Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adh-kaar - zisomwazo- wakati wa swala.

Hadithi 14

Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدْعُو وَيَقُولُ: «اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ، وَمِنْ عَذَابِ النَّارِ، وَمِنْ فِتْنَةِ المَحْيَا وَالمَمَاتِ، وَمِنْ فِتْنَةِ المَسِيحِ الدَّجَّالِ». وفِي لَفْظٍ لِمُسْلِمٍ: «إِذَا فَرَغَ أَحَدُكُمْ مِنَ التَّشَهُّدِ الْآخِرِ، فَلْيَتَعَوَّذْ بِاللهِ مِنْ أَرْبَعٍ: مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ، وَمِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَمِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ، وَمِنْ شَرِّ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba akisema: "Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na adhabu ya moto, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo manne, baada ya tashahudi ya mwisho na kabla ya swala, na akatuamrisha tuombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na mambo hayo, Jambo la kwanza: Kuomba kinga kutokana na adhabu za kaburi. Jambo la pili: Kuomba kinga ya kuepukana na adhabu ya moto siku ya Kiyama. La tatu: Kuomba kinga itokanayo na fitina za uhai ikiwemo matamanio ya dunia yaliyoharamishwa na ikiwemo pia shub-ha (utata) wenye kupoteza, na kutokana na fitina za mauti, yaani muda wa kukata roho, tusije kupinda tukatoka katika Uislamu au Sunna, au fitina za kaburini kama maswali ya Malaika wawili. Jambo la nne:Kuomba kinga zitokanazo na fitina za Masihi Dajali atakeyetokea zama za mwisho, Mwenyezi Mungu atawapa mtihani waja wake kupitia yeye; na Mtume kamtaja kwa jina kutokana na ukubwa wa fitina zake.

Mafunzo
  1. Ombi hili la kinga ni miongoni mwa dua muhimu na ni dua inayokusanya mambo mengi, kwakuwa imekusanya kuomba kinga dhidi ya shari za Duani na Akhera.
  2. Kuthibiti uwepo wa adhabu za kaburi nakuwa adhabu hizo ni kweli.
  3. Uhatari wa fitina na umuhimu wa kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu na kuomba dua ya kusalimika nazo.
  4. Kuthibitika kutokea kwa Dajali na ukubwa wa fitina zake.
  5. Sunna ya kusoma dua hii baada ya tashahudi ya mwisho.
  6. Sunna ya kuomba dua baada ya matendo mema.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 99) (1377). صحيح مسلم (1/ 412) (588). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 172). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص212). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص96).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِذَا كَبَّرَ فِي الصَّلَاةِ، سَكَتَ هُنَيَّةً قَبْلَ أَنْ يَقْرَأَ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ بِأَبِي أَنْتَ وَأُمِّي أَرَأَيْتَ سُكُوتَكَ بَيْنَ التَّكْبِيرِ وَالْقِرَاءَةِ، مَا تَقُولُ؟ قَالَ «أَقُولُ: اللهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللهُمَّ اغْسِلْنِي مِنْ خَطَايَايَ بِالثَّلْجِ وَالْمَاءِ وَالْبَرَدِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema “Allahu Akbar” kwa ajili ya swala, alikuwa akitulia kidogo kabla ya kusoma Al-Fatiha, ambamo alikuwa akiianza Swala yake kwa baadhi ya dua, miongoni mwa dua hizo zilizoripotiwa ni kauli yake: "Allaahumma baaid bainii wa baina khatwaa yaaya, kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi, Allaahu naqinii min khatwaayaaya, kamaa yunaqqah-thaubal abyadhwa minad-danasi, Allaahuma gh-silnii bil maai wath-thalji wal baradai", Hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amtenge mbali na madhambi ili asije akaangukia ndani yake, hata kusiwe na kukutana nayo, kama vile hakuna kukutana baina ya Mashariki na Magharibi, na ikitokea katumbukia ndani yake, basi amtakase kutokana na madhambi hayo kama uchafu unavyotolewa kwenye nguo nyeupe, na amuoshe dhambi zake na kuupoza miale na joto lake, kwa vitakatishi hivi baridi; Maji, theluji na baridi.

