Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa Mwenyezi Mungu alitolea mfano wa Uislamu na njia iliyonyooka pana isiyokuwa na konakona, na pambizoni mwa njia hii kuna kuta mbili zimeizunguka njia hii katika pande zake mbili, na njia hizo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, katikati ya hizi kuta mbili kuna milango iliyofunguliwa, na hiyo milango ni makatazo ya Mwenyezi Mungu, na katika milango hiyo kuna mapazia ambayo humzuia mwenye kupita kumuona aliye ndani, na mwanzo wa njia kuna mwenye kuita akielekeza watu na kuwaongoza na akiwaambia: Ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na huyu mwenye kuita ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na juu ya njia kuna muitaji mwingine, na huyu muitaji humkemea kila mwenye kutembea katika njia hii ambaye anaelekea kutaka kufunua pazia za milango hiyo humkemea na kumwambia Ole wako usiufungue mlango huo! kwa hakika ukiufungua mlango huo utaingia na wala hutoweza kuizuia nafsi yako isiingie humo, na huyu mwenye kuita ni mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu.
- Uislamu ndiyo Dini ya kweli, na ndiyo njia iliyonyooka ambayo hutufikisha peponi.
- Ni wajibu kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kuchunga yale aliyoyahalalisha na yale aliyoyaharamisha, na kuyapuuzia hayo kunapelekea maangamivu.
- Ubora wa Qur'ani tukufu, na kuhimizwa kuifanyia kazi, kwakuwa ndani yake kuna muongozo, mwanga na mafanikio.
- Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwa namna alivyoweka kwenye nyoyo za waumini kitu ambacho kinawazuia na kuwapa mawaidha ya kuwaepusha kuingia kwenye maangamivu.
- Mwenyezi Mungu kwa huruma zake amewawekea waja wake kizuizi kinachowazuia kutumbukia kwenye maasi.
- Miongoni mwa nyenzo za kufundishia ni kupiga mifano ili kuliweka jambo karibu na kuliweka wazi.
سنن الترمذي (4/ 539) (2859)، مسند أحمد (29/ 181، 183) (17634)، جامع العلوم والحكم (2/161)، فيض القدير (4/253)، التنوير شرح الجامع الصغير (7/100)، الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني (1/ 83).