Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Matendo ya moyoni.

Hadithi 22

Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?”

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ السَّاعَةِ، فَقَالَ: مَتَى السَّاعَةُ؟ قَالَ: «وَمَاذَا أَعْدَدْتَ لَهَا». قَالَ: لاَ شَيْءَ، إِلَّا أَنِّي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ». قَالَ أَنَسٌ: فَمَا فَرِحْنَا بِشَيْءٍ، فَرِحْنَا بِقَوْلِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ» قَالَ أَنَسٌ: فَأَنَا أُحِبُّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَبَا بَكْرٍ، وَعُمَرَ، وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ مَعَهُمْ بِحُبِّي إِيَّاهُمْ، وَإِنْ لَمْ أَعْمَلْ بِمِثْلِ أَعْمَالِهِمْ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?” Akasema: Hapana, isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Hakuna lililotufurahisha zaidi ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Mimi ninampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na ninataraji kuwa pamoja nao kutokana na mapenzi yangu kwao, hata kama nisipofanya sawa na matendo yao.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Bedui mmoja anayeishi jangwani alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Je, saa ya Kiyama itatokea wakati gani? Basi rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Umeiandalia mambo gani mema? Akasema muulizaji: Sikutayarisha jambo kubwa kwa ajili yake isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wala hakutaja ibada nyinginezo za moyo, za kimwili, au za kifedha. Kwa sababu zote ni matawi ya upendo unaotokana na hayo, na kwa sababu upendo wa dhati humsukuma mtu kujitahidi kufanya matendo mema. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Wewe utakuwa pamoja na unayempenda peponi. Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakafurahishwa sana na habari hii njema. Kisha Anas radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakika anampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na anatarajia kuwa pamoja nao, hata kama amali zake si kama amali zao.

Mafunzo
  1. Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kumjibu muulizaji, kwani alimuongoza katika yale yanayomhusu na kumuokoa, nayo ni: kujiandaa na Akhera kwa yenye manufaa na matendo mema.
  2. Mwenyezi Mungu ameficha kwa waja wake elimu ya kujua Kiyama, ili mtu aendelee kuwa tayari na kujiandaa kukutana na Mwenyezi Mungu.
  3. Fadhila za kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na watu wema miongoni mwa waumini, na onyo la kuwapenda washirikina.
  4. Kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: Wewe utakuwa pamoja na umpendaye. Kinachokusudiwa sio usawa wa daraja na hadhi, bali ni kuwa, wao watakuwa Peponi kiasi kwamba kila mmoja wao ataweza kumuona mwenzake, hata kama sehemu hiyo iko mbali.
  5. Kumuelekeza Muislamu kuzingatia yale yaliyo bora na yenye manufaa kwake, na kuacha kuuliza juu ya yale ambayo hayamnufaishi.
Marejeo

صحيح البخاري (5/ 12) (3688). صحيح مسلم (4/ 2032) (2639). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 435). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 177). المعجم الأوسط، للطبراني (1/ 131). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 342).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ: «يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، آمَنَّا بِكَ وَبِمَا جِئْتَ بِهِ فَهَلْ تَخَافُ عَلَيْنَا؟ قَالَ: «نَعَمْ، إِنَّ القُلُوبَ بَيْنَ أُصْبُعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ اللهِ يُقَلِّبُهَا كَيْفَ يَشَاءُ».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Dua nyingi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu uthabiti katika dini na utiifu, na kujiepusha na kupinda na upotofu. Anas bin Malik radhi za Allah ziwe juu yake alistaajabu kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiiomba dua hii mara kwa mara, basi Mtume rehema na amani zimshukie akamwambia kuwa nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, huzigeuza apendavyo, hivyo, moyo ni kituo cha imani na ukafiri, na moyo umeitwa Qalbu kwa sababu ya kugeukageuka kwake mara kwa mara, moyo hugeuka sana kuliko chungu kinapokusanyika kile kinachotokota ndani yake. Amtakaye Mwenyezi Mungu huudumisha moyo wake katika uongofu na uthabiti katika Dini, na anayemtaka Mwenyezi Mungu huugeuza moyo wake kutoka katika uongofu na kuupeleka katika upotofu.

