Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu

عَنْ مَعْقِلِ بْنِ يَسَارٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الْعِبَادَةُ فِي الْهَرْجِ كَهِجْرَةٍ إِلَيَّ».
Kutoka kwa Ma'qal bin Yasari -radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati za vurugu na fitina na mauaji na kuparaganyika kwa mambo ya watu katika ibada na kushikamana nayo, na kwamba malipo yake ni kama kuhama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni kwa sababu watu hughafilika nayo, na hawatengi muda ila mtu mmoja mmoja.

Mafunzo
  1. Himizo la kufanya ibada na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu nyakati za fitina; kwa ajili ya kujilinda na fitina, na kujihifadhi na ufisadi.
  2. Kumebainishwa fadhila za kufanya ibada nyakati za fitina na nyakati za watu kughafilika.
  3. Inapaswa kwa muislamu ajitenge mbali na mazingira ya fitina na kughafilika.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2268) (2948). كشف المشكل من حديث الصحيحين (2/ 42). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (45/ 5). بهجة الناظرين (2/ 455). نزهة المتقين (ص942).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora na fadhila za matendo mema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com