Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ubora na fadhila za matendo mema.

Hadithi 20

Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «رِبَاطُ يَوْمٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ مِنَ الجَنَّةِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَالرَّوْحَةُ يَرُوحُهَا العَبْدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوِ الغَدْوَةُ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kubakia katika eneo ambalo liko kati ya waislamu na makafiri kwa ajili ya kuwalinda dhidi yao kwa siku moja, kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba mahali pa kuweka mjeledi unaotumika kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba malipo na thawabu za kutembea katika wakati wa mwanzo wa mchana mpaka mwanzo wa wakati wa adhuhuri, au mchana: Ni kwanzia adhuhuri mpaka usiku katika njia ya Mwenyezi Mungu mara moja, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.

Mafunzo
  1. Fadhila za kuthubutu katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya hatari zilizomo zinazoihatarisha nafsi, na kwa yale yanayofungamana nalo kama kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuitetea dini yake, kwa hivyo, thawabu za siku moja pekee, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  2. Udhalili wa dunia ukiilinganisha na akhera; kwa sababu sehemu ya kuweka mjeledi pekee peponi, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  3. Ubora wa kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ukubwa wa thawabu zake; kwa sababu thawabu za mwendo mmoja wa asubuhi au mchana, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  4. Kauli yake: "Katika njia ya Mwenyezi Mungu" hapa kuna dalili ya umuhimu wa kutakasa nia, na kwamba malipo yanaambatana na hilo.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 35) (2892). صحيح مسلم (3/ 1500) (1881). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص739).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمِنين رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ: جَاءَتْنِي مِسْكِينَةٌ تَحْمِلُ ابْنَتَيْنِ لَهَا، فَأَطْعَمْتُهَا ثَلَاثَ تَمَرَاتٍ، فَأَعْطَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِنْهُمَا تَمْرَةً، وَرَفَعَتْ إِلَى فِيهَا تَمْرَةً لِتَأْكُلَهَا، فَاسْتَطْعَمَتْهَا ابْنَتَاهَا، فَشَقَّتِ التَّمْرَةَ الَّتِي كَانَتْ تُرِيدُ أَنْ تَأْكُلَهَا بَيْنَهُمَا، فَأَعْجَبَنِي شَأْنُهَا، فَذَكَرْتُ الَّذِي صَنَعَتْ لِرَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «إِنَّ اللهَ قَدْ أَوْجَبَ لَهَا بِهَا الْجَنَّةَ، أَوْ أَعْتَقَهَا بِهَا مِنَ النَّارِ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alinijia mwanamke mmoja Masikini akiwa amebeba mabinti zake wawili, nikawalisha tende tatu, akawapa kila mmoja wao tende moja, kisha akanyanyua tende moja ili kuitumia , akawalishi mabinti zake kwa kuigawa tende ile vipande viwili, ambayo alihitaji kuila mwenyewe, kikanistaajabisha kitendo chake hicho, nikamueleza Mtume alicho kifanya mwanamke yule, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleeza mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba mwanamke moja masikini alimjia akiwa kawabeba watoto wake wa kike wawili, akamuomba chakula, akampatia tende tatu, akampatia kila mmoja miongoni mwa mabinti zake tende moja ili ale, watoto wake wakaihitaji tende ile mmoja aliyotaka kuila, akawakatia tende ile vipande viwili, jambo hilo likamshanga mno Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akakieleza kitendo alichokifanya mwanamke yule kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika Mwenyezi Mungu kamuwajibishia Pepo kwa tende hii, au kamuacha huru na Moto.

Mafunzo
  1. Fadhila ya sadaka hata kama ikiwa ndogo, nayo inaonyesha ukweli wa Muumini katika imani yake kwa Mola wake Mlezi na uaminifu wake kwa ahadi yake na fadhila zake.
  2. Ukubwa wa huruma ya akina mama kwa watoto, na hofu yao juu ya kuwapoteza.
  3. Fadhila za kuidhiki nafsi kwa kuwapendelea wengine, na kuwahurumia wadogo, na ziada ya wema na upole kwa watoto wa kike, na kwamba hilo ni sababu ya kuingia Peponi, na kuachwa huru na Moto.
  4. Kitu kidogo hakizuiliwi kutolewa sadaka kwa sababu ya kubezwa kwake, bali ni wajibu kwa amtoaji sadaka atoe sadaka kwa kiasi anachokiweza kiwe kidogo au kikubwa.
  5. Hapa kumeelezwa hali zilivyokuwa nyumba za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na vipi yalikuwa maisha yake na familia yake, kiasi kwamba hapakuwa na chochote cha kuliwa ndani ya nyumba zao, zaidi ya tende moja au tatu.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2027) (2630). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص199). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 111). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 278).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hana mja wangu muumini toka kwangu malipo yoyote pindi ninapomchukua kipenzi chake katika familia yake duniani kisha akasubiri (malipo mazuri) zaidi ya pepo

عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «يقول الله تعالى : ما لِعَبدِي المُؤمن عِندِي جَزَاء إِذَا قَبَضتُ صَفِيَّه مِنْ أَهلِ الدُّنيَا ثُمَّ احْتَسَبَه إِلاَّ الجنَّة».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hana mja wangu muumini toka kwangu malipo yoyote pindi ninapomchukua kipenzi chake katika familia yake duniani kisha akasubiri (malipo mazuri) zaidi ya pepo".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Nabii -Ziwe juu yake Amani- katika hadithil Qudsiy hii, kuwa yeyote atakayetahiniwa kwa kumkosa kipenzi chake miongoni mwa ndugu wa karibu au yeyote, atakaposubiri mwanadamu juu ya kuondokewa na yule aliyemteua na kumchagua na akaona kua huyu ndiye mwenye mahusiano mazuri na yeye, kama mtoto, au baba mdogo, au baba, au mama, au rafiki, anapomchukua Mwenyezi Mungu Mtukufu kisha mwanadamu akataraji malipo basi hana malipo mengine zaidi ya pepo.

Marejeo

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي، ط1، دار ابن الجوزي، الدمام، 1415هـ. رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ. رياض الصالحين، ط4، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، 1428هـ. كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين برئاسة حمد بن ناصر العمار، ط1، كنوز إشبيليا، الرياض، 1430هـ. شرح رياض الصالحين، للشيخ ابن عثيمين، دار الوطن للنشر، الرياض، 1426هـ. صحيح البخاري، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر، ط1، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu

عَنْ ثَوْبَانَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَفْضَلُ دِينَارٍ يُنْفِقُهُ الرَّجُلُ، دِينَارٌ يُنْفِقُهُ عَلَى عِيَالِهِ، وَدِينَارٌ يُنْفِقُهُ الرَّجُلُ عَلَى دَابَّتِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ، وَدِينَارٌ يُنْفِقُهُ عَلَى أَصْحَابِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ» قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: وَبَدَأَ بِالْعِيَالِ، ثُمَّ قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: وَأَيُّ رَجُلٍ أَعْظَمُ أَجْرًا مِنْ رَجُلٍ يُنْفِقُ عَلَى عِيَالٍ صِغَارٍ، يُعِفُّهُمْ أَوْ يَنْفَعُهُمُ اللهُ بِهِ وَيُغْنِيهِمْ.
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aina za matumizi, na akazipanga pale panapokuwa na namna nyingi za kutoa matumizi kulingana na kile ambacho ni wajibu zaidi kwako, hivyo alianza na muhimu zaidi na kisha muhimu zaidi. Akaeleza kuwa mali yenye malipo mengi ni ile anayoitoa muislamu kwa wale anaolazimika kuwahudumia; kwanzia mkewe na watoto, kisha kutoa katika kipando kilichoandaliwa kwa ajili vita katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha kuwahudumia jamaa zake na rafiki zake wanapokuwa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Mpangilio wa matumizi katika ubora ni kwa namna ulivyotajwa, lizingatiwe hilo panapokuwa na majukumu mengi.
  2. Kumebainishwa umuhimu wa kuanza na familia katika kutoa matumizi, na ndiko kuna fadhila nyingi kuliko kutoa sehemu zingine.
  3. Kuhudumia Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni katika kutoa kukubwa, kama kuandaa vifaa na watu kwa ajili ya Jihadi.
  4. Inasemekana kuwa: Makusudio ya njia ya Mwenyezi Mungu ni kila jambo la ibada, mfano kama Hija.
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 691) (994). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 315). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 156). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 291). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 374).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قُبُورًا، وَلَا تَجْعَلُوا قَبْرِي عِيدًا، وَصَلُّوا عَلَيَّ؛ فَإِنَّ صَلَاتَكُمْ تَبْلُغُنِي حَيْثُ كُنْتُمْ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kubaki tupu bila ibada ya swala ndani yake, yakawa kama makaburi ambayo hayaswaliwi ndani yake, Na akakataza kurudi mara kwa mara kutembelea kaburi lake na kukusanyika hapo kwa namna ya mazoea; kwani hilo ni njia ya kuelekea katika ushirikina, Na akaamrisha kumtakia rehema na amani juu yake mahala popote katika uso wa ardhi; kwani dua hizo humfikia kutoka kwa aliyekaribu na aliyembali kwa kiwango sawa, haina haja ya kurudi mara kwa mara katika kaburi lake.

