Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji kwa wema katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana
Kutoka kwa Zaidi bin Khalid radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji kwa wema katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayemuandalia mwenye kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu sababu za safari yake na anachohitaji katika silaha muhimu, vipando, chakula, gharama na vitu vingine; basi yuko katika nafasi sawa na mpiganaji, na atapata malipo ya mpiganaji.
Na atakayesimamia jambo la mpiganaji kwa wema, na akakaa badala yake katika kulea familia yake wakati asipokuwepo basi naye yuko katika hukumu ya mpiganaji.
Mafunzo
Hili ni himizo kwa waislamu kusaidizana katika heri.
Amesema bin Hajar: Katika Hadithi hii kuna himizo la kuwafanyia wema wale wanaowafanyia wema Waislamu, au kutekeleza moja ya wajibu wao.
Kanuni ya jumla nikuwa: Yeyote anayemsaidia mtu katika kumtii Mwenyezi Mungu atapata malipo sawa na malipo yake, bila ya kupunguzwa ujira wake hata kidogo.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 27) (2843).
صحيح مسلم (3/ 1506) (1895).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 267).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص143).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 588).
لسان العرب، لابن منظور (15/ 123).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 374).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 202).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com