Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika hadithil Qudsiy: Nimeigawanya suratul fatiha ndani ya swala kati yangu na mja wangu nusu mbili, nusu moja ya kwangu, na nusu moja ya kwake. Nusu yake ya kwanza: Himdi na sifa na kumtukuza Mwenyezi Mungu, nitamlipa kwa hayo malipo bora zaidi. Na nusu yake ya pili: Unyenyekevu na dua, ninamuitikia na ninampa alichoomba. Msaliji akisema: "Al-hamdulillaahi rabbil aalaamiin", Mwenyezi Mungu husema: Amenihimidi mja wangu, na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim", husema Mwenyezi Mungu: Amenisifu mja wangu akanihimidi na akakiri kutoka kwangu neema zangu zote juu ya viumbe wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin", husema Mwenyezi Mungu: Amenitukuza mja wangu, nayo ni heshima kubwa. Akisema: "Iyyaakana'budu wa iyyaaka nastaiin", Mwenyezi Mungu husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu. Nusu ya kwanza katika aya hii ni ya Mwenyezi Mungu nayo ni: "Iyyaakana'budu" Nayo ni kukiri uungu kwa Mwenyezi Mungu, na kuitika wito wa ibada, na kwake ndiko inakoishia nusu ambayo ni yake Mwenyezi Mungu. Na nusu ya pili katika aya nayo ni ya mja: "Iyyaakanastaiinu" Ni kutaka msaada kwa Allah, na kamuahidi kumsaidia. Akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim * Swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", Mwenyezi Mungu husema: Huu ni unyenyekevu na ni dua kutoka kwa mja wangu, na mja wangu anastahiki kupata alichoomba, na tayari nimejibu dua yake.
- Utukufu wa suratul faatiha kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu kaiita kuwa ni swala.
- Kumebainishwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kumshughulikia mja wake, kiasi kwamba amemsifia kwa sababu ya kumhimidi na kumsifia kwake na kumtukuza kwake, na akamuahidi kumpa alichoomba.
- Sura hii tukufu imekusanya, kumhimidi Mwenyezi Mungu, na kukumbuka marejeo, na kumuomba Mwenyezi Mungu, na kutakasa ibada kwa ajili yake, na kuomba uongofu katika njia iliyo nyooka, na tahadhari ya njia za batili.
- Kuvuta hisia za hadithi hii mwenye kuswali -anaposoma suratul fatiha- kutaongeza utulivu wake ndani ya swala.
صحيح مسلم (1/ 296) (395)، إكمال المعلم (2/275)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 27)، شرح النووي على مسلم (4/103)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (9/ 232) (9/ 253).