Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ، وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، لَا أَقُولُ {الم} حَرْفٌ، وَلَكِنْ {أَلِفٌ} حَرْفٌ، وَ{لَامٌ} حَرْفٌ، وَ{مِيمٌ} حَرْفٌ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na huzidishiwa malipo hayo mpaka mara kumi mfano wake. Kisha akaliweka wazi hilo kwa kauli yake: (Sisemi "Alif Laam Miim" ni herufi, lakini Alif ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi): Inakuwa herufi zote tatu zina thawabu thelathini (30).

Mafunzo
  1. Himizo la kukithirisha kusoma Qur'ani.
  2. Msomaji kwa kila herufi anayoisoma kwa kila neno analolisema huzidishwa mara kumi mfano wake.
  3. Upana wa rehema za Allah na ukarimu wake kiasi kwamba huzidishwa malipo kwa waja ikiwa ni fadhila na ukarimu toka kwake.
  4. Ubora wa Qur'ani juu ya maneno mengine, na kisomo chake kutumika kama ibada; nakuwa hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 33) (2910). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 229). سلسلة الأحاديث الصحيحة، للألباني (7/ 970). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 655). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 742).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora wa kuitilia umuhimu Qur'ani.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com