Mafunzo
  1. Katazo la kuziacha nyumba bila ya kumuabudia Allah Mtukufu ndani ya majumba hayo.
  2. Katazo la kufunga safari kwa ajili ya kuzuru kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwani yeye aliamrisha kumuombea rehema juu yake na akaeleza kuwa zinamfikia, bali hufungwa safari kwa kuukusudia msikiti pekee na kusali ndani yake.
  3. Uharamu wa kulifanyia matembezi kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni sikukuu, kwa kukithirisha kulizuru kwa namna maalum na kwa nyakati maalum, na vile vile ziara ya kaburi lolote.
  4. Utukufu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Mola wake, kwa kuwekwa sheria ya kumtakia rehema kwa kila zama na kila mahali.
  5. Kiasi kwamba katazo la kuswali makaburini limepitishwa kwa maswahaba; kwa ajili hii alikataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- majumba kufanywa kuwa kama makaburi hakusaliwi ndani yake.
Marejeo

سنن أبي داود (3/ 385) (2042). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص202). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص185).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ عَالَ جَارِيَتَيْنِ حَتَّى تَبْلُغَا جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَنَا وَهُوَ» وَضَمَّ أَصَابِعَهُ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeruzukiwa mabinti wawili au dada wawili, akawasimamia katika mahitaji na malezi na kuwaelekeza katika kheri na kuwatahadharisha na shari na mfano wa hayo mpaka wakakua na kubalehe; atakuja siku ya Kiyama akiwa yeye na Mtume rehema na amani ziwe juu yake mfano wa hivi viwili, akaunganisha vidole vyake viwili, kidole cha shahada na cha kati.

Mafunzo
  1. Thawabu kubwa kwa atakayewasimamia watoto wa kike kwa mahitaji na malezi mpaka watakapoolewa au kuvunja uongo, hivyo hivyo hata dada.
  2. Malipo ya kuwasimamia watoto wa kike ni makubwa kuliko malipo ya kuwasimamia watoto wa kiume; kwa sababu hayakutajwa malipo kama hayo katika haki za watoto wa kiume; na hii ni kwa sababu mahitajio ya watoto wa kike na kuwapa kipaumbele ni jambo kubwa kuliko mambo ya watoto wa kiume; kwa sababu ni sawa na wako tupu, mambo yao mengi hawawezi kuyafanya wenyewe, na wala hawawezi kufanya harakati kama za watoto wa kiume, na ni kwa sababu wao huhitaji zaidi nguvu ya baba katika kupambana na maadui na kuhuisha jina lake na kuunga nasaba yake, na mengineyo, kama wanavyofanya kwa wanaume; ikahitajika subira na ikhlasi katika hilo kwa huyu mtoaji ikiwa pamoja na kusafisha nia; akayafanya malipo kuwa makubwa, akawa rafiki wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Kiyama.
  3. Alama za mwanamke kuvunja ungo: Kufikisha miaka kumi na tano, au akaingia katika hedhi hata kama hajafikisha miaka kumi na tano, au akaota nywele sehemu za siri, nazo ni nywele zinazoizunguka tupu ya mbele, au kwa kujiotea, nako ni kushusha manii usingizini.
  4. Amesema Al-Qurtubi: Na anakusudia kubalehe kwake ni kufikia kwao hali ya kujitegemea wenyewe; na hii kwa wanawake inakuwa kwa kuingiliwa na waume zao, haimaanishi kuvunja ungo kwa kuingia katika hedhi na kuanza kutekeleza wajibu; kwani anaweza kuolewa hata kabla ya hapo, akatosheka na mume wake katika kusimamiwa mahitaji yote, na anaweza kuingia katika hedhi na bado hajajitegemea kwa chochote katika masilahi yake, na lau akiachwa atapotea na hali yake kuharibika, bali anapofikia hali hii ndio anakuwa na haki zaidi ya kulindwa na kuhifadhiwa na kusimamiwa ili ukamilike ulinzi wake na ili ajiandae kumuozesha, na kwa maana hii wamesema wanachuoni wetu, haziondolewi huduma kwa mzazi wa binti kwa sababu ya kuvunja kwake ungo bali zitaondoka kwa kuingiliwa na mume wake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2027) (2631). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 352). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص198). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 144). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 105). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 276).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بِن مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ العَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الوَالِدَيْنِ» قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ» قَالَ: حَدَّثَنِي بِهِنَّ، وَلَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِي.
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu" Akasema: Alinihadithia mambo hayo, na lau ningemtaka ziada angenizidishia.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliulizwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu?. Akasema: Ni swala za faradhi katika wakati wake uliopangwa na sheria, Kisha wema kwa wazazi wawili, kwa kuwafanyia wema, na kusimamia haki zao, na kuacha kuwaasi, kisha Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuitetea dini ya Uislamu na waislamu, na kudhihirisha alama zake, na hii inakuwa kwa nafsi na mali. Akasema bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake: Alinieleza amali hizi; na lau kama ningelimwambia: Kisha ipi? Basi angenizidishia.