Mafunzo
  1. Kujisalimisha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na kunyenyekea kwake, na kuuelekeza umma kuliomba hilo.
  2. Umuhimu wa kuwa na msimamo na uthabiti katika dini, na kuwa kinachozingatiwa ni hatima ya mtu ya maisha yake.
  3. Mja hawezi kujitosheleza mwenyewe hata kwa kupepesa jicho bila ya kutiwa uthabiti na Mwenyezi Mungu katika Uislamu.
  4. Himizo la kuomba dua hii kwa wingi, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  5. Kudumu katika Uislamu ni neema kubwa ambayo mja anatakiwa kuifanyia juhudi na kumshukuru Mola wake Mlezi.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 19) (2140). مسند أحمد (19/ 160) (12107). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 476). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 567). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1014). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص808). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 41).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake

عَن سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ سَأَلَ اللهَ الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ، وَإِنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ».
Kutoka kwa Sahali bin Hunaif radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeomba shahada na kuuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawa mkweli na mwenye ikhlasi katika nia yake hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu atamjaalia kupata daraja za mashahidi kwa nia yake ya kweli, hata akifa kitandani katika hali isiyokuwa jihadi.

Mafunzo
  1. Nia ya dhati na kufanya linalowezekana ni sababu ya kupata thawabu na malipo yaliyokusudiwa, hata kama amali inayotakiwa haijatekelezwa.
  2. Himizo la jihadi na kuomba shahada katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa umma huu, kwani anaupa kupitia amali ndogo daraja za juu zaidi peponi.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1517) (1909). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 123). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 87).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Je nisikuelezeni kwa kile ambacho ninakiogopea zaidi kwenu nyinyi kuliko hata masihi dajali? Wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anapendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama

عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه مرفوعاً: "ألا أخبركم بما هو أَخْوَفُ عليكم عندي من المسيح الدجال؟ قالوا: بلى يا رسول الله، قال: الشرك الخفي يقوم الرجل فيصلي فَيُزَيِّنُ صلاته لما يرَى من نَظَرِ رَجُلٍ".
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Je nisikuelezeni kwa kile ambacho ninakiogopea zaidi kwenu nyinyi kuliko hata masihi dajali? Wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anapendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama".
Imepokelewa na Ibnu MaajahDarajaNi nzuri
Maelezo

Walikuwa maswahaba wakikumbushana fitina ya masihi dajali na wakiogopeshana juu yake, akawaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa kuna jambo la haramu analowaogopea kuliko hata hofu ya fitina ya masihi dajali, nayo ni shirki katika nia na makusudio ambayo haionekani kwa watu, kisha akalifasiri hilo kwa kuyafanya vizuri matendo ambayo hutafutiwa kwayo radhi za Mwenyezi Mungu kwaajili ya kuwaonyesha watu.

Marejeo

فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، مطبعة السنة المحمدية، القاهرة، مصر، الطبعة: السابعة، 1377هـ - 1957م. القول المفيد على كتاب التوحيد، دار ابن الجوزي، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الثانية، 1424هـ. الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة الرياض، الطبعة: الأولى، 1422هـ - 2001م. الجديد في شرح كتاب التوحيد، مكتبة السوادي، جدة، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م. التمهيد لشرح كتاب التوحيد، دار التوحيد، تاريخ النشر: 1424هـ. سنن ابن ماجه، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء الكتب العربية - فيصل عيسى البابي الحلبي. صحيح الجامع، طبعة المكتب الإسلامي.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «قَالَ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ، مَنْ عَمِلَ عَمَلًا أَشْرَكَ فِيهِ مَعِي غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ».
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa: Yeye amejitosheleza na uhitaji wa washirika wa kushirikishwa naye, Yeye ni tajiri wa kila kitu, na kuwa mwanadamu atakapofanya jambo katika ibada na akalifanya kuwa ni la Mwenyezi Mungu na mwingine asiyekuwa yeye, basi Allah humuacha na halikubali jambo hilo, na hulirejesha kwa mwenye nalo. Ni lazima kutakasa amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Yeye Mtukufu hakubali isipokuwa yale yatakayokuwa yametakaswa kwa kutaka radhi zake Yeye Mkarimu.

