Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ubora wa Qur'an tukufu.

Hadithi 8

Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ، وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، لَا أَقُولُ {الم} حَرْفٌ، وَلَكِنْ {أَلِفٌ} حَرْفٌ، وَ{لَامٌ} حَرْفٌ، وَ{مِيمٌ} حَرْفٌ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na huzidishiwa malipo hayo mpaka mara kumi mfano wake. Kisha akaliweka wazi hilo kwa kauli yake: (Sisemi "Alif Laam Miim" ni herufi, lakini Alif ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi): Inakuwa herufi zote tatu zina thawabu thelathini (30).

Mafunzo
  1. Himizo la kukithirisha kusoma Qur'ani.
  2. Msomaji kwa kila herufi anayoisoma kwa kila neno analolisema huzidishwa mara kumi mfano wake.
  3. Upana wa rehema za Allah na ukarimu wake kiasi kwamba huzidishwa malipo kwa waja ikiwa ni fadhila na ukarimu toka kwake.
  4. Ubora wa Qur'ani juu ya maneno mengine, na kisomo chake kutumika kama ibada; nakuwa hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 33) (2910). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 229). سلسلة الأحاديث الصحيحة، للألباني (7/ 970). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 655). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 742).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ، لَهُ أَجْرَانِ».
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba anayesoma Qur'ani, akiwa na hifdhi nzuri na mfanisi, na mahiri na hodari kwa kisomo chake, basi huyu ana thawabu Akhera kiasi cha daraja yake kuwa pamoja na Malaika wema na wakarimu, na kwamba anayesoma Qur'ani na huku akipata tabu ndani yake na anasitasita katika kisomo chake; kwa sababu ya udhaifu wa hifudhi yake, lakini pamoja na hivyo bado anashikamana nayo, na kwake bado ni ngumu na nzito basi ana malipo mara mbili; malipo ya kisomo na malipo ya tabu na kusitasita kwake katika kisomo.

Mafunzo
  1. Himizo la kuhifadhi Qur'ani na kuwa na ustadi, na kuisoma kwa wingi kwa ajili ya kupata malippo na thawabu, na kumebainishwa nafasi ya mwenye kufanya hivyo.
  2. Amesema Kadhi: Na haina maana kuwa anayesitasita ana malipo makubwa zaidi kuliko mahiri, bali mahiri ndiye bora na ndiye mwenye malipo mengi; kwa sababu yuko pamoja na Malaika na anamalipo mengi, na hakutaja nafasi hii kwa mwingine, ni vipi ataungana naye ambaye hajakipa kipaumbele kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kukihifadhi na kuwa na umahiri na wingi wa kukisoma na kukielewa kwake ni kama kukipa kipaumbele mpaka akawa mahiri ndani yake.
  3. Amesema bin Bazi: Anayesoma Qur'ani hali yakuwa ni mahiri, na anaisoma vizuri, na anaihifadhi vizuri yuko pamoja na Malaika wema watukufu, yaani: Ikiwa kama ataisoma kwa kauli na matendo, na si ilimradi kuisoma pekee, anaisoma vizuri, na anaifanyia kazi, yaani anaisimamia kwa lafudhi na maana.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 166) (4937). صحيح مسلم (1/ 549) (798). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 226). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، لمحمد المباركفوري (8/ 174). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص580). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 639). شرح كتاب التوحيد من صحيح البخاري، لعبدالله الغنيمان (2/ 592). فتح الباري بشرح صحيح البخاري، لابن حجر العسقلاني (9/ 127). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (12/ 562). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 740).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Someni Qur'ani, kwani, itakuja Siku ya Kiyama kama muombezi kwa sahibu wake

