Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam

عن ثَوْبَانَ رضي الله عنه قال: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا انْصَرَفَ مِنْ صَلَاتِهِ اسْتَغْفَرَ ثَلَاثًا، وَقَالَ: «اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلَامُ، وَمِنْكَ السَّلَامُ، تَبَارَكْتَ ذَا الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ»، قَالَ الْوَلِيدُ: فَقُلْتُ لِلْأَوْزَاعِيِّ: كَيْفَ الْاسْتِغْفَارُ؟ قَالَ: تَقُولُ: أَسْتَغْفِرُ اللهَ، أَسْتَغْفِرُ اللهَ.
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapoondoka katika swala yake anaomba msamaha mara tatu, na anasema: "Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam", Anasema Walid: Nikasema kumwambia Auzaiy: Ni vipi unaomba msamaha: Akasema: Unasema: Astagh-firullaah, Astagh-firullaah.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema anapomaliza swala yake: Astagh-firullaah, Astagh-firullaah, Astagh-firullaah. Kisha anamtukuza Mola wake Mlezi kwa kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni amani, na amani inatoka kwako, umetukuka ewe mwenye utukufu na ukarimu" Mwenyezi Mungu aliyesalimika na kukamilika katika sifa zake, aliyetakasika na kila aibu na mapungufu, na unaomba kutoka kwake Mtukufu amani kutokana na shari za dunia na akhera na si kwa mwingine asiyekuwa yeye, naye Mtukufu kheri zake ni nyingi duniani na akhera, mwenye utukufu na wema na ihisani.

Mafunzo
  1. Sunna ya kuomba msamaha baada ya swala na kudumu nazo.
  2. Sunna ya kuomba msamaha ili kuziba mapungufu ndani ya ibada na kuipa nguvu ibada na uzembe uliojitokeza ndani yake.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 414) (591). مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعبيد الله المباركفوري (3/ 317). سبل السلام، للصنعاني (1/ 294). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 301).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adh-kaar - zisomwazo- wakati wa swala.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com