Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

“Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ: أَنَّ رَجُلًا سَمِعَ رَجُلًا يَقْرَأُ: {قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ} يُرَدِّدُهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ جَاءَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ، وَكَأَنَّ الرَّجُلَ يَتَقَالُّهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ إِنَّهَا لَتَعْدِلُ ثُلُثَ القُرْآنِ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kuwa mwanamume mmoja alimsikia mtu akisoma: "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Huku akiirudiarudia. Ilipofika asubuhi, alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na akamueleza hilo. Na ni kana kwamba mwanamume huyo aliona jambo hilo ni jambo dogo. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake akasema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani."
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba mtu mmoja alimsikia bwana mmoja akisoma suratu: "Qul-huwallaahu Ahad" akiikariri kila usiku na wala hazidishi sura nyingine, palivopambazuka alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamsimulia tukio hilo, ni kana kwamba muulizaji anaiona kuwa ndogo, akatoa kiapo rehema na amani ziwe juu yake kwa maana ya kuonyesha msisitizo, akasema: Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake hakika sura hiyo inalingana na theluthi ya Qur'ani.

Mafunzo
  1. Fadhila za Suratul Ikhlaswi, na kuwa inalingana sawa na theluthi ya Qur'ani
  2. Inafaa kusoma katika kisimamo cha usiku walau kwa aya chache na kuzirudia rudia, na kutokuziona ndogo.
  3. Amesema Al-Maaziri: Inasemekana maana yake: Nikuwa Qur'ani iko katika sehemu tatu; visa na hukumu na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na (Qul-huwallaahu Ahad) imejikita kwa ajili ya sifa za Mwenyezi Mungu, hivyo ni theluhti, na ni moja kati ya sehemu tatu, na imesemekana maana yake kuwa: Thawabu za kuisoma kwake hulipwa mara dufu kwa kiasi cha kusoma theluthi ya Qur'ani bila kuzidishwa.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 189) (5013). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (7/ 463).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Fadhila za Sura na Aya.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com