Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: "Pindi Jibrili alipokuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisikia kishindo kutoka juu yake, akanyanyua kichwa chake, akasema: "Huu ni mlango kutoka Mbinguni umefunguliwa leo haukuwahi kufunguliwa kabisa isipokuwa leo, kisha akateremka kutoka kwenye mlango ule Malaika, akasema: "Huyu ni Malaika ameteremka Ardhini hakupata kuteremka kabisa isipokuwa leo, akawasalimia, kisha akasema: "Pokea habari njema ya kupewa Nuru mbili hakupewa Nabii yeyote kabla yako: Ufunguzi wa kitabu (Alfatiha) na Aya za mwisho katika Suratul-baqarah, hautasoma herufi miongoni mwa Sura hizo mbili isipokuwa utapewa (unacho hitaji)"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Malaika Jibril amani iwe juu yake alikuwa amekaa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasikia sauti kutoka mbinguni kama sauti ya mlango unapofunguliwa, Jibril akanyanyua kichwa chake na macho yake mbinguni, kisha akaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango huu kutoka mbinguni umefunguliwa leo, na haukuwahi kufunguliwa katu isipokuwa leo, akateremka kutoka humo Malaika kuja Ardhini, hakuwahi kuteremka kabla isipokuwa leo, Malaika akamtolea salamu Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Kuwa na habari njema ya kupata Nuru mbili ulizopewa, ambazo hakuwahi kupewa Nabii yeyote kabla yako; nazo ni: Suratul-Fatiha, na Aya mbili za mwisho wa suratul-Baqara. Kisha Malaika akasema: Hatosoma yeyote harufi moja katika hizo isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa yale yaliyomo ndani yake miongoni mwa heri na dua na maombi.
Mafunzo
Fadhila za Suratul-Fatiha na mwisho wa Suratul-Baqara, na himizo la kuzisoma na kuyafanyia kazi mafundisho yake.
Mbingu zina milango ambayo huteremka amri za Mola kupitia hapo, na wala hazifunguliwi isipokuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kumebainishwa takrima za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi, kiasi ambacho amemkirimu kwa mambo ambayo hakuwakirimu Manabii waliokuwa kabla yake, akampatia Nuru hizi mbili.
Miongoni mwa nyenzo za kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu ni kuwapa habari njema.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 554) (806).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 244).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 700).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (4/ 1464).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 760).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (13/ 122).
عن أبي هريرة رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ، إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ الْبَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuyatelekeza majumba kwa kutoka swali ndani yake, yakawa kama makaburi yasiyoswaliwa ndani yake.
Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Shetani hukimbia nyumba ambayo husomwa suratul Baqara ndani yake.
Mafunzo
Kumependekezwa kuzidisha ibada na swala za sunna ndani ya majumba.
Haifai kuswali makaburini; kwa sababu ni njia katika njia za shirki na kuwakweza wafu, isipokuwa swala ya jeneza.
Katazo la kuswali makaburini limethibiti kwa Masahaba, na kwa sababu hiyo amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nyumba kufanywa mfano wa makaburi hakuswaliwi ndani yake.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 539) (780).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 240).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 682).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 757).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (4/ 1460).
عن أبي الدرداء رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ حَفِظَ عَشْرَ آيَاتٍ مِنْ أَوَّلِ سُورَةِ الكَهْفِ، عُصِمَ مِنَ الدَّجَّالِ». وفي رواية: «مِنْ آخِرِ سُورَةِ الكَهْف».
Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayehifadhi aya kumi kwa moyo wake za mwanzo wa suratul Kahaf atakingwa na kuepushwa na kuhifadhiwa na fitina za Masihi Dajali atakayetoka zama za mwisho na atadai uungu, na fitina zake ni fitina kubwa itakayotokea katika Ardhi tangu kuumbwa kwa Adam mpaka kusimama kwa Kiyama; kwa yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo ya ajabu ambayo atawafitinisha kwayo watakaomfuata, na hii ni kwa sababu mwanzo wa suratul Kahaf kuna maajabu na miujiza mikubwa kuliko fitina na za Dajali kwa watu, atakayezizingatia hatofitinika na Dajali. Na katika riwaya nyingine: Ni aya kumi za mwisho wa sura kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Hivi wanadhani wale waliokufuru kuwa wanaweza kujifanyia..."
