Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma
عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «يقالُ لصاحبِ القرآن: اقرَأ وارتَقِ، ورتِّل كما كُنْتَ ترتِّل في الدُنيا، فإن منزِلَكَ عندَ آخرِ آية تقرؤها».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa msomaji wa Qur'ani mwenye kufanyia kazi yaliyomo ndani yake, aliyeshikamana na kuisoma na kuihifadhi, akiingia Peponi ataambiwa: Isome Qur'ani na upande cheo na daraja katika daraja za peponi, na usome kama vile ulivokuwa ukisoma Duniani kwa kuisoma kwa upole na utulivu; kwa hakika Cheo chako kitaishia kwenye Aya ya mwisho utakayo isoma.
Mafunzo
Malipo huwa kwa mujibu wa matendo, kwa kuangalia wingi wake na namna yalivyofanywa.
Himizo juu ya kuisoma Qur'ani kwa namna nzuri na kuihifadhi na kuizingatia pamoja na kuifanyia kazi.
Pepo ina vituo na daraja nyingi, watu wa Qur'ani hupata daraja la juu kabisa.
Marejeo
سنن أبي داود (2/ 592) (1464)، سنن الترمذي (5/ 35) (2914)، مسند أحمد (11/ 403) (6799)، السنن الكبرى للنسائي (7/ 272) (8002)، معالم السنن (1/290)، تحفة الأحوذي (8/187)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (4/ 237).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com