عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «رِبَاطُ يَوْمٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ مِنَ الجَنَّةِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَالرَّوْحَةُ يَرُوحُهَا العَبْدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوِ الغَدْوَةُ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kubakia katika eneo ambalo liko kati ya waislamu na makafiri kwa ajili ya kuwalinda dhidi yao kwa siku moja, kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba mahali pa kuweka mjeledi unaotumika kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba malipo na thawabu za kutembea katika wakati wa mwanzo wa mchana mpaka mwanzo wa wakati wa adhuhuri, au mchana: Ni kwanzia adhuhuri mpaka usiku katika njia ya Mwenyezi Mungu mara moja, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
Mafunzo
- Fadhila za kuthubutu katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya hatari zilizomo zinazoihatarisha nafsi, na kwa yale yanayofungamana nalo kama kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuitetea dini yake, kwa hivyo, thawabu za siku moja pekee, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
- Udhalili wa dunia ukiilinganisha na akhera; kwa sababu sehemu ya kuweka mjeledi pekee peponi, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
- Ubora wa kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ukubwa wa thawabu zake; kwa sababu thawabu za mwendo mmoja wa asubuhi au mchana, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
- Kauli yake: "Katika njia ya Mwenyezi Mungu" hapa kuna dalili ya umuhimu wa kutakasa nia, na kwamba malipo yanaambatana na hilo.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 35) (2892).
صحيح مسلم (3/ 1500) (1881).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص739).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَن سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ سَأَلَ اللهَ الشَّهَادَةَ بِصِدْقٍ بَلَّغَهُ اللهُ مَنَازِلَ الشُّهَدَاءِ، وَإِنْ مَاتَ عَلَى فِرَاشِهِ».
Kutoka kwa Sahali bin Hunaif radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayeomba shahada na kuuawa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na akawa mkweli na mwenye ikhlasi katika nia yake hiyo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu atamjaalia kupata daraja za mashahidi kwa nia yake ya kweli, hata akifa kitandani katika hali isiyokuwa jihadi.
Mafunzo
- Nia ya dhati na kufanya linalowezekana ni sababu ya kupata thawabu na malipo yaliyokusudiwa, hata kama amali inayotakiwa haijatekelezwa.
- Himizo la jihadi na kuomba shahada katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa umma huu, kwani anaupa kupitia amali ndogo daraja za juu zaidi peponi.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1517) (1909).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 123).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 87).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَن زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ جَهَّزَ غَازِيًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَقَدْ غَزَا، وَمَنْ خَلَفَ غَازِيًا فِي سَبِيلِ اللَّهِ بِخَيْرٍ فَقَدْ غَزَا».
Kutoka kwa Zaidi bin Khalid radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji kwa wema katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayemuandalia mwenye kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sababu za safari yake na anachohitaji katika silaha muhimu, vipando, chakula, gharama na vitu vingine; basi yuko katika nafasi sawa na mpiganaji, na atapata malipo ya mpiganaji.
Na atakayesimamia jambo la mpiganaji kwa wema, na akakaa badala yake katika kulea familia yake wakati asipokuwepo basi naye yuko katika hukumu ya mpiganaji.
Mafunzo
- Hili ni himizo kwa waislamu kusaidizana katika heri.
- Amesema bin Hajar: Katika Hadithi hii kuna himizo la kuwafanyia wema wale wanaowafanyia wema Waislamu, au kutekeleza moja ya wajibu wao.
- Kanuni ya jumla nikuwa: Yeyote anayemsaidia mtu katika kumtii Mwenyezi Mungu atapata malipo sawa na malipo yake, bila ya kupunguzwa ujira wake hata kidogo.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 27) (2843).
صحيح مسلم (3/ 1506) (1895).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 267).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص143).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 588).
لسان العرب، لابن منظور (15/ 123).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 374).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 202).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي عَبْسٍ عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنِ جَبْرٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا اغْبَرَّتْ قَدَمَا عَبْدٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَتَمَسَّهُ النَّارُ».
Kutoka kwa Abuu Absi Abdulrahman bin Jabri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimbashiria yeyote itakayepatwa na vumbi miguu yake huku akiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa moto hautomgusa.
Mafunzo
- Habari njema kwa mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ya kuokoka na moto.