عن أبي أمامة الباهلي رضي الله عنه قال: سمعتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «اقرؤوا القرآنَ فإنَّه يأتي يوم القيامة شَفِيعًا لأصحابه، اقرؤوا الزَّهرَاوَين البقرةَ وسورةَ آل عِمران، فإنهما تأتِيان يوم القيامة كأنهما غَمَامَتان، أو كأنهما غَيَايَتانِ، أو كأنهما فِرْقانِ من طَيْر صَوافٍّ، تُحاجَّان عن أصحابهما، اقرؤوا سورة البقرة، فإن أخذها بَرَكة، وتركها حَسْرة، ولا تستطيعها البَطَلَة».
Kutoka kwa Abuu Umama Al-bahily radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Someni Qur'ani, kwani, itakuja Siku ya Kiyama kama muombezi kwa sahibu wake, Zisomeni Az-Zahraawaini: Al-Baqara na Surat Al-Imran. Kwani, zitakuja Siku ya Kiyama kana kwamba ni mawingu mawili au Ghayayatani (kitu chenye kumpa kivuli mtu kwa juu ya kichwa chake), au kana kwamba ni makundi mawili ya ndege walio katika safu, (sura hizo mbili) zikiwatetea wasomaji wake. Isomeni Surat Al-Baqara. Kwani kuichukua (kuisoma) ni baraka, na kuiacha ni majuto, na wala wachawi hawaiwezi."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kudumu kuisoma Qur'ani; kwa sababu itawatetea wasomaji wake wenye kuifanyia kazi siku ya Kiyama, kisha akatilia mkazo katika kusoma sura mbili, Baqara na Al-Imrani, ameziita kuwa ni mapambo mawili yenye kung'aa; kwa sababu ya nuru yake na muongozo wake, na kwamba malipo na thawabu za kuzisoma na kuzingatia maana zake, na kuyafanyia kazi yaliyomo, haya yatakuja siku ya Kiyama kama mawingu mawili, au kinginecho, au kama makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao walioungana baadhi yao kwa baadhi, zikimkinga msomaji wake na zikimtetea. Kisha akatilia mkazo rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Suratul-Baqara na kuzingatia maana zake na kuyafanyia kazi yaliyomo, na kwamba hilo lina baraka na manufaa makubwa ndani yake katika dunia na Akhera, na kuliacha hilo kuna masikitiko na majuto siku ya Kiyama, na kwamba miongoni mwa fadhila za sura hii nikuwa wachawi hawawezi kumdhuru mwenye kuisoma.

Mafunzo
  1. Amri ya kuisoma Qur'ani na kukithirisha kufanya hivyo, na kwamba itawatetea watu wake siku ya Kiyama, na wenye kuisoma, wenye kushikamana na muongozo wake, wenye kuzifanyia kazi amri zake, na wenye kuacha iliyoyakataza.
  2. Fadhila za kusoma Suratul-Baqara na Ali-Imrani na ukubwa malipo yake.
  3. Fadhila za kusoma Suratul-Baqara, na kwamba inamlinda msomaji wake na wachawi.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 553) (804). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (4/ 1460). التنوير شرح الجامع الصغير، لمحمد الصنعاني (2/ 606). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص232). معارج القبول بشرح سلم الوصول إلى علم الأصول، لحافظ الحكمي (2/ 846). التَّحبير لإيضَاح مَعَاني التَّيسير، لمحمد الصنعاني (2/ 9). تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص579).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka

