Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «رُبَّ أَشْعَثَ مَدْفُوعٍ بِالْأَبْوَابِ لَوْ أَقْسَمَ عَلَى اللهِ لَأَبَرَّهُ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Huenda mwenye nywele timtimu mwenye kusukumwa katika milango, lau angeliapia kwa Mwenyezi Mungu angelimuepusha".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kuna baadhi ya watu wana nywele zilizoshikana tena zilizojaa vumbi, na hawazipaki mafuta wala hajali kuziosha, na wala hawana heshima yoyote mbele za watu, basi watu humsukuma mtu kama huyu katika milango yao, na kumfukuza kwa kumdharau; isipokuwa mtu huyu lau angeapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa litokee jambo basi Mwenyezi Mungu angelitenda jambo hilo kwa sababu ya kumkirimu na kumtukuza kwa kujibu ombi lake, na kumlinda asijekupotoka katika kiapo chake, na hii ni kwa sababu ya ubora wake na nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Mwenyezi Mungu hatazami sura ya mja, lakini anatazama ndani ya nyoyo na matendo.
  2. Ni jukumu la kila mtu kuyapa kipaumbele matendo yake na usafi wa moyo wake zaidi kuliko kuutilia maanani mwili wake na mavazi yake.
  3. Kujinyenyekeza kwa Mwenyezi Mungu na kujidhalilisha kwake ni sababu ya kujibiwa dua, na ndiyo maana; Mwenyezi Mungu hukiepusha kuanguka patupu kiapo cha wachamungu na wenye maisha duni.
  4. Kumebainishwa malezi ya kiutume kwa watu; ili wasidharauliane wao kwa wao.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2024) (2622). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 48). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 344). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (1/ 268) شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 63).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora na fadhila za matendo mema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com