Mafunzo
  1. Tahadhari ya ushirikina kwa aina zake zote; nakuwa ushirikina huzuia kukubaliwa amali.
  2. Kuleta hisia ya utajiri wa Allah na utukufu wake ni katika mambo yanayosaidia kutakasa matendo.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2289) (2985). شرح النووي على مسلم (18/ 115). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص287). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص325).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ عَدْوَى وَلاَ طِيَرَةَ، وَلاَ هَامَةَ وَلاَ صَفَرَ، وَفِرَّ مِنَ المَجْذُومِ كَمَا تَفِرُّ مِنَ الأَسَدِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza baadhi ya mambo ya zama za kabla ya Uislamu, kuwa kama ni onyo dhidi yao, na kwa kuwabainishia kuwa amri yote iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, na kwamba hakuna kinachotokea isipokuwa kwa amri yake, na kadari zake, nayo ni: La kwanza: Watu wa zama za kabla ya Uislamu waliamini kwamba ugonjwa huwa unaambukiza peke yake. Kwa hiyo, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akakataza kuamini kwamba ugonjwa huwa una asili ya kuambukiza kutoka kwa mgonjwa kwenda mgonjwa mwingine. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka ya kuundesha ulimwengu; Na Yeye ndiye anayeteremsha maradhi na kuyaondoa, na halitokei hilo ila kwa kutaka kwake na kwa Kadari Yake. La Pili: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakitoka kwa ajili ya safari au biashara walikuwa wanawafukuza ndege, wakiruka kwenda kulia wanafurahi, na wakiruka kushoto wanakata tamaa na kurudi (wakiamini kuwa ni mkosi) basi, Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akakataza hali hii ya kuamini mikosi kwa sababu ya ndege, na akabainisha kuwa ni imani potofu. Tatu: Watu wa zama za kabla ya Uislamu walikuwa wakisema: Ndege bundi akitua juu ya nyumba, kuna msiba utawapata watu wa nyumba hiyo. Kwa hivyo, akakataza rehema na amani ziwe juu yake, kuamini mikosi katika hilo. Nne: Ni haramu kuamini mwezi wa Swafari kuwa ni mikosi, ambao ni mwezi wa pili katika miezi ya mwandamo. Ilisemekana kuwa Swafari ni: Nyoka tumboni anayeambukiza mifugo na watu, wanadai kuwa anaambukiza zaidi ya upele; akakanusha imani hii. Tano: Aliamrisha kujitenga mbali na mwenye ugonjwa wa ukoma kama vile mtu anavyojiweka mbali na simba. Hii ni kujikinga na kutafuta usalama kwa ajili yake na kufanya sababu alizoamrisha Mwenyezi Mungu, na ukoma ni maradhi ambayo viungo vya mtu hulika.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kumwamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kufanya sababu za kisheria.
  2. Ni wajibu kuamini hukumu na Kadari ya Mwenyezi Mungu, na kwamba sababu ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na Yeye ndiye anayezifanya zitokee au kuondoa athari zake.
  3. Kubatilika kwa baadhi ya mambo wanayoyafanya baadhi ya watu kwa kupima bao kwa kutumia rangi, kama vile nyeusi na nyekundu, au namba fulani, na majina, na watu wenye ulemavu.
  4. Katika kukataza ukaribu na wenye ukoma na wale walio na magonjwa ya kuambukiza; Ni moja ya sababu ambazo Mwenyezi Mungu aliweka desturi kuwa zinapelekea katika matokeo yake. Sababu hazijitegemei zenyewe binafsi, bali ni Mwenyeezi Mungu ambaye, Akitaka, Anaziondoa nguvu zake, kwa hivyo haziwezi kuathiri chochote, na Akitaka, Anazibakisha, hivyo zitaweza kuathiri.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 126) (5707). صحيح مسلم (4/ 1742) (2220). فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، لعبد الرحمن التميمي (ص307). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 565). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص228). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص253). التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص77).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu

عن ابن عباس رضي الله عنهما مرفوعاً: «عَيْنَانِ لاَ تَمسُّهُمَا النَّار: عَيْنٌ بَكَتْ من خَشْيَة الله، وعَيْنٌ بَاتَت تَحْرُسُ في سَبِيل الله».
Kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Maana ya hadithi: Nikuwa moto hautogusa jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo pindi anapokumbuka mtu ukubwa wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake juu ya waja wake na uzembe wake katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu; akalia kwa kutaraji rehema zake na kuogopa adhabu zake na hasira zake, basi huyu kaahidiwa kusalimika na moto. Na jicho jingine ambalo moto hautoligusa, nalo ni: Yule atakayelala akilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu katika mipaka au sehemu ya mapigano kwa kuhifadhi roho za waislamu. Na kauli yake: "Hautoyagusa moto" Hii ni katika sehemu ya kutaja sehemu ya kitu na makusudio yake ni chote: nakuwa atakayelia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu na atakayelala akilinda katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anaiharamisha miili yao katika moto.