Mafunzo
  1. Kuzidiana kwa amali kati yake ni kulingana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa amali hiyo.
  2. Himizo kwa muislamu katika kupupia amali bora kisha inayofuata kwa ubora.
  3. Kutofautiana kwa majibu ya Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhusu amali bora kulingana na watu na hali zao, na kulingana na lenye manufaa mengi kwa kila mmoja miongoni mwao.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 112) (527). صحيح مسلم (1/ 90) (85). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 70). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص84). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 108).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake?

عن ابن شماسة المهري قال: حَضَرنَا عَمرو بن العاص رضي الله عنه وهُو فِي سِيَاقَةِ الْمَوتِ، فَبَكَى طَوِيلاً، وَحَوَّلَ وَجهَهُ إِلَى الجِدَارِ، فَجَعَلَ ابنَهُ، يقول: يَا أَبَتَاهُ، أَمَا بَشَّرَكَ رسُول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- بكَذَا؟ أمَا بشَّركَ رسول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- بِكَذَا؟ فَأَقبَلَ بِوَجهِهِ، فقَالَ: إِنَّ أَفضَلَ مَا نُعِدُّ شَهَادَةُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ الله، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رسولُ الله، إِنِّي قَدْ كُنتُ عَلَى أَطْبَاقٍ ثَلاَثٍ: لَقَدْ رَأَيتُنِي وَمَا أَحَدٌ أَشَدَّ بُغْضًا لِرَسُولِ الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- مِنِّي، وَلاَ أَحَبَّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَكُونَ قَدْ اسْتَمْكَنْتُ مِنْهُ فَقَتَلْتُهُ، فَلَوْ مُتُّ عَلَى تِلْكَ الحَالِ لَكُنْتُ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، فَلَمَّا جَعَلَ اللهُ الإِسْلاَمَ فِي قَلْبِي أَتَيتُ النَبيَّ -صلَّى الله عليه وسلَّم-، فَقُلتُ: ابْسُطْ يَمِينَكَ فَلِأُبَايِعُكَ، فَبَسَطَ يَمِينَهُ فَقَبَضْتُ يَدِي، فقال: «مَا لَكَ يَا عَمرُو؟» قُلتُ: أَرَدْتُ أَنْ أَشْتَرِطَ، قال: «تَشْتَرِطُ مَاذَا؟» قُلتُ: أَنْ يُغْفَرَ لِي، قال: «أَمَا عَلِمتَ أَنَّ الإِسْلاَمَ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ، وَأَنَّ الهِجْرَةَ تَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهَا، وَأَنَّ الحَجَّ يَهْدِمُ مَا كَانَ قَبْلَهُ؟» وَمَا كَان أَحَدٌ أَحبَّ إِلَيَّ مِنْ رسُول الله -صلَّى الله عليه وسلَّم- وَلاَ أَجَلَّ فِي عَينِي مِنْهُ، وَمَا كُنْتُ أُطِيقُ أَنْ أَمْلَأَ عَينِي مِنْهُ؛ إِجْلاَلاً لَهُ، وَلَوْ سُئِلْتُ أَنْ أَصِفَهُ مَا أَطَقْتُ؛ لِأَنِّي لَمْ أَكُنْ أَمْلَأُ عَينِي مِنْهُ، وَلَوْ مِتُّ عَلَى تِلْكَ الحَالِ لَرَجَوْتُ أَنْ أَكُونَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، ثُمَّ وَلِينَا أَشْيَاءَ مَا أَدْرِي مَا حَالِي فِيهَا؟ فَإِذَا أَنَا مِتُّ فَلاَ تَصْحَبْنِي نَائِحَةٌ وَلاَ نَارٌ، فَإِذَا دَفَنْتُمُونِي، فَشُنُّوا عَلَيَّ التُرَابَ شَنًّا، ثُمَّ أَقِيمُوا حَولَ قَبرِي قَدْرَ مَا تُنْحَرُ جَزُور، وَيُقْسَمُ لَحْمُهَا، حتَّى أَسْتَأْنِسَ بِكُم، وَأَنْظُر مَا أُرَاجِعُ بِهِ رُسُلَ رَبِّي.
Kutoka kwa bin Shammasa Al Mihriy Amesema:Tulifika kwa Amru bin Aaswi naye akiwa katika safari ya kifo, akalia kwa muda mrefu, na akageuza uso wake kuelekea ukutani, mwanaye akaanza kusema, Ewe baba yangu, kwani hakukubashiria Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake kwa jambo kadhaa (yaani pepo)? kwani hakukubashiria Mtume-Rehema na Amani ziwe juu yake kwa jambo kadhaa? akageuka kwa uso wake, kisha akasema: Hakika jambo bora katika yale tunayoyaandaa ni kushuhudia kuwa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hakika mimi nilikuwa katika hali za aina tatu: Nilijikuta mimi kuwa hakuna anayemchukia kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuliko mimi, Na hakuna kitu nilichotamani zaidi kama kumtia mikononi ili nimuue, basi lau ningekufa katika hali hiyo ningekuwa ni katika watu wa motoni, Basi Mwenyezi Mungu alipouweka Uislamu moyoni mwangu, nilimuendea Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Kisha nikasema: Nyoosha mkono wako wa kulia ili nikupe utiifu wangu kwako, basi