Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesoma aya mbili za mwisho katika suratul-Baqara usiku, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza na shari na kila lenye kuchukiza, na imesemwa: Zitamtosheleza na kisimamo cha usiku, na imesemwa: Zita mtosha na nyiradi zote, na imesemwa kuwa: Ni kiwango kidogo kinachoweza kumtosheleza mtu na kusoma Qur'ani katika kisimamo cha usiku, na imesemwa kinyume na hivyo, na huenda yote yaliyotajwa yanakusanywa na tamko hilo.
- Kumebainisha fadhila za mwisho wa suratul-Baqara, nazo ni kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Aamanarrasuulu..." mpaka mwisho wa sura.
- Mwisho wa suratul-Baqara humzuilia mabaya msomaji wake na shari na Shetani atakaposoma katika usiku.
- Usiku huanza kwa kuzama jua, na humalizika kwa kuchomoza Alfajiri.
صحيح البخاري (6/ 188) (5008-5009). صحيح مسلم (1/ 554) (807). فتح الباري بشرح صحيح البخاري، لابن حجر (9/ 56). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 240). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص593). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لملا علي القاري (4/ 1465). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 757).