kwa sababu ya jizia (kodi), akasema Hisham: Ninashuhudia kuwa nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alipita Hisham bin Hakim bin Hizam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, kwa wakulima wasiokuwa Waarabu huko Sham, wakiwa wamesimamishwa chini ya joto la Jua, akauliza kuhusu jambo lililowapata? Akaambiwa kuwa wamefanywa hivyo kwa sababu ya kutolipa Jizia (kodi) hali yakuwa wanauwezo wa kulipa. Amesema Hisham radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ninashuhudia kuwa hakika nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Hakika Mwenyezi Mungu huwaadhibu wale wanaowaadhibu watu duniani kwa dhuluma pasina haki.

Mafunzo
  1. Jizia: Ni mali inayowekwa kuwa sheria kwa wanaume miongoni mwa Mayahudi na Manaswara waliobalehe wenye uwezo, kwa ajili ya kulindwa kwao na kuishi kwao katika mji wa kiislamu.
  2. Uharamu wa kuwaadhibu watu hata makafiri, pasina kigezo cha kisheria.
  3. Onyo kwa madhalimu kutokana na dhuluma.
  4. Walishikamana Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kuamrisha mema na kukataza maovu.
  5. Amesema Nawawi: Hii inachukuliwa katika kuadhibu bila haki, haiingii kuadhibu kwa haki kama kisasi, na kusimamishiwa sheria, na kuonya, na mfano wake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2018) (2613). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1103). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (19/ 108). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 117). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (6/ 2301). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 295).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia mbovu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com