عَنْ النَّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ الْأَنْصَارِيِّ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «ضَرَبَ اللهُ مَثَلًا صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا، وَعَلَى جَنْبَتَيْ الصِّرَاطِ سُورَانِ، فِيهِمَا أَبْوَابٌ مُفَتَّحَةٌ، وَعَلَى الْأَبْوَابِ سُتُورٌ مُرْخَاةٌ، وَعَلَى بَابِ الصِّرَاطِ دَاعٍ يَقُولُ: أَيُّهَا النَّاسُ، ادْخُلُوا الصِّرَاطَ جَمِيعًا، وَلَا تَتَعَرَّجُوا، وَدَاعٍ يَدْعُو مِنْ فَوْقِ الصِّرَاطِ، فَإِذَا أَرَادَ يَفْتَحُ شَيْئًا مِنْ تِلْكَ الْأَبْوَابِ، قَالَ: وَيْحَكَ لَا تَفْتَحْهُ، فَإِنَّكَ إِنْ تَفْتَحْهُ تَلِجْهُ، وَالصِّرَاطُ الْإِسْلَامُ، وَالسُّورَانِ: حُدُودُ اللهِ، وَالْأَبْوَابُ الْمُفَتَّحَةُ: مَحَارِمُ اللهِ، وَذَلِكَ الدَّاعِي عَلَى رَأْسِ الصِّرَاطِ: كِتَابُ اللهِ، وَالدَّاعِي مِنِ فَوْقَ الصِّرَاطِ: وَاعِظُ اللهِ فِي قَلْبِ كُلِّ مُسْلِمٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Nawwaas bin Sam'aan Al-Answaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kapokea kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka ,na pambizoni mwa njia kuna kuta mbili, kuta hizo zina milango ilikuwa wazi, na kwenye milango kuna pazia isiyomuonesha mwenyekupita, na mbele ya kila mlango kuna mwenye kuita akisema: Enyi watu, ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na juu ya huyu muitaji kuna muitaji mwingine akiita juu ya njia, na kila mja anapotaka kufungua kidogo milango hiyo anasema: Ole wako wacha usiufungue mlango huo, ikiwa utaufungua tu hutoweza kujizuia, na njia hapa ni Uislamu, na kuta mbili: Ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, na milango iliyofunguliwa: Ni maharamisho ya Mwenyezi Mungu, na huyo muitaji aliyopo mwanzo wa mlango ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muitaji aliyepo juu: Ni Mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu."
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa Mwenyezi Mungu alitolea mfano wa Uislamu na njia iliyonyooka pana isiyokuwa na konakona, na pambizoni mwa njia hii kuna kuta mbili zimeizunguka njia hii katika pande zake mbili, na njia hizo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, katikati ya hizi kuta mbili kuna milango iliyofunguliwa, na hiyo milango ni makatazo ya Mwenyezi Mungu, na katika milango hiyo kuna mapazia ambayo humzuia mwenye kupita kumuona aliye ndani, na mwanzo wa njia kuna mwenye kuita akielekeza watu na kuwaongoza na akiwaambia: Ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na huyu mwenye kuita ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na juu ya njia kuna muitaji mwingine, na huyu muitaji humkemea kila mwenye kutembea katika njia hii ambaye anaelekea kutaka kufunua pazia za milango hiyo humkemea na kumwambia Ole wako usiufungue mlango huo! kwa hakika ukiufungua mlango huo utaingia na wala hutoweza kuizuia nafsi yako isiingie humo, na huyu mwenye kuita ni mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu.

Mafunzo
  1. Uislamu ndiyo Dini ya kweli, na ndiyo njia iliyonyooka ambayo hutufikisha peponi.
  2. Ni wajibu kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kuchunga yale aliyoyahalalisha na yale aliyoyaharamisha, na kuyapuuzia hayo kunapelekea maangamivu.
  3. Ubora wa Qur'ani tukufu, na kuhimizwa kuifanyia kazi, kwakuwa ndani yake kuna muongozo, mwanga na mafanikio.
  4. Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwa namna alivyoweka kwenye nyoyo za waumini kitu ambacho kinawazuia na kuwapa mawaidha ya kuwaepusha kuingia kwenye maangamivu.
  5. Mwenyezi Mungu kwa huruma zake amewawekea waja wake kizuizi kinachowazuia kutumbukia kwenye maasi.
  6. Miongoni mwa nyenzo za kufundishia ni kupiga mifano ili kuliweka jambo karibu na kuliweka wazi.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 539) (2859)، مسند أحمد (29/ 181، 183) (17634)، جامع العلوم والحكم (2/161)، فيض القدير (4/253)، التنوير شرح الجامع الصغير (7/100)، الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني (1/ 83).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ إِذَا رَجَعَ إِلَى أَهْلِهِ أَنْ يَجِدَ فِيهِ ثَلَاثَ خَلِفَاتٍ عِظَامٍ سِمَانٍ؟» قُلْنَا: نَعَمْ. قَالَ: «فَثَلَاثُ آيَاتٍ يَقْرَأُ بِهِنَّ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ خَيْرٌ لَهُ مِنْ ثَلَاثِ خَلِفَاتٍ عِظَامٍ سِمَانٍ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?" Tukasema: Ndiy. Akasema: "Basi aya tatu anazozisoma mmoja wenu katika sala zake ni bora kwake kuliko Ngamia watatu wenye mimba na walionenepa."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo ya kusoma Aya tatu katika sala; ni bora kuliko mtu kupata nyumbani kwake Ngamia wakubwa wenye mimba na walio nenepa.