akanyoosha mkono wake wa kulia nikakunja mkono wangu, akasema: "Umekuwaje wewe Amru?" Nikasema: Nilitaka niweke sharti kwanza, akasema: "Unaweka sharti la kitu gani?" Nikasema: Nisamehewe, akasema: "Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta makosa yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta makosa yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija hufuta makosa yaliyokuwa kabla yake?" Kuanzia hapo hapakuwa tena na yeyote niliyempenda zaidi kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- wala niliyemuheshimu zaidi machoni mwangu kuliko yeye, Na sikuwa naweza kumtazama kwa macho yangu; kwasababu ya kumuheshimu, na hata kama ningeombwa nimsifie nisingeweza; kwasababu mimi sikuwa naweza kumtazama kwa macho yangu, na lau ningekufa katika hali hiyo ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, Kisha tukatawala mambo ambayo mpaka sasa sijui hali yangu ndani yake? Basi ikiwa nitakufa nisifuatwe na maombolezo wala moto, na mkinizika, basi nimwagieni udongo kidogo kidogo, kisha bakini kaburini kwangu kwa kiasi cha muda wa kuweza kumchinja ngamia na kumchuna, na kugawanywa nyama yake, ili nijiliwaze kwenu, na nisubiri nini nitawajibu wajumbe wa Mola wangu.
Imepokelewa na Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Imekusanya hadithi ya Amru bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- maudhui za habari njema na pongezi za kheri ndani ya kisa, na muhtasari wa kisa hiki kitukufu: Nikuwa yeye walimfikia baadhi ya jamaa zake naye akiwa katika safari ya kifo, akalia kilio kikubwa, na akageuza uso wake upande wa ukutani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, naye akiwa katika safari ya kifo ataachana na dunia, mwanaye akasema kumwambia: Unalilia nini na haliyakuwa tayari alishakubashiria pepo Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-? Akasema: Ewe mwanangu, hakika mimi nilikuwa katika hali tatu, kisha akazitaja hali hizi tatu: Yakuwa yeye alikuwa akimchukia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chuki ya hali ya juu, nakuwa duniani hapakuwa na mtu anayemchukia zaidi kama yeye, mpaka Mwenyezi Mungu akauingiza Uislamu ndani ya moyo wake akaja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, akasema: Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Nyoosha mkono wako ili nikupe utiifu wangu juu ya uislamu, na alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni mwenye tabia nzuri kuliko watu wote akanyoosha mkono wake, lakini Amri bin Aaswi akakunja mkono wake, si kwasababu ya kiburi, lakini ni kwasababu ya kuyathibitisha yale atakayoyaeleza, akasema kumwambia: "Umekuaje?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika mimi ninaweka sharti -yaani juu ya kusilimu- Akasema: "Ni kitu gani unaweka sharti?" Akasema: Ninaweka sharti kuwa anisamehe Mwenyezi Mungu mimi yaliyopita katika ukafiri miongoni mwa madhambi. Hii ndio ilikuwa hamu yake kubwa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Anaweka sharti kuwa Mwenyezi Mungu amsamehe, alidhani kuwa Mwenyezi Mungu hatomsamehe katika yale aliyokuwa nayo nyuma, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akasema kumwambia-: "Hivi hukujua kuwa uislamu unabomoa(unafuta) yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunabomoa yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inabomoa yaliyokuwa kabla yake?". Mambo matatu. Ama Uislamu unabomoa yaliyokuwa kabla yake kwa ushahidi wa kitabu kitukufu: Amesema Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka: "Waambie wale waliokufuru: "kama wataacha (yale mabaya waliyokuwa nayo) watasamehewa yaliyopita, na wakiyarudia (tutawatesa kama tulivyo watesa wao mara zilizopita) Imekwisha kuwapitia wao mifano (ya mambo yaliyowapata) watu wa zamani". Na kuhama: atakapohama mtu kutoka katika mji wake ambao anaishi ndani yake, na katika mji wa kikafiri hilo linafuta yaliyokuwa