Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake

عن أنس بن مالك رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ أَحَبَّ أَنْ يُبْسَطَ لَهُ فِي رِزْقِهِ، وَيُنْسَأَ لَهُ فِي أَثَرِهِ، فَلْيَصِلْ رَحِمَهُ».
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kuwaunga ndugu wa karibu kwa kuwatembelea na takrima za mwili na mali na mengineyo, nakuwa kufanya hilo ni sababu ya kukunjuliwa riziki, na kupewa umri mrefu.

Mafunzo
  1. Ndugu wa karibu ni wale wa upande wa baba na mama, na kadiri anavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo anavyokuwa bora zaidi kwa kuungwa udugu.
  2. Malipo huendana na matendo, atakayeunga udugu wake kwa wema na ihisani, naye pia Mwenyezi Mungu atamuunga katika umri wake na riziki yake.
  3. Kuunga udugu ni sababu ya kukunjuliwa riziki na kupanuliwa kwake, na ni sababu ya umri mrefu, hata kama kifo na riziki vina muda maalum isipokuwa hili linaweza kuwa ni baraka katika riziki na umri, akafanya mengi katika umri wake na yenye manufaa zaidi kuliko atakavyofanya mwingine, na wanasema wanachuoni; ziada katika riziki na umri ni zaida ya uhalisia. Na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 5) (5986). صحيح مسلم (4/ 1982) (2557). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 320). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 188). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 275). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص224). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 81).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora na fadhila za matendo mema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com