Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto

عَنْ أَبِي عَبْسٍ عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنِ جَبْرٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا اغْبَرَّتْ قَدَمَا عَبْدٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَتَمَسَّهُ النَّارُ».
Kutoka kwa Abuu Absi Abdulrahman bin Jabri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimbashiria yeyote itakayepatwa na vumbi miguu yake huku akiwa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa moto hautomgusa.

Mafunzo
  1. Habari njema kwa mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ya kuokoka na moto.
  2. Ametaja miguu miwili pamoja nakuwa vumbi huenea mwili mzima; kwa sababu wapigana ji wengi katika zama hizo walikuwa watembea kwa miguu, na miguu hupata vumbi kwa namna yoyote ile.
  3. Amesema bin Hajari: Ikiwa kitendo cha kuguswa na vumbi pekee kinaharamisha kuguswa na moto; vipi kwa atakayekwenda mbio na akatoa juhudi na akapoteza muda wake.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 20) (2811)، (2/ 7) (907). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 424). التنوير شرح الجامع الصغير، للصنعاني (7/ 361). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 437). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 911).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Fadhila za Jihadi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com