Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «رِبَاطُ يَوْمٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ مِنَ الجَنَّةِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَالرَّوْحَةُ يَرُوحُهَا العَبْدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوِ الغَدْوَةُ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kubakia katika eneo ambalo liko kati ya waislamu na makafiri kwa ajili ya kuwalinda dhidi yao kwa siku moja, kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba mahali pa kuweka mjeledi unaotumika kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba malipo na thawabu za kutembea katika wakati wa mwanzo wa mchana mpaka mwanzo wa wakati wa adhuhuri, au mchana: Ni kwanzia adhuhuri mpaka usiku katika njia ya Mwenyezi Mungu mara moja, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.

Mafunzo
  1. Fadhila za kuthubutu katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya hatari zilizomo zinazoihatarisha nafsi, na kwa yale yanayofungamana nalo kama kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuitetea dini yake, kwa hivyo, thawabu za siku moja pekee, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  2. Udhalili wa dunia ukiilinganisha na akhera; kwa sababu sehemu ya kuweka mjeledi pekee peponi, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  3. Ubora wa kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ukubwa wa thawabu zake; kwa sababu thawabu za mwendo mmoja wa asubuhi au mchana, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  4. Kauli yake: "Katika njia ya Mwenyezi Mungu" hapa kuna dalili ya umuhimu wa kutakasa nia, na kwamba malipo yanaambatana na hilo.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 35) (2892). صحيح مسلم (3/ 1500) (1881). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص739).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora na fadhila za matendo mema.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com