عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «تَعَاهَدُوا هَذَا الْقُرْآنَ، فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَهُوَ أَشَدُّ تَفَلُّتًا مِنَ الْإِبِلِ فِي عُقُلِهَا».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Shikamaneni vizuri na hii Qur'ani, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hutoroka kwa kasi mno kuliko hata Ngamia katika kamba yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kushikamana na Qur'ani na kudumu na kuisoma ili mtu asiisahau baada yakuwa kaihifadhi katika kifua chake, na akalisisitiza hilo kwa kiapo chake -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Qur'ani hujitoa haraka mno na kuondoka kutoka vifuani kuliko hata Ngamia aliyefungwa, naye ni yule aliyekazwa kwa kamba kati kati ya muhundi, mtu akikaa karibu naye atamshika, na akimuacha ataondoka na atapotea.
Mafunzo
- Aliyehifadhi Qur'ani akidumu katika kuisoma kila mara itabakia kuwa imehifadhiwa katika moyo wake, na asipofanya hivyo itaondoka na ataisahau.
- Katika faida za kushikana na Qur'ani ni: Malipo na thawabu, na kunyanyuliwa daraja siku ya Kiyama.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 545) (791).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، تأليف سليم الهلالي (2/ 231).
رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين (ص299) (1002).
شرح رياض الصالحين، للشيخ محمد بن صالح العثيمين (4/ 657).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (13/ 5).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عثمان رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «خَيْرُكُمْ مَنْ تَعَلَّمَ الْقُرْآنَ وَعَلَّمَهُ».
Imepokewa kutoka kwa Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mmbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu bora na aliye na daraja ya juu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu: Ni yule aliyejifunza Qur'ani, kwa kuisoma na kuihifadhi na kuisoma vizuri na kuielewa na kuitafsiri, na akamfundisha mwingine kile alichonacho katika elimu za Qur'ani pamoja na kuifanyia kazi.
Mafunzo
- Kumebainishwa utukufu wa Qur'ani, nakuwa ndio maneno bora; kwani ni maneno ya Allah.
- Mwanafunzi bora ni yule anayefundisha wengine, hatosheki kujifunza mwenyewe pekee.
- Kujifunza Qur'ani na kuifundisha kunakusanya, kuisoma na maana yake na hukumu zake.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 192) (5027).
فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن حجر العسقلاني (1/ 374).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 226).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن وغيره (1/ 740).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 638).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَن أَبي مُوْسى الأَشْعريِّ رضي الله عنه قال: قال رسولُ اللهِ صلى اللهُ عليه وسلم: «مَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ الْأُتْرُجَّةِ، رِيحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا طَيِّبٌ، وَمَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي لَا يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ التَّمْرَةِ، لَا رِيحَ لَهَا وَطَعْمُهَا حُلْوٌ، وَمَثَلُ الْمُنَافِقِ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ مَثَلُ الرَّيْحَانَةِ، رِيحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا مُرٌّ، وَمَثَلُ الْمُنَافِقِ الَّذِي لَا يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ الْحَنْظَلَةِ، لَيْسَ لَهَا رِيحٌ وَطَعْمُهَا مُرٌّ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu, na mfano wa mnafiki mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa Ua la Raihana harufu yake nzuri lakini ladha yake chungu, na mfano wa mnafiki ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tango pori, halina harufu na ladha yake chungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake migawanyiko ya watu katika kuisoma Qur'ani na kunufaika nayo.
Sehemu ya kwanza: Ni muumini anayesoma Qur'ani na ananufaika nayo, yeye ni mfano wa chenza, lina ladha nzuri na harufu nzuri na rangi nzuri, na manufaa yake ni mengi, kwani yeye huyafanyia kazi anayoyasoma, na kuwanufaisha waja wa Mwenyezi Mungu.
Sehemu ya pili: Ni muumini asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tende, ladha yake tamu, lakini haina harufu, moyo wake umejawa na imani mfano wa tende ilivyojawa utamu katika ladha yake na juu yake, na kutosikika harufu yake ambayo watu huinusa; kwa kutosikika kisomo toka kwake ambacho watu watapata raha kwa kukisikiliza
Sehemu ya tatu: Mnafiki anayesoma Qur'ani, yeye ni mfano wa Ua Raihana, lina harufu nzuri na ladha yake chungu, kwakuwa hakuurekebisha moyo wake kwa imani, na hakuifanyia kazi Qur'ani, na anaonekana mbele za watu kuwa ni muumini, harufu yake nzuri inafanana na kisomo chake, na ladha ya chungu inafanana na ukafiri wake.
Sehemu ya nne: Mnafiki asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tango pori, kiasi kwamba halina harufu nzuri, na ladha yake ni chungu, kukosekana kwa harufu yake kumefanana na harufu yake; kwa kutoisoma, na uchungu wa ladha yake unafanana na uchungu wa ukafiri wake, ndani mwake kuko tupu hakuna imani, na nje yake hakuna manufaa, bali kuna madhara.
Mafunzo
- Kumebainishwa ubora wa mwenye kuibeba Qur'ani mwenye kuifanyia kazi.
- Miongoni mwa njia za ufundishaji ni kupiga mifano; ili kusogeza karibu uelewa.
