Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha

عن أنس رضي الله عنه قال: كُنَّا عِنْدَ عُمَرَ فَقَالَ: «نُهِينَا عَنِ التَّكَلُّفِ».
Imepokewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Tulikuwa kwa Omari akasema: "Tumekatazwa kujilazimisha".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Omari -Radhi za Allaha ziwe juu yake- kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwakataza kuyafanya mambo yenye uzito bila kuwa na haja nayo, sawa sawa iwe ni kauli au kitendo.

Mafunzo
  1. Miongoni mwa kujikalifisha kuliko katazwa: Kuuliza uliza, au mtu kujikalifisha mambo asiyo na elimu nayo, au akalikazia jambo ambalo Mwenyezi Mungu kalipa nafasi pana.
  2. Ni lazima muislamu ailazimishe nafsi yake wepesi na kutojikalifisha katika kauli na vitendo: Katika kula kwake, na kunywa kwake, na maneno yake, na hali zake zote.
  3. Uislamu ni dini ya wepesi.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 95) (7293). نزهة المتقين، لمصطفى الخن وغيره (2/ 1136). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 391). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن حجر (13/ 270). النهاية في غريب الحديث والأثر، لابن الأثير (4/ 196). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص930).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Tabia mbovu.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com