Marejeo

- رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين؛ للإمام أبي زكريا النووي، تحقيق د. ماهر الفحل، دار ابن كثير-دمشق، الطبعة الأولى، 1428ه . - بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين؛ تأليف سليم الهلالي، دار ابن الجوزي- الطبعة الأولى1418ه - نزهة المتقين شرح رياض الصالحين؛ تأليف د. مصطفى الخِن وغيره، مؤسسة الرسالة-بيروت، الطبعة الرابعة عشر، 1407هـ. سنن الترمذي، لمحمد بن عيسى الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر ومحمد فؤاد عبد الباقي وإبراهيم عطوة عوض -شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي - مصر الطبعة: الثانية، 1395 هـ - 1975 م مشكاة المصابيح، لمحمد بن عبد الله الخطيب العمري أبو عبد الله ولي الدين التبريزي، المحقق: محمد ناصر الدين الألباني المكتب الإسلامي – بيروت- الطبعة: الثالثة، 1985.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَبْلَ وَفَاتِهِ بِثَلَاثٍ يَقُولُ: «لَا يَمُوتَنَّ أَحَدُكُمْ إِلَّا وَهُوَ يُحْسِنُ بِاللهِ الظَّنَّ».
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufa kwake kwa siku tatu akisema: "Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemhimiza muislamu kuwa asife isipokuwa katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu kwa kuwa na matarajio makubwa ya kheri wakati wa kufikwa na mauti kuwa Mwenyezi Mungu atamhurumia na kumsamehe, kwa sababu hofu hutakiwa kwa ajili ya kufanya vizuri katika matendo, na katika hali hiyo si hali ya kufanya amali yoyote, kinachotakiwa hapo nikuwa na matumaini makubwa.

Mafunzo
  1. Pupa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuuelekeza umma wake, na huruma yake kubwa kwao katika hali zake zote; hata katika maradhi ya kifo chake unaunasihi umma wake na anauelekeza katika njia za kuokoka.
  2. Amesema Attwaibi: Fanyeni matendo yenu kuwa mazuri hivi sasa ili dhana yenu iwe nzuri kwa Mwenyezi Mungu wakati wa kifo, kwani yatakayekuwa mabaya matendo yake kabla ya kifo chake atakuwa na dhana mbaya wakati wa kufa kwake.
  3. Hali kamili ya mja nikuwa kati ya matumaini na hofu, na mapenzi makubwa; mapenzi ndio kipando, na matumaini ndio gurudumu, na hofu ndio mwendo, na Mwenyezi Mungu ndiye mfikishaji kwa neema zake na karama zake.
  4. Inalazimu kwa atakayekuwa karibu na aliyefikwa na mauti azidishe kwake kumpa matumaini na kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, katika hadithi hii Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameyasema haya kabla ya kufa kwake kwa siku tatu.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2205) (2877). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 333). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 509). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 398).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 22
Hadithi 22
  1. Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?”
  2. Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”
  3. Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake
  4. Je nisikuelezeni kwa kile ambacho ninakiogopea zaidi kwenu nyinyi kuliko hata masihi dajali? Wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anapendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama
  5. Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake
  6. Hakuna kuambukizana, wala mikosi ya ndege, wala mkosi wa Bundi, wala mkosi wa Kipanga (Jamii ya ndege). Na mkimbie mwenye ukoma kama unavyomkimbia simba
  7. Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu
  8. Asife mmoja wenu isipokuwa afe katika hali ya kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu
  9. Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni
  10. Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile litakalokukereketa katika kifua chako, na ukachukia watu wasilione
  11. Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu
  12. Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia
  13. Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri,
  14. Na hakika Mwenyezi Mungu ameniteremshia wahyi kuwa, kuweni wanyenyevu, mpaka asijikweze yeyote kwa mwingine, na wala asimfanyie uadui yeyote mwenzake
  15. Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote
  16. Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
  17. Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka
  18. Hakika mja anaweza kuswali swala, hakuna anachoandikiwa isipokuwa moja ya kumi yake, moja ya tisa yake, nane ya kumi yake, saba ya kumi yake, sita ya kumi yake, tano ya kumi yake, robo yake, theluthi yake, nusu yake
  19. Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo
  20. Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?
  21. Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilolinuia
  22. Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile lililokukereketa katika nafsi yako na ukawa hukupendezwa watu walione

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com