- Inatakiwa muislamu awe na kiwango maalum cha fungu katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 77) (5427).
صحيح مسلم (1/ 549) (797).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 227).
نزهة المتقين، لجمعٌ من المشايخ (1/ 741).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (12/ 568).
شرح رياض الصالحين، للعثيمين (4/ 642).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ، وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، لَا أَقُولُ {الم} حَرْفٌ، وَلَكِنْ {أَلِفٌ} حَرْفٌ، وَ{لَامٌ} حَرْفٌ، وَ{مِيمٌ} حَرْفٌ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na huzidishiwa malipo hayo mpaka mara kumi mfano wake.
Kisha akaliweka wazi hilo kwa kauli yake: (Sisemi "Alif Laam Miim" ni herufi, lakini Alif ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi): Inakuwa herufi zote tatu zina thawabu thelathini (30).
Mafunzo
- Himizo la kukithirisha kusoma Qur'ani.
- Msomaji kwa kila herufi anayoisoma kwa kila neno analolisema huzidishwa mara kumi mfano wake.
- Upana wa rehema za Allah na ukarimu wake kiasi kwamba huzidishwa malipo kwa waja ikiwa ni fadhila na ukarimu toka kwake.
- Ubora wa Qur'ani juu ya maneno mengine, na kisomo chake kutumika kama ibada; nakuwa hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 33) (2910).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 229).
سلسلة الأحاديث الصحيحة، للألباني (7/ 970).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 655).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 742).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ، لَهُ أَجْرَانِ».
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba anayesoma Qur'ani, akiwa na hifdhi nzuri na mfanisi, na mahiri na hodari kwa kisomo chake, basi huyu ana thawabu Akhera kiasi cha daraja yake kuwa pamoja na Malaika wema na wakarimu, na kwamba anayesoma Qur'ani na huku akipata tabu ndani yake na anasitasita katika kisomo chake; kwa sababu ya udhaifu wa hifudhi yake, lakini pamoja na hivyo bado anashikamana nayo, na kwake bado ni ngumu na nzito basi ana malipo mara mbili; malipo ya kisomo na malipo ya tabu na kusitasita kwake katika kisomo.
Mafunzo
- Himizo la kuhifadhi Qur'ani na kuwa na ustadi, na kuisoma kwa wingi kwa ajili ya kupata malippo na thawabu, na kumebainishwa nafasi ya mwenye kufanya hivyo.
- Amesema Kadhi: Na haina maana kuwa anayesitasita ana malipo makubwa zaidi kuliko mahiri, bali mahiri ndiye bora na ndiye mwenye malipo mengi; kwa sababu yuko pamoja na Malaika na anamalipo mengi, na hakutaja nafasi hii kwa mwingine, ni vipi ataungana naye ambaye hajakipa kipaumbele kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kukihifadhi na kuwa na umahiri na wingi wa kukisoma na kukielewa kwake ni kama kukipa kipaumbele mpaka akawa mahiri ndani yake.
- Amesema bin Bazi: Anayesoma Qur'ani hali yakuwa ni mahiri, na anaisoma vizuri, na anaihifadhi vizuri yuko pamoja na Malaika wema watukufu, yaani: Ikiwa kama ataisoma kwa kauli na matendo, na si ilimradi kuisoma pekee, anaisoma vizuri, na anaifanyia kazi, yaani anaisimamia kwa lafudhi na maana.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 166) (4937).
صحيح مسلم (1/ 549) (798).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 226).
تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، لمحمد المباركفوري (8/ 174).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص580).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 639).
شرح كتاب التوحيد من صحيح البخاري، لعبدالله الغنيمان (2/ 592).
فتح الباري بشرح صحيح البخاري، لابن حجر العسقلاني (9/ 127).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (12/ 562).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 740).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «يقالُ لصاحبِ القرآن: اقرَأ وارتَقِ، ورتِّل كما كُنْتَ ترتِّل في الدُنيا، فإن منزِلَكَ عندَ آخرِ آية تقرؤها».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa msomaji wa Qur'ani mwenye kufanyia kazi yaliyomo ndani yake, aliyeshikamana na kuisoma na kuihifadhi, akiingia Peponi ataambiwa: Isome Qur'ani na upande cheo na daraja katika daraja za peponi, na usome kama vile ulivokuwa ukisoma Duniani kwa kuisoma kwa upole na utulivu; kwa hakika Cheo chako kitaishia kwenye Aya ya mwisho utakayo isoma.
Mafunzo
- Malipo huwa kwa mujibu wa matendo, kwa kuangalia wingi wake na namna yalivyofanywa.
- Himizo juu ya kuisoma Qur'ani kwa namna nzuri na kuihifadhi na kuizingatia pamoja na kuifanyia kazi.
- Pepo ina vituo na daraja nyingi, watu wa Qur'ani hupata daraja la juu kabisa.
Marejeo
سنن أبي داود (2/ 592) (1464)، سنن الترمذي (5/ 35) (2914)، مسند أحمد (11/ 403) (6799)، السنن الكبرى للنسائي (7/ 272) (8002)، معالم السنن (1/290)، تحفة الأحوذي (8/187)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (4/ 237).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com