Mafunzo
  1. Kuificha dua ya ufunguzi wa swala, hata kama swala itakuwa ni ya kusoma kwa sauti.
  2. Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kutaka kujua hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika harakati zake na kutulia kwake.
  3. Zimekuja namna nyingine za dua ya ufunguzi, na kilicho bora kwa mtu afuatilie dua zilizokuja na kuthibiti kutoka kwake rehema na amani ziwe juu yake, ili asome hii wakati mwingine, na hii wakati mwingine.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 149) (744). صحيح مسلم (1/ 419) (598). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 118). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص143). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 186).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako

عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رضي الله عنه: أَنَّ رَسُولَ صَلَّى عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخَذَ بِيَدِهِ، وَقَالَ: «يَا مُعَاذُ، وَاللَّهِ إِنِّي لَأُحِبُّكَ»، فَقَالَ: «أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ لَا تَدَعَنَّ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ تَقُولُ: اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ».
Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".
Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alishika mkono wa Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Wallahi hakika mimi ninakupenda, na ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha kusema mwisho wa kila swala: Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukutaja, katika kila kauli na kitendo kinachoniweka karibu na utiifu, "na kukushukuru" kwa kutimia neema na kuzuia mabaya, "na kuzifanya vizuri ibada zako" kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Mafunzo
  1. Sheria ya kumueleza mtu kuwa unampenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
  2. Inapendeza kuomba dua hii mwisho wa kila swala ya faradhi na ya sunna.
  3. Katika kuomba kwa matamshi haya machache kuna mahitaji yote ya Dunia na Akhera
  4. Katika faida za kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kuusiana katika na kupeana nasaha katika mambo mema na uchamungu.
  5. Amesema Attwayibi: Kumtaja Mwenyezi Mungu ni utangulizi wa kukunjua kifua, na kumshukuru ni njia ya kuzilinda neema, na kuzifanya vizuri ibada ni kujiweka mbali na yote yanayomshughulisha mtu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 630) (1522). سنن النسائي (3/ 53) (1303). مسند أحمد (36/ 429) (22119). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 450). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص259). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 264). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 284). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 353).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako

عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: فَقَدْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيْلَةً مِنَ الْفِرَاشِ فَالْتَمَسْتُهُ فَوَقَعَتْ يَدِي عَلَى بَطْنِ قَدَمَيْهِ وَهُوَ فِي الْمَسْجِدِ وَهُمَا مَنْصُوبَتَانِ، وَهُوَ يَقُولُ: «اللهُمَّ أَعُوذُ بِرِضَاكَ مِنْ سَخَطِكَ، وَبِمُعَافَاتِكَ مِنْ عُقُوبَتِكَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْكَ لَا أُحْصِي ثَنَاءً عَلَيْكَ أَنْتَ كَمَا أَثْنَيْتَ عَلَى نَفْسِكَ».
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja nyakati za usiku nilimkosa kitandani Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikaanza kumtafuta ukaangukia mkono wangu ndani ya nyayo zake zikiwa zimesimamishwa akiwa ndani ya msikiti, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anasema Aisha radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nimelala pembezoni mwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamkosa wakati wa usiku, nikagusa kwa mkono wangu sehemu aliyokuwa akiswalia ndani ya chumba; ghafla nikamuona amesujudu na miguu yake ikiwa imesimamishwa, mara nikamsikia akisema: "Ninajilinda" Na ninapitia "Katika radhi zako dhidi ya hasira zako" juu yangu au juu ya umma wangu, "na" ninaomba kinga "kwa salama yako" na msamaha wako mwingi "kutokana na adhabu zako", "na ninajilinda kwako kutokana nawe" na kwa sifa za uzuri wako kutokana na sifa za utukufu wako, kiasi kwamba hakuna awezaye kukinga dhidi yako ila wewe, hakuna pa kusalimika wala pa kujilinda kutokana na Mwenyezi Mungu ila kwake, "Siwezi kuzihesabu sifa zako" Sina uwezo wala siwezi kufikia kuzidhibiti na kuzihesabu kwa idadi kwa kushindwa kwangu kuzidhibiti kwa wingi neema zako na ihisani yako kama unavyostahiki, hata kama nikijitahidi katika hilo, "Wewe kama ulivyoisifia nafsi yako" wewe ndiye uliyeisifu dhati yako sifa zinazokustahiki, ni nani awezaye kutimiza haki ya sifa zako?!