Mafunzo
Kumebainishwa fadhila ya suratul Kahaf, na kuwa mwanzo wake na mwisho wake zinakinga na fitina za Dajali.
Kumeelezwa swala la Dajali, na kumebainishwa yanayokinga na fitina hiyo.
Himizo la kuihifadhi suratul Kahaf nzima, ikiwa atashindwa basi ahifadhi aya kumi za mwanzo na za mwisho.
Amesema Al-Qurtubi katika sababu ya hilo: Imesemekana: Kwa sababu ya yale yaliyoko ndani ya kisa cha watu wa pangoni katika maajabu na miujiza, atakayeizingatia hatoshangazwa na jambo la Dajali na halitamtisha hilo na wala hatofitinika, na imesemekana: Kwa sababu ya kauli yake Mtukufu: "Ili kitoe onyo kali kutoka kwake" Kwa kuuhusisha ugumu na ukali na kwake, na ndio unafaa kwa yale atakayokuwa nayo Dajali katika kudai uungu na kutawala kwake na ukubwa wa fitina yake, inakuwa maana ya hadithi nikuwa: atakayesoma aya hizi na akazizingatia na akasimama katika maana zake zitamtahadharisha na atasalimika naye.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 555) (809).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 243).
شرح النووي على مسلم (6/ 92).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (6/ 119).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (13/ 115).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لملا القاري (4/ 1465).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن (2/ 760).
عن أبي مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «مَنْ قَرَأَ بِالْآيَتَيْنِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesoma aya mbili za mwisho katika suratul-Baqara usiku, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza na shari na kila lenye kuchukiza, na imesemwa: Zitamtosheleza na kisimamo cha usiku, na imesemwa: Zita
mtosha na nyiradi zote, na imesemwa kuwa: Ni kiwango kidogo kinachoweza kumtosheleza mtu na kusoma Qur'ani katika kisimamo cha usiku, na imesemwa kinyume na hivyo, na huenda yote yaliyotajwa yanakusanywa na tamko hilo.
Mafunzo
Kumebainisha fadhila za mwisho wa suratul-Baqara, nazo ni kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Aamanarrasuulu..." mpaka mwisho wa sura.
Mwisho wa suratul-Baqara humzuilia mabaya msomaji wake na shari na Shetani atakaposoma katika usiku.
Usiku huanza kwa kuzama jua, na humalizika kwa kuchomoza Alfajiri.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 188) (5008-5009).
صحيح مسلم (1/ 554) (807).
فتح الباري بشرح صحيح البخاري، لابن حجر (9/ 56).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 240).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص593).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لملا علي القاري (4/ 1465).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 757).
عن أبي أمامة الباهلي رضي الله عنه قال: سمعتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «اقرؤوا القرآنَ فإنَّه يأتي يوم القيامة شَفِيعًا لأصحابه، اقرؤوا الزَّهرَاوَين البقرةَ وسورةَ آل عِمران، فإنهما تأتِيان يوم القيامة كأنهما غَمَامَتان، أو كأنهما غَيَايَتانِ، أو كأنهما فِرْقانِ من طَيْر صَوافٍّ، تُحاجَّان عن أصحابهما، اقرؤوا سورة البقرة، فإن أخذها بَرَكة، وتركها حَسْرة، ولا تستطيعها البَطَلَة».
