Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake

عَن سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ سَأَلَ اللهَ الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ، وَإِنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ».
Kutoka kwa Sahali bin Hunaif radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeomba shahada na kuuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawa mkweli na mwenye ikhlasi katika nia yake hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu atamjaalia kupata daraja za mashahidi kwa nia yake ya kweli, hata akifa kitandani katika hali isiyokuwa jihadi.

Mafunzo
  1. Nia ya dhati na kufanya linalowezekana ni sababu ya kupata thawabu na malipo yaliyokusudiwa, hata kama amali inayotakiwa haijatekelezwa.
  2. Himizo la jihadi na kuomba shahada katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa umma huu, kwani anaupa kupitia amali ndogo daraja za juu zaidi peponi.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1517) (1909). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 123). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 87).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Matendo ya moyoni.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com