kabla yake. Na hija: inabomoa yaliyokuwa kabla yake; kwa kauli ya Mtume- Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakayehiji akawa hakufanya mabaya na akawa hakufanya machafu atarudi kama siku alivyozaliwa na mama yake". Hapo akampa utiifu -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akampenda Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- mapenzi makubwa mpaka akawa ni mtu anayependeka zaidi kwake, na mpaka akawa hawezi kumkazia jicho; kwa kumuheshimu yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ametakasika mwenye kuzigeuza nyoyo! jana alikuwa akimchukia chuki kubwa mpaka anatamani apate nafasi ili amuuwe, na sasa hivi hawezi hata kunyanyua jicho lake kumtazama; kwasababu ya kumuheshimu, na wala hawezi hata kumuelezea kwasababu hawezi kumtazama akamaliza, kiasi ambacho hakuweza kumjua vizuri; kwasababu ya mapenzi yake kwake -Rehema na Amani ziwe juu yake- Anasema -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-. Laiti angelikufa katika hali ya kwanza; basi angelikuwa ni katika watu wa motoni: Anasema: Na lau ningelikufa katika hali ile yaani hali ya pili; ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, hebu tazama alivyojipa uwezekano, amejihakikishia kuwa laiti angelikufa katika hali ya kwanza; angelikuwa miongoni mwa watu wa motoni, Ama hali ya pili kutokana na hofu yake kubwa amesema: Laiti ningelikufa katika hali hii basi ningetaraji kuwa miongoni mwa watu wa peponi, na hakusema: Ningekuwa ni miongoni mwa watu wa pepo; kwasababu ushuhuda wa kuingia peponi ni jambo gumu. Kisha yeye baada ya hapo akasimamia mambo -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, alisimamia madaraka na uongozi, na yakatokea yaliyotokea katika kisa cha vita vya Muawiya na wengineo, na Amru bin Aaswi alikuwa anafahamika kwa waarabu kuwa ni katika waarabu wajanja na werevu mno, basi anasema: ninahofia kwa haya yaliyotokea kwangu baada ya ile hali ya katikati huenda yakawa yameyazingira matendo yangu. Kisha akatoa usia -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye atakapokufa asifuatwe na maombolezo, na muombolezaji: Ni mwanamke anayemuomboleza maiti, na analia kilio kinachofanana na mlio wa punda, na akaamrisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- watakapomzika wabakie katika kaburi lake kiasi cha kuchinja ngamia mmoja, na kugawika nyama yake, mpaka awajibu wajumbe wa Mola wake nao ni Malaika wale wanaomjia maiti anapozikwa, Maiti anapozikwa humjia Malaika wawili na wanamkalisha ndani ya kaburi lake, na wanamuuliza maswali matatu: wanasema: Nani Mola wako? Na ni ipi dini yako? Na ni nani Nabii wako?. Akaamrisha Amru bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- watu wake wasimame juu yake kiasi cha kuchinjwa ngamia na kugawanywa nyama yake; ili ajiliwaze kupitia wao, Na hii inaonyesha kuwa maiti huwa anawahisi watu wake, na imethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa maiti husikia nyayo za viatu vyao, wanapoondoka baada ya kumzika, nyayo za viatu za kimya kimya anazisikia maiti wanapoondoka baada ya kumzika. Na imethibiti kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi ambayo daraja yake ni (Hasan) kuwa yeye alikuwa anapomzika maiti anasimama juu yake, na Anasema: "Muombeeni msamaha ndugu yenu, na muombeeni kuthubutu; kwani yeye wakati huu anaulizwa", Hivyo ni sunna na inapendeza anapozikwa maiti mtu asimame juu ya kaburi lake na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu mpe uthubutu (umakinifu), Ewe Mwenyezi Mungu msamehe; kwasababu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa anapotoa salamu basi anatoa salamu mara tatu, na anapoomba anaomba mara tatu. Kilichopo nikuwa mtoto wa Amru bin Aaswi alisema kumwambia: Alikupa habari njema wewe Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ya kuingia peponi, na hii ni sehemu ya kujipa bishara njema na kujipongeza kwayo.