Mafunzo
  1. Sunna ya kuomba dua hii katika sijida.
  2. Amesema Miriki: Na katika moja kati ya riwaya za Nasaai: Alikuwa akisema dua hii anapomaliza swala yake na akaelekea kitandani kwake.
  3. Sunna ya kumsifia Mwenyezi Mungu kwa sifa zake na kumuomba kwa majina yake yaliyothibiti katika Qur'ani na Sunna.
  4. Hapa kuna kumtukuza muumba wakati wa kurukuu na kusujudu.
  5. Inafaa kuomba ulinzi kupitia sifa za Mwenyezi Mungu, kama ambavyo inafaa kuomba ulinza kupitia dhati yake Yeye Aliyetakasika na kutukuka.
  6. Amesema Al-Khattwabi: Katika maneno haya kuna maana ya ndani sana, nayo: Nikuwa aliomba kinga kwa Mwenyezi Mungu amkinge kupitia radhi zake kutokana na hasira zake, na kwa salama yake dhidi ya adhabu zake, na ridhaa na hasira ni maneno mawili tofauti yanayokwenda sambamba, vile vile kusalimika na kuadhibiwa pia, alipofikia kumtaja ambaye hana kinyume chake ambaye ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka alitaka kinga kutokana na Yeye kwake mwenyewe na si kwa mwingine, na maana yake: Ni kuomba msamaha dhidi ya mapungufu ya kutofikia wajibu wa haki stahiki katika kumuabudu, na kumtukuza. Na kauli yake: Sizidhibiti sifa juu yako: Yaani sina uwezo wala siwezi kuzifikia.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 352) (486). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص781). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 510). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين 2/ 979). طريق الهجرتين وباب السعادتين، لابن قيم الجوزية (ص136).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا صَلَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلاَةً بَعْدَ أَنْ نَزَلَتْ عَلَيْهِ: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالفَتْحُ} [النصر: 1] إِلَّا يَقُولُ فِيهَا: «سُبْحَانَكَ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي». وعَنْها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ فِي رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ: «سُبْحَانَكَ اللهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللهُمَّ اغْفِرْ لِي» يَتَأَوَّلُ الْقُرْآنَ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)". Na kutoka kwa Aisha amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha kusema katika rukuu yake na sijida yake: "Sub-haanaka llaahumma Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii" Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi, na sifa njema ni zako, ewe Mola wangu Mlezi nisamehe" Akiifasiri Qur'ani.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipoteremshiwa juu yake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" Akaifasiri Qur'ani na akaanza kuitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: "Basi zitakase sifa za Mola wako Mlezi na umuombe msamaha", akawa akikithirisha kusema katika rukuu zake na sijida zake wakati wa swala: "Umetakasika" Na ni kukutakasa wewe dhidi ya kila mapungufu yale yasiyokufaa, "Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako" Kwa sifa nzuri kwako kwa ukamilifu wa dhati yako na sifa zako na matendo yako, "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe" na zifute kwangu dhambi zangu, na uziachilie mbali.

Mafunzo
  1. Kupendeza kukithirisha dua hii katika rukuu na sijida.
  2. Kuomba msamaha mwisho wa umri kuna angalizo la kuhitimisha ibada zote namna hiyo, na hasa hasa swala kwa kuomba msamaha, ili azibe yale yaliyojitokeza ndani yake miongoni mwa mapungufu.
  3. Jambo zuri linalotumika kukubaliwa dua kupitia jambo hilo ni kutaja mazuri yake na sifa zake, na kumtakasa dhidi ya mapungufu na aibu.
  4. Fadhila ya kuomba msamaha, na kuutafuta katika kila hali.
  5. Ukamilifu wa utumwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutekeleza kwake amri ya Mwenyezi Mungu.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 178) (4968، 4967). صحيح مسلم (1/ 350-351) (484). تيسير العلام، للبسام (ص214). تنبيه الأفهام، للعثيمين (2/ 278). الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص263). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 176). خلاصة الكلام، فيصل المبارك (ص97).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema?

عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى قَالَ: لَقِيَنِي كَعْبُ بْنُ عُجْرَةَ، فَقَالَ: أَلاَ أُهْدِي لَكَ هَدِيَّةً؟ إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَرَجَ عَلَيْنَا، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَدْ عَلِمْنَا كَيْفَ نُسَلِّمُ عَلَيْكَ، فَكَيْفَ نُصَلِّي عَلَيْكَ؟ قَالَ: «فَقُولُوا: اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ، اللَّهُمَّ بَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ، كَمَا بَارَكْتَ عَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ، إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ».
Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? Akasema: "Basi semeni: Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammadi na juu ya watu wa Muhammadi, kama ulivyompa rehema Ibrahim na juu ya watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa, ewe Mwenyezi Mungu shusha baraka juu ya Muhammad na juu ya watu wa Muhammad, kama ulivyoteremsha baraka kwa watu wa Ibrahim, hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Masahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu namna ya kumtakia rehema? baada ya kujua kwao namna kumuombea amani (salam) katika kikao cha tahiyatu ndani ya swala: "Amani iwe juu yako ewe Nabii na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake...?" Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akawaeleza namna ya kumtakia rehema, na maana yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mpe rehema Muhammad na juu ya watu wa Muhammad" Yaani: Mtaje kwa sifa nzuri kwa Malaika walioko juu mbinguni, na juu ya wafuasi wake katika dini yake, na waumini katika ndugu zake wa karibu. "Kama ulivyoteremsha rehema juu ya watu wa Ibrahim" Kama ulivyotoa takrima juu ya watu wa Ibrahim amani iwe juu yake, nao ni Ibrahim na Ismail na Is'haka na kizazi chake na wafuasi wao miongoni mwa waumini, basi zipeleke fadhila zako kwa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake. "Hakika wewe ni mhimidiwa mwenye kutukuzwa". Yaani: Mwenye kuhimidiwa katika dhati yako na sifa zako na vitendo vyako, mpana katika utukufu wako na ugawaji riziki wako. "Ewe Mwenyezi Mungu teremsha baraka kwa Muhammad na juu ya watu wa Muhammad kama ulivyoteremsha baraka juu ya watu wa Ibrahim" Yaani: Mpe katika kheri na karama zile zilizo kubwa zaidi na uzizidishe na umdumishie kheri hizo.

Mafunzo
  1. Wema waliotangulia walikuwa wakizawadiana kuhusu mambo ya elimu.
  2. Uwajibu wa kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika tashahudi ya mwisho katika swala.
  3. Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwafundisha Masahaba wake kumtakia amani na rehema juu yake.
  4. Namna hii ya kuomba ndio namna sahihi zaidi katika kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 77) (6357). صحيح مسلم (1/ 305) (406). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص208). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 270). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 170).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala

عَنْ ‌أَبِي الزُّبَيْرِ قَالَ: كَانَ ‌ابْنُ الزُّبَيْرِ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ حِينَ يُسَلِّمُ: «لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، ‌وَلَا ‌نَعْبُدُ ‌إِلَّا إِيَّاهُ، لَهُ النِّعْمَةُ وَلَهُ الْفَضْلُ وَلَهُ الثَّنَاءُ الْحَسَنُ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ» وَقَالَ: «كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُهَلِّلُ بِهِنَّ دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ».
Kutoka kwa Abuu Zubairi amesema: Alikuwa bin Zubairi akisema mwisho wa kila swala anapotoa salamu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul-hamdu wahuwa a'laa kulli shai-in qadiir, Laa haula walaa quwwata illaa billaah, Laa ilaaha illa llaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun-ni'matu walahul-fadhlu walahuth-thanaaul hasan, Laa ilaaha illa llaahu Mukhliswiina lahud-diina walau karihal kaafiruun" Na akasema: "Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akinyanyua sauti baada ya salamu ya kila swala ya faradhi kwa dhikri hii tukufu, na maana yake: "Laa ilaaha illa llaahu": Yaani: Hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. "Wah-dahu Laa shariika lahu" Yaani: Hana ushirika katika Uungu wake na Uumbaji wake na Majina yake na Sifa zake. "Lahul Mulku" Yaani: Ana Ufalme usio na mipaka mpana na ulioenea kila kitu, Ufalme wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo. "Walahul-hamdu" Yaani: Yeye ndiye anasifika kwa ukamilifu usio na kikomo, mwenye kusifika kwa ukamilifu na kwa kupendwa na kutukuzwa kwa hali zote, katika furaha na majonzi. "Wahuwa alaa kulli shai-in qadiir": Uwezo wake umekamilika na umetimia kwa namna zote, hakimshindi kitu, na hakuna jambo lolote linalokataa katika mambo yote. "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah" Yaani: Hakuna kugeuka kutoka hali moja kwenda nyingine, na kutoka katika kumuasi Mwenyezi Mungu kuja katika kumtii, na hakuna nguvu ila ni kwa Mwenyezi Mungu Yeye ndiye msaidizi na kwake ndiko kwa kutegemewa. "Laa ilaaha illa llaah, walaa na'budu illa iyyaah": (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na hatumuabudu yeyote ila Yeye) Huu ni msisitizo wa maana ya Uungu na kukemea shirki, nakuwa hakuna anayestahiki kuabuduiwa zaidi yake. "Lahun-ni'matu wal fadhlu: (Ni mmiliki wa neema na fadhila) Yeye ndiye anaumba neema na kuzimiliki, na humfadhilisha amtakaye katika waja wake. "Walahuth thanaaul hasan" (Na ni zake sifa nzuri): Juu ya dhati yake na sifa zake na matendo yake na neema zake, na kwa kila hali. "Laa ilaaha illa llahu, Mukhliswiina lahud-diin: Hapana Mola mwingine isipokuwa Yeye, tunamtakasia Yeye matendo yote: Yaani: Tunampwekesha si kwa kutaka kujionyesha wala kutaka kusikika katika kumtii Mwenyezi Mungu. "Walau karihal kaafiruun", (Hata kama makafiri watachukia) Yaani: Tumethubutu katika kumpwekesha Mwenyezi Mungu na ibada zake hata kama makafiri watachukia.

