Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote

عن أنس رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ».
Imepokewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu hawezi kua na imani kamili mpaka atangulize mapenzi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuliko mapenzi ya mama yake na baba yake na kijana wake wa kuime na wa kike na watu wote, na mapenzi yanaambatana na kumtii na kumtetea, na kuacha kumuasi.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na kutanguliza mapenzi yake kuliko mapenzi ya viumbe wote.
  2. Katika alama za ukamilifu wa mapenzi: Ni kuzitetea sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu, na kutoa nafsi na mali katika hilo.
  3. Kumpenda Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kunaendana na kumtii katika yale aliyoyaamrisha na kumsadikisha katika yale aliyoyaeleza na kuyaepuka yale aliyoyakataza na kuyakemea, na kumfuata na kuacha uzushi.
  4. Haki ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kubwa na ni ya mkazo kuliko watu wote; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya sisi kuongoka kutoka katika upotevu na kutuokoa na moto na kufuzu kuipata Pepo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 12) (15). صحيح مسلم (1/ 67) (44). فتح الباري لابن رجب (1/ 48). الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص281). الملخص في شرح كتاب التوحيد، للفوزان (ص252). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (2/ 50).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Matendo ya moyoni.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com