Ameeleeza mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba mwanamke moja masikini alimjia akiwa kawabeba watoto wake wa kike wawili, akamuomba chakula, akampatia tende tatu, akampatia kila mmoja miongoni mwa mabinti zake tende moja ili ale, watoto wake wakaihitaji tende ile mmoja aliyotaka kuila, akawakatia tende ile vipande viwili, jambo hilo likamshanga mno Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akakieleza kitendo alichokifanya mwanamke yule kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika Mwenyezi Mungu kamuwajibishia Pepo kwa tende hii, au kamuacha huru na Moto.
- Fadhila ya sadaka hata kama ikiwa ndogo, nayo inaonyesha ukweli wa Muumini katika imani yake kwa Mola wake Mlezi na uaminifu wake kwa ahadi yake na fadhila zake.
- Ukubwa wa huruma ya akina mama kwa watoto, na hofu yao juu ya kuwapoteza.
- Fadhila za kuidhiki nafsi kwa kuwapendelea wengine, na kuwahurumia wadogo, na ziada ya wema na upole kwa watoto wa kike, na kwamba hilo ni sababu ya kuingia Peponi, na kuachwa huru na Moto.
- Kitu kidogo hakizuiliwi kutolewa sadaka kwa sababu ya kubezwa kwake, bali ni wajibu kwa amtoaji sadaka atoe sadaka kwa kiasi anachokiweza kiwe kidogo au kikubwa.
- Hapa kumeelezwa hali zilivyokuwa nyumba za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na vipi yalikuwa maisha yake na familia yake, kiasi kwamba hapakuwa na chochote cha kuliwa ndani ya nyumba zao, zaidi ya tende moja au tatu.
صحيح مسلم (4/ 2027) (2630). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص199). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 111). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 278).