Mafunzo
  1. Kumewekwa wazi ubora wa kuisoma Qur'ani ndani ya sala.
  2. Matendo mema ni bora na ni yenye kubakia kuliko starehe za Dunia zenye kuisha.
  3. Fadhila hizi haziishii tu kwa kusoma Aya tatu, bali kila msomaji anapozidi kusoma Aya nyingi za Qur'ani katika sala zake, malipo yake yanakuwa ni bora kwake kuliko idadi ya Ngamia wanene wenye mimba.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 552) (802)، إكمال المعلم (3/172)، الإفصاح عن معاني الصِّحاح (8/65)، فتح المنعم شرح صحيح مسلم (3/620)، البحر المحيط الثجاج (16/343).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «يقالُ لصاحبِ القرآن: اقرَأ وارتَقِ، ورتِّل كما كُنْتَ ترتِّل في الدُنيا، فإن منزِلَكَ عندَ آخرِ آية تقرؤها».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa msomaji wa Qur'ani mwenye kufanyia kazi yaliyomo ndani yake, aliyeshikamana na kuisoma na kuihifadhi, akiingia Peponi ataambiwa: Isome Qur'ani na upande cheo na daraja katika daraja za peponi, na usome kama vile ulivokuwa ukisoma Duniani kwa kuisoma kwa upole na utulivu; kwa hakika Cheo chako kitaishia kwenye Aya ya mwisho utakayo isoma.

Mafunzo
  1. Malipo huwa kwa mujibu wa matendo, kwa kuangalia wingi wake na namna yalivyofanywa.
  2. Himizo juu ya kuisoma Qur'ani kwa namna nzuri na kuihifadhi na kuizingatia pamoja na kuifanyia kazi.
  3. Pepo ina vituo na daraja nyingi, watu wa Qur'ani hupata daraja la juu kabisa.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 592) (1464)، سنن الترمذي (5/ 35) (2914)، مسند أحمد (11/ 403) (6799)، السنن الكبرى للنسائي (7/ 272) (8002)، معالم السنن (1/290)، تحفة الأحوذي (8/187)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (4/ 237).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka

عن عُقبة بن عامر الجُهني رضي الله عنه قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم: «الجاهِرُ بالقرآن كالجاهِرِ بالصَّدَقَةِ، والمُسِرُّ بالقرآن كالمُسِرِّ بالصَّدَقَة».
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir Al-juhaniy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka."
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kuweka wazi kusoma Qur'ani ni sawa na mwenye kuweka wazi anapotoa sadaka, na mwenye kuficha kisomo cha Qur'ani ni sawa na mwenye kuificha sadaka.

Mafunzo
  1. Kuficha usomaji wa Qur'ani ni bora, kama ilivyo kuficha sadaka ni bora zaidi, kwa kuwa kufanya hivyo ni katika utakasifu wa nia na kujiweka mbali na kujionesha na kujisikia, isipokuwa itakapohitajika, na maslahi ya kuisoma kwa wazi ni katika kuifundisha.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 494) (1333)، سنن الترمذي (5/ 40) (2919)، سنن النسائي (5/ 80) (2561)، الكاشف عن حقائق السُّنن (5/1688)، شرح أبي داود للعيني (5/238)، تحفة الأحوذي (8/ 191)، التنوير في شرح الجامع الصغير (5/286).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nimeigawa swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, na mja wangu ana haki ya kupata alichooomba