- Ametaja miguu miwili pamoja nakuwa vumbi huenea mwili mzima; kwa sababu wapigana ji wengi katika zama hizo walikuwa watembea kwa miguu, na miguu hupata vumbi kwa namna yoyote ile.
- Amesema bin Hajari: Ikiwa kitendo cha kuguswa na vumbi pekee kinaharamisha kuguswa na moto; vipi kwa atakayekwenda mbio na akatoa juhudi na akapoteza muda wake.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 20) (2811)، (2/ 7) (907).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 424).
التنوير شرح الجامع الصغير، للصنعاني (7/ 361).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 437).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 911).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «مَا يَجِدُ الشَّهيد من مَسِّ القتل إلا كما يَجِدُ أَحَدُكُمْ من مَسِّ القَرْصَةِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Anachokipata aliyekufa shahidi katika maumivu ya kifo, ni kama maumivu anayoyapata mmoja wenu kutokana na kung'atwa na mdudu chungu".
Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na AddaaramyDarajaNi nzuri
Maelezo
Maana ya hadithi: nikuwa mtu atakapokufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakika yale yanayompata katika mguso wa kifo, na katika riwaya ya Daaramiy (katika maumivu ya kifo) hayahisi isipokuwa ni kama anavyohisi mmoja wetu anapong'atwa na mdudu chungu, na katika riwaya ya Daaramiy "kutokana na maumivu ya kung'atwa". Na maana yake nikuwa: Shahidi hasongwi na ukali wa maumivu ya kifo, kama ilivyo hali ya watu wengine, bali ukali anaoupata na ukamsumbua wakati wa kifo chake ni kama ule tunaoupata kwasababu ya kung'atwa na mdudu chungu, na maumivu anayosababu mdudu huyo na uharaka wa kumalizika kwake, basi wala hayahisi, Na hii ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa shahidi, kwani yeye alipoitanguliza roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kiurahisi, basi Mwenyezi Mungu akampunguzia juu yake maumivu ya kuuwawa.
Marejeo
- سنن أبي داود، سليمان بن الأشعث السِّجِسْتاني تحقيق: محمد محيي الدين عبد الحميد، المكتبة العصرية.
- سنن ابن ماجه، ابن ماجه أبو عبد الله محمد بن يزيد القزويني، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي- دار إحياء الكتب العربية - فيصل عيسى البابي الحلبي.
- السنن الصغرى، للنسائي، أحمد بن شعيب، النسائي، تحقيق: عبد الفتاح أبو غدة، مكتب المطبوعات الإسلامية، حلب، الطبعة الثانية، 1406ه – 1986م.
- مسند الإمام أحمد بن حنبل، المحقق: شعيب الأرنؤوط - عادل مرشد، وآخرون، إشراف: د عبد الله بن عبد المحسن التركي، مؤسسة الرسالة، الطبعة الأولى، 1421هـ - 2001م.
- سنن الترمذي، محمد بن عيسى الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر ومحمد فؤاد عبد الباقي وإبراهيم عطوة عوض، شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي – مصر، الطبعة الثانية، 1395هـ - 1975م.
-مسند الدارمي المعروف بـ (سنن الدارمي) عبد الله بن عبد الرحمن الدارمي، تحقيق: حسين سليم أسد الداراني - دار المغني للنشر والتوزيع، المملكة العربية السعودية، الطبعة الأولى، 1412هـ - 2000م.
- صحيح الجامع الصغير وزياداته، الألباني، دار المكتب الإسلامي، بيروت، لبنان.
- كنوز رياض الصالحين، لحمد بن ناصر العمار، دار كنوز إشبيليا- الطبعة الأولى، 1430ه.
- شرح رياض الصالحين، للشيخ محمد بن صالح العثيمين، مدار الوطن، الرياض، 1426هـ.
-التَّنويرُ شَرْحُ الجَامِع الصَّغِيرِ، محمد بن إسماعيل الصنعاني، محمَّد إسحاق محمَّد إبراهيم، مكتبة دار السلام، الرياض، الطبعة الأولى، 1432هـ - 2011م.
- نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، تأليف مصطفى سعيد الخن - مصطفى البغا - محي الدين مستو-علي الشربجي- محمد أمين لطفي- مؤسسة الرسالة، بيروت –لبنان، الطبعة الرابعة عشرة.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَا أَبَا سَعِيدٍ، مَنْ رَضِيَ بِاللهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا، وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ»، فَعَجِبَ لَهَا أَبُو سَعِيدٍ، فَقَالَ: أَعِدْهَا عَلَيَّ يَا رَسُولَ اللهِ، فَفَعَلَ، ثُمَّ قَالَ: «وَأُخْرَى يُرْفَعُ بِهَا الْعَبْدُ مِائَةَ دَرَجَةٍ فِي الْجَنَّةِ، مَا بَيْنَ كُلِّ دَرَجَتَيْنِ كَمَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ»، قَالَ: وَمَا هِيَ يَا رَسُولَ اللهِ؟ قَالَ: «الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ، الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake amesema-: "Ewe baba Saidi, yeyote atakayeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammadi kuwa ni Nabii, basi atakuwa kastahiki Pepo", Abuu Saidi likamshangaza sana hilo, akasema: Naomba uyarudie tena maneno hayo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akarudia, kisha akasema: "Na la mwisho mja ananyanyuliwa kwalo daraja katika Pepo, umbali ulio kati ya daraja mbili hizo ni kama baina ya mbingu na ardhi", Akasema: Ni lipi hilo ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alimueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake kwamba yeyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na akamridhia kuwa Mola na Mungu na mmiliki na mtukufu na muamrishaji, na Uislamu kuwa ni dini, kwa kutii na kujisalimisha katika amri zake zote na makatazo yake yote, na Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni Nabii, kwa yote aliyotumwa kwayo na akayafikisha; itamthibitikia kwake Pepo, Abuu Saidi akastaajabu radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Yarudie tena ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akafanya hivyo, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na nina jambo jingine ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu humnyanyua mja daraja mia moja Peponi kwalo, masafa yaliyoko kati ya daraja mbili hizo ni kama umbali ulioko baina ya mbingu na ardhi, akasema Abuu Saidi: Na nilipi hilo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ni kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Miongoni mwa mambo yanayopelekea kuingia peponi ni kuridhia kuwa Allah ndiye mola na Uislamu kuwa ni dini na Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni Nabii.
- Kutukuzwa swala la Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kunyanyuliwa kwa daraja ya Jihadi Peponi.
- Peponi kuna daraja nyingi zisizohesabika, na nyumba zisizohesabika, na wapiganaji watakuwa na daraja mia moja ndani yake.
- Mapenzi ya Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kutaka kujua kheri, na milango yake na sababu zake.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1501) (1884).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 910).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 423).
النهاية في غريب الحديث والأثر، لابن الأثير (5/ 153).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي قتادة الحارث بن رِبْعِيِّ رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم : أَنَّهُ قامَ فيهم، فذكرَ لهم أَنَّ الجهادَ في سبيلِ اللهِ، والإيمانَ باللهِ أفضلُ الأعمالِ، فقامَ رَجُلٌ، فقال: يا رسولَ اللهِ، أرأيتَ إن قُتِلْتُ في سبيلِ اللهِ، تُكَفَّرُ عَنِّي خَطَايَايَ؟ فقالَ له رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : «نعم، إنْ قُتِلْتَ في سبيلِ اللهِ، وأنتَ صَابِرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيْرُ مُدْبِرٍ». ثم قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : «كَيْفَ قُلْتَ؟» قال: أَرَأَيتَ إنْ قُتِلْتُ في سَبِيلِ اللهِ، أَتُكَفَّرُ عَنِّي خَطَايَايَ؟ فقالَ له رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : «نعم، وأنتَ صَابِرٌ مُحْتَسِبٌ، مُقْبِلٌ غَيْرُ مُدْبِرٍ، إلا الدَّيْنَ؛ فَإنَّ جِبْرِيلَ -عليه السلام- قالَ لِي ذَلِكَ».
