Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kudumu kuisoma Qur'ani; kwa sababu itawatetea wasomaji wake wenye kuifanyia kazi siku ya Kiyama, kisha akatilia mkazo katika kusoma sura mbili, Baqara na Al-Imrani, ameziita kuwa ni mapambo mawili yenye kung'aa; kwa sababu ya nuru yake na muongozo wake, na kwamba malipo na thawabu za kuzisoma na kuzingatia maana zake, na kuyafanyia kazi yaliyomo, haya yatakuja siku ya Kiyama kama mawingu mawili, au kinginecho, au kama makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao walioungana baadhi yao kwa baadhi, zikimkinga msomaji wake na zikimtetea. Kisha akatilia mkazo rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Suratul-Baqara na kuzingatia maana zake na kuyafanyia kazi yaliyomo, na kwamba hilo lina baraka na manufaa makubwa ndani yake katika dunia na Akhera, na kuliacha hilo kuna masikitiko na majuto siku ya Kiyama, na kwamba miongoni mwa fadhila za sura hii nikuwa wachawi hawawezi kumdhuru mwenye kuisoma.
- Amri ya kuisoma Qur'ani na kukithirisha kufanya hivyo, na kwamba itawatetea watu wake siku ya Kiyama, na wenye kuisoma, wenye kushikamana na muongozo wake, wenye kuzifanyia kazi amri zake, na wenye kuacha iliyoyakataza.
- Fadhila za kusoma Suratul-Baqara na Ali-Imrani na ukubwa malipo yake.
- Fadhila za kusoma Suratul-Baqara, na kwamba inamlinda msomaji wake na wachawi.
صحيح مسلم (1/ 553) (804). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (4/ 1460). التنوير شرح الجامع الصغير، لمحمد الصنعاني (2/ 606). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص232). معارج القبول بشرح سلم الوصول إلى علم الأصول، لحافظ الحكمي (2/ 846). التَّحبير لإيضَاح مَعَاني التَّيسير، لمحمد الصنعاني (2/ 9). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص579).