Mafunzo
  1. Sunna ya kudumu na adhkari za baada ya swala za faradhi.
  2. Muislamu hujifaharisha kwa dini yake, na hudhihirisha nembo zake, hata kama makafiri watachukia.
  3. Linapokuja katika hadithi neno: "Mwisho wa swala", Ikiwa kilichotajwa ndani ya hadithi ni dhikri, basi asili yake hapa ni baada ya salamu, na ikiwa ni dua inakuwa kabla ya salamu ndani ya swala.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 415) (594). سبل السلام شرح بلوغ المرام، للصنعاني (1/ 293). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 61). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 973). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 499). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (2/ 762). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 492).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)

عَنْ كَعْبِ بْنِ عُجْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مُعَقِّبَاتٌ لَا يَخِيبُ قَائِلُهُنَّ -أَوْ فَاعِلُهُنَّ- دُبُرَ كُلِّ صَلَاةٍ مَكْتُوبَةٍ، ثَلَاثٌ وَثَلَاثُونَ تَسْبِيحَةً، وَثَلَاثٌ وَثَلَاثُونَ تَحْمِيدَةً، وَأَرْبَعٌ وَثَلَاثُونَ تَكْبِيرَةً».
Kutoka kwa Ka'b Bin Ujrah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Adhkari (Dua) hatopata hasara wala kujuta msemaji wake, bali maneno haya yanathawabu, na yanakuja kwa kufuatana, na husemwa baada ya swala za faradhi, nayo ni: "Sub-haana llaah" -Ametakasika Mwenyezi Mungu- mara thelathini na tatu, yaani ametakasika Mtukufu na kila mapungufu. "Na Alhamdulillaah" Mara thelathini na tatu, nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza. "Allaahu Akbaru" Mara thelathini na nne, Mwenyezi Mungu ni mkubwa mno na ni Mtukufu na Mwenye nguvu kuliko kila kitu.

Mafunzo
  1. Fadhila za kusema Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Allaahu Akbar, maneno haya ndio mema yenye kubakia.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 418) (596). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 501). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 976). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (2/ 766). تيسير العلام، للبسام (ص227). فيض القدير شرح الجامع الصغير، لزين الدين المناوي (5/ 525).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 14
Hadithi 14
  1. Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali
  2. Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi
  3. usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako
  4. Ewe Mwenyezi Mungu ninajilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, na salama yako dhidi ya adhabu zako, na ninajilinda kwako kutokana nawe, siwezi kuzidhibiti sifa zako kwa idadi maalum kama ambavyo wewe ulivyoisifu nafsi yako
  5. Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)
  6. Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema?
  7. Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitoa tahlil (Laa ilaaha illa llaah) kwa maneno haya mwisho wa kila swala
  8. Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)
  9. Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kati ya sijida mbili: "Allaahumma ghfir lii, warhamnii, wa aafiniii, wahdinii, warzuqniii
  10. Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam
  11. Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila swala mara thelathini na tatu (33), na akamhimidi Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu (33), na akamtukuza Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, hizo ni tisini na tisa (99) Na akasema ili kukamilisha mia moja (100): Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul hamdu, wahuwaa'laa kulli shai in qadiir, basi yatasamehewa madhambi yake, hata kama yalikuwa na wingi mfano wa povu la Bahari
  12. Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa
  13. Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah
  14. Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikua akisema mwishoni mwa kila swala ya faradhi

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com