Kutoka kwa Abii Qatada Haritha bin Ribiy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye alisimama kati yao, akawaeleza kuwa kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kumwamini Mweyezi Mungu ndio matendo bora, akasimama bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia: "Ndiyo, ikiwa utauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu na wewe ukiwa ni mwenye subira na kutaraji malipo ukiwa mstari wa mbele pasi na kurudi nyuma" Kisha akasema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- "Umesema vipi?" Akasema: Hivi unaonaje ikiwa nitauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu, je yatafutwa makosa yangu? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia: "Ndiyo, ikiwa utauwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu na wewe ukiwa ni mwenye subira na kutaraji malipo ukiwa mstari wa mbele pasina kurudi nyuma, isipokuwa deni; kwani Jibrili ziwe juu yake Amani kanieleza hivyo mimi".
Imepokelewa na Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alisimama Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kati ya maswahaba kwaajili ya kuwahutubia, akawaeleza kuwa kupigana jihadi kwaajili ya kulinyanyua jina la Mwenyezi Mungu na kumuamini Mwenyezi Mungu ndiyo matendo bora, akasimama bwana mmoja akamuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Hivi unaonaje kama nitauwawa kwaajili ya kulinyanyua jina la Mwenyezi Mungu je nitasamehewa mimi madhambi yangu?, akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Ndiyo, lakini kwa sharti uwe umeuwawa ukiwa na subira na uvumilivu kwa yale yaliyokupata, ukitakasa nia kwaajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bila kukimbia kiwanja cha vita, kisha akakumbuka Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kitu, nacho ni deni, akakumbusha kuwa jihadi na shahada havifuti haki za wanadamu.
Marejeo
دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين، لابن علان، نشر دار الكتاب العربي.
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، نشر: مؤسسة الرسالة، الطبعة: الرابعة عشر، 1407هـ - 1987م.
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، للهلالي، نشر: دار ابن الجوزي. الطبعة الأولى 1418هـ.
المعجم الوسيط، نشر: دار إحياء التراث العربي، بيروت، لبنان، الطبعة: الثانية.
صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، نشر: دار إحياء التراث العربي، بيروت.
تطريز رياض الصالحين، تأليف فيصل آل مبارك، تحقيق د. عبد العزيز آل حمد، دار العاصمة-الرياض، الطبعة الأولى، 1423هـ.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن ابن عباس رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «ما مِنْ أيَّامٍ العمَلُ الصَّالِحُ فيها أحبُّ إلى اللهِ مِن هذه الأيام» يعني أيامَ العشر، قالوا: يا رسُولَ الله، ولا الجهادُ في سبيلِ الله؟ قال: «ولا الجهادُ في سبيلِ الله، إلا رجلٌ خَرَجَ بنفسِه ومالِه فلم يَرْجِعْ من ذلك بشيءٍ».
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao na baba yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna siku ambazo matendo mema yanapendeka zaidi ndani yake kwa Mwenyezi mungu kuliko siku hizi" Yaani: Siku kumi (za mwanzo wa Dhul-Hija), Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa mtu aliyetoka kwa nafsi yake na mali yake na hakurudi na chochote katika hivyo".
Imepokelewa na Bukhari na Abu Daud na matamshi ya hadithi ni yakeDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa amali njema ndani ya siku kumi za mwanzo wa mwezi Dhul-Hija ni bora kuliko siku zingine.
Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kupigana Jihadi katika siku kumi hizi, je ni bora au kufanya matendo mema katika siku hizi? Kwakuwa linajulikana kwao kuwa Jihadi ni amali bora.
Akajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Yakuwa amali njema ndani ya siku hizi ni bora kuliko Jihadi katika siku zingine, isipokuwa mtu aliyetoka Jihadi na akaihatarisha nafsi yake na mali yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, akapoteza mali yake na ikatoka roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu, Hiki ndicho kilicho bora kuliko amali njema ndani ya siku hizi bora.
Mafunzo
- Ubora wa matendo mema katika siku kumi za Dul-Hija, ni juu ya muislamu atumie fursa ya siku hizi na azidishe ibada ndani yake, kama kumtaja Allah Mtukufu, na kusoma Qur'ani, na takbiri (Allahu Akbar) na tahlil (Laa ilaaha illa llaah) na tahmidi (Alhamdulillaah), na swala na sadaka na swaumu, na amali zote njema.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 20) (969).
سنن أبي داود (4/ 102) (2438).
فتح الباري بشرح صحيح البخاري، لابن حجر (2/ 459).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل المبارك (ص699).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 301).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (1/ 884).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (15/ 234).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 382).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com