Marejeo

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي، الدمام، الطبعة: الأولى 1415هـ. تطريز رياض الصالحين، فيصل بن عبد العزيز المبارك، تحقيق: عبد العزيز بن عبد الله آل حمد، دار العاصمة للنشر والتوزيع، الرياض، الطبعة: الأولى 1423هـ، 2002م. رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين، أبو زكريا محيي الدين النووي، تحقيق ماهر الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، الطبعة: الأولى 1428هـ. شرح رياض الصالحين، محمد بن صالح العثيمين، مدار الوطن، الرياض، 1426هـ. صحيح البخاري، محمد بن إسماعيل البخاري الجعفي، تحقيق: محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى 1422هـ. صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، الطبعة: 1423هـ. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة: الرابعة عشر 1407هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 20
Hadithi 20
  1. Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake
  2. Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya
  3. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Hana mja wangu muumini toka kwangu malipo yoyote pindi ninapomchukua kipenzi chake katika familia yake duniani kisha akasubiri (malipo mazuri) zaidi ya pepo
  4. Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu
  5. Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, na wala msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, na nitakieni rehema, kwani dua zenu hunifikia mahala popote muwapo
  6. Atakaye walea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya Kiyama mimi na yeye (Namna hii)" Na akaviunganisha vidole vyake viwili
  7. Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu
  8. Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake?
  9. Mcheni na Allah Mola wenu Mlezi, na salini swala zenu tano, na fungeni mwezi wenu, na tekelezeni zaka zenu, na mtiini mwenye mamlaka kwenu, (Mkiyafanya haya) mtaingia pepo ya Mola wenu
  10. Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?
  11. Swala tano, na ijumaa mpaka ijumaa, na Ramadhani hadi Ramadhani, hufuta madhambi yaliyo kati yake, ikiwa mtu atayaepuka madhambi makubwa
  12. Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha
  13. Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu
  14. Kila wema ni sadaka
  15. Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake
  16. Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani
  17. Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana
  18. Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake
  19. Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala
  20. Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com