Kutoka kwa Abuu Umama Al-bahily radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Someni Qur'ani, kwani, itakuja Siku ya Kiyama kama muombezi kwa sahibu wake, Zisomeni Az-Zahraawaini: Al-Baqara na Surat Al-Imran. Kwani, zitakuja Siku ya Kiyama kana kwamba ni mawingu mawili au Ghayayatani (kitu chenye kumpa kivuli mtu kwa juu ya kichwa chake), au kana kwamba ni makundi mawili ya ndege walio katika safu, (sura hizo mbili) zikiwatetea wasomaji wake. Isomeni Surat Al-Baqara. Kwani kuichukua (kuisoma) ni baraka, na kuiacha ni majuto, na wala wachawi hawaiwezi."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kudumu kuisoma Qur'ani; kwa sababu itawatetea wasomaji wake wenye kuifanyia kazi siku ya Kiyama, kisha akatilia mkazo katika kusoma sura mbili, Baqara na Al-Imrani, ameziita kuwa ni mapambo mawili yenye kung'aa; kwa sababu ya nuru yake na muongozo wake, na kwamba malipo na thawabu za kuzisoma na kuzingatia maana zake, na kuyafanyia kazi yaliyomo, haya yatakuja siku ya Kiyama kama mawingu mawili, au kinginecho, au kama makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao walioungana baadhi yao kwa baadhi, zikimkinga msomaji wake na zikimtetea. Kisha akatilia mkazo rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Suratul-Baqara na kuzingatia maana zake na kuyafanyia kazi yaliyomo, na kwamba hilo lina baraka na manufaa makubwa ndani yake katika dunia na Akhera, na kuliacha hilo kuna masikitiko na majuto siku ya Kiyama, na kwamba miongoni mwa fadhila za sura hii nikuwa wachawi hawawezi kumdhuru mwenye kuisoma.
Mafunzo
Amri ya kuisoma Qur'ani na kukithirisha kufanya hivyo, na kwamba itawatetea watu wake siku ya Kiyama, na wenye kuisoma, wenye kushikamana na muongozo wake, wenye kuzifanyia kazi amri zake, na wenye kuacha iliyoyakataza.
Fadhila za kusoma Suratul-Baqara na Ali-Imrani na ukubwa malipo yake.
Fadhila za kusoma Suratul-Baqara, na kwamba inamlinda msomaji wake na wachawi.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 553) (804).
مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (4/ 1460).
التنوير شرح الجامع الصغير، لمحمد الصنعاني (2/ 606).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص232).
معارج القبول بشرح سلم الوصول إلى علم الأصول، لحافظ الحكمي (2/ 846).
التَّحبير لإيضَاح مَعَاني التَّيسير، لمحمد الصنعاني (2/ 9).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص579).
Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi kwako?" Akasema: Nikasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi. Akasema: "Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuuliza Ubaiyya bin Kaab kuhusu aya tukufu zaidi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu, akasitasita katika kutoa jibu, kisha akasema: Aya hiyo ni Ayatul Kursiy {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} basi- Rehema na amani ziwe juu yake- akamuunga mkono, na Mtume akapiga katika kifua chake ikiwa ni ishara ya kifua hicho kujaa elimu na hekima, na akamuombea awe na furaha kwa elimu hii na Allah amfanyie wepesi.
Mafunzo
Fadhila kubwa alizokuwa nazo Ubaiyya bin Kaab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-
Ayatul Kursiy ni Aya tukufu zaidi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo inapasa kuihifadhi na kuzingatia maana yake pamoja na kuifanyia kazi.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 556) (810)، إكمال المعلم (3/178)، الكاشف عن حقائق السنن (5/1644)، المفهم (2/436)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (16/ 394).
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wakati wa kila usiku alikuwa akikusanya viganja vyake, kisha akivipuliza na kuvisomea : {Qul-huwallahu Ahad}, na {Qul-A uudhu birabbil falaq} na (Qul-Auudhu birabbi naas } Kisha hujipaka kwa viganja hivyo sehemu awezayo katika mwili wake, anaanza kupaka kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele ya mwili wake, anafanya hivyo mara tatu.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ilikuwa katika miongozo yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- pindi anapopanda kitandani kwake kwa ajili ya kulala, ni kukusanya viganja vyake na kuviinua juu kama anavyofanya mwenye kuomba-na huvipuliza viganja hivyo kwa mdomo wake upulizaji wa taratibu pamoja na kutemea matemate kidogo na anasoma Sura tatu {Qul-huwallahu Ahadu} na {Qul-audhu birabbil falaq} na {Qul-auudhu birabbi naas} Kisha hupaka kwa kutumia viganja vyake sehemu anayoweza katika mwili wake; Kwa kuanzia kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele katika mwili wake, na hurudia kitendo hicho mara tatu.