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عنه سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: «قَالَ اللهُ تَعَالَى: قَسَمْتُ الصَّلَاةَ بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي نِصْفَيْنِ، وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ، فَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: {الْحَمْدُ لِلهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ}، قَالَ اللهُ تَعَالَى: حَمِدَنِي عَبْدِي، وَإِذَا قَالَ: {الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ}، قَالَ اللهُ تَعَالَى: أَثْنَى عَلَيَّ عَبْدِي، وَإِذَا قَالَ: {مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ}، قَالَ: مَجَّدَنِي عَبْدِي، -وَقَالَ مَرَّةً: فَوَّضَ إِلَيَّ عَبْدِي-، فَإِذَا قَالَ: {إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ}، قَالَ: هَذَا بَيْنِي وَبَيْنَ عَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ، فَإِذَا قَالَ: {اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ، صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلا الضَّالِّينَ}، قَالَ: هَذَا لِعَبْدِي وَلِعَبْدِي مَا سَأَلَ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nimeigawa swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, na mja wangu ana haki ya kupata alichooomba, atakaposema mja: "Al-hamdulillaahi rabbil aalamiin" (Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu), Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: "Amenihimidi mja wangu", na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim" (Mwingi wa rehema mwenye kurehemu) Mwenyezi Mungu Mtukufu husema: Kanisifu mja wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin" (Mmiliki wa siku ya malipo) husema: Kanitukuza mja wangu, na mara nyingine husema: Kakabidhi kwangu mja wangu, akisema: "Iyyaaka na'budu wa iyyaaka nastaiin" (Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada) husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu, na mja wangu ana haki ya kupata alichokiomba, akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", husema: Hili ni la mja wangu na mja wangu ana haki ya kupata alichoomba".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema katika hadithil Qudsiy: Nimeigawanya suratul fatiha ndani ya swala kati yangu na mja wangu nusu mbili, nusu moja ya kwangu, na nusu moja ya kwake. Nusu yake ya kwanza: Himdi na sifa na kumtukuza Mwenyezi Mungu, nitamlipa kwa hayo malipo bora zaidi. Na nusu yake ya pili: Unyenyekevu na dua, ninamuitikia na ninampa alichoomba. Msaliji akisema: "Al-hamdulillaahi rabbil aalaamiin", Mwenyezi Mungu husema: Amenihimidi mja wangu, na akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiim", husema Mwenyezi Mungu: Amenisifu mja wangu akanihimidi na akakiri kutoka kwangu neema zangu zote juu ya viumbe wangu, na akisema: "Maaliki yaumid-diin", husema Mwenyezi Mungu: Amenitukuza mja wangu, nayo ni heshima kubwa. Akisema: "Iyyaakana'budu wa iyyaaka nastaiin", Mwenyezi Mungu husema: Hili ni kati yangu mimi na mja wangu. Nusu ya kwanza katika aya hii ni ya Mwenyezi Mungu nayo ni: "Iyyaakana'budu" Nayo ni kukiri uungu kwa Mwenyezi Mungu, na kuitika wito wa ibada, na kwake ndiko inakoishia nusu ambayo ni yake Mwenyezi Mungu. Na nusu ya pili katika aya nayo ni ya mja: "Iyyaakanastaiinu" Ni kutaka msaada kwa Allah, na kamuahidi kumsaidia. Akisema: "Ihdinas swiraatwal mustaqiim * Swiraatwalladhiina an amta alaihim, ghairil maghdhuubi alaihim waladh dhwaalliin", Mwenyezi Mungu husema: Huu ni unyenyekevu na ni dua kutoka kwa mja wangu, na mja wangu anastahiki kupata alichoomba, na tayari nimejibu dua yake.

Mafunzo
  1. Utukufu wa suratul faatiha kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu kaiita kuwa ni swala.
  2. Kumebainishwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kumshughulikia mja wake, kiasi kwamba amemsifia kwa sababu ya kumhimidi na kumsifia kwake na kumtukuza kwake, na akamuahidi kumpa alichoomba.
  3. Sura hii tukufu imekusanya, kumhimidi Mwenyezi Mungu, na kukumbuka marejeo, na kumuomba Mwenyezi Mungu, na kutakasa ibada kwa ajili yake, na kuomba uongofu katika njia iliyo nyooka, na tahadhari ya njia za batili.
  4. Kuvuta hisia za hadithi hii mwenye kuswali -anaposoma suratul fatiha- kutaongeza utulivu wake ndani ya swala.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 296) (395)، إكمال المعلم (2/275)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 27)، شرح النووي على مسلم (4/103)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (9/ 232) (9/ 253).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com