عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «كُلُّ مَعْرُوفٍ صَدَقَةٌ».
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kila wema ni sadaka"
Imepokelewa na Bukhari kutokana na hadithi ya Jaabir, na amepokea Muslim kutokana na hadithi ya HudhaifaDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa kila wema na kuwanufaisha wengine kuanzia kauli au matendo huwa ni sadaka, na kuna malipo na thawabu.
Mafunzo
- Nikuwa sadaka haishii tu katika vile anavyovitoa mtu katika mali yake, bali inajumuisha kila kheri anayoifanya mwanadamu au kuitamka na kuifikisha kwa wengine.
- Hapa kuna himizo la kutenda wema, na kila jambo lenye manufaa kwa wengine.
- Kutodharau kitu katika wema, hata kama ni kidogo.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 11) (6021). صحيح مسلم (2/ 697) (1005). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 117). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 341).