Mafunzo
Ni sunna kusoma suratul Ikhlaas na Muawidhataini (Sura mbili za kinga) kabla ya kulala na kupuliza kwa sura hizo, na kupakaa sehemu aiwezayo katika mwili wake.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 190) (5017)، (7/ 133) (5748)، الكاشف عن حقائق السُّنن (5/1651)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (20/ 35)، التوضيح لشرح الجامع الصحيح ( 24/ 91)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 929)، شرح سنن أبي داود لابن رسلان (19/268).
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nimeigawa swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, na mja wangu ana haki ya kupata alichooomba, atakaposema mja: "Al-hamdulillaahi rabbil aalamiin" (Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu), Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: "Amenihimidi mja wangu", na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim" (Mwingi wa rehema mwenye kurehemu) Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: Kanisifu mja wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin" (Mmiliki wa siku ya malipo) husema: Kanitukuza mja wangu, na mara nyingine husema: Kakabidhi kwangu mja wangu, akisema: "Iyyaaka na'budu wa iyyaaka nastaiin" (Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada) husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu, na mja wangu ana haki ya kupata alichokiomba, akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", husema: Hili ni la mja wangu na mja wangu ana haki ya kupata alichoomba".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika hadithil Qudsiy: Nimeigawanya suratul fatiha ndani ya swala kati yangu na mja wangu nusu mbili, nusu moja ya kwangu, na nusu moja ya kwake.
Nusu yake ya kwanza: Himdi na sifa na kumtukuza Mwenyezi Mungu, nitamlipa kwa hayo malipo bora zaidi.
Na nusu yake ya pili: Unyenyekevu na dua, ninamuitikia na ninampa alichoomba.
Msaliji akisema: "Al-hamdulillaahi rabbil aalaamiin", Mwenyezi Mungu husema: Amenihimidi mja wangu, na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim", husema Mwenyezi Mungu: Amenisifu mja wangu akanihimidi na akakiri kutoka kwangu neema zangu zote juu ya viumbe wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin", husema Mwenyezi Mungu: Amenitukuza mja wangu, nayo ni heshima kubwa.
Akisema: "Iyyaakana'budu wa iyyaaka nastaiin", Mwenyezi Mungu husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu.
Nusu ya kwanza katika aya hii ni ya Mwenyezi Mungu nayo ni: "Iyyaakana'budu" Nayo ni kukiri uungu kwa Mwenyezi Mungu, na kuitika wito wa ibada, na kwake ndiko inakoishia nusu ambayo ni yake Mwenyezi Mungu.
Na nusu ya pili katika aya nayo ni ya mja: "Iyyaakanastaiinu" Ni kutaka msaada kwa Allah, na kamuahidi kumsaidia.
Akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim * Swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", Mwenyezi Mungu husema: Huu ni unyenyekevu na ni dua kutoka kwa mja wangu, na mja wangu anastahiki kupata alichoomba, na tayari nimejibu dua yake.
Mafunzo
Utukufu wa suratul faatiha kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu kaiita kuwa ni swala.
Kumebainishwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kumshughulikia mja wake, kiasi kwamba amemsifia kwa sababu ya kumhimidi na kumsifia kwake na kumtukuza kwake, na akamuahidi kumpa alichoomba.
Sura hii tukufu imekusanya, kumhimidi Mwenyezi Mungu, na kukumbuka marejeo, na kumuomba Mwenyezi Mungu, na kutakasa ibada kwa ajili yake, na kuomba uongofu katika njia iliyo nyooka, na tahadhari ya njia za batili.
Kuvuta hisia za hadithi hii mwenye kuswali -anaposoma suratul fatiha- kutaongeza utulivu wake ndani ya swala.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 296) (395)، إكمال المعلم (2/275)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 27)، شرح النووي على مسلم (4/103)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (9/